Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu
Pro dikteta.

Nchi bila demokrasia kwa Afrika ni hakuna kitu. Rushwa na ufisadi ndio ngao ya vyama tawala.

Huyo Jpm alitupuga 1.5T huku akijiita Mzalendo
Tofautisha udikteta na nidhamu.

Serikali iliyopo madarakani ina mandate ya kufanya maamuzi ya kisera.

Lenye wengi hakuna maamuzi yenye kuwafurahisha wote popote duniani.

Ni haki ya watu kukosoa au hata kupinga on merit; lakini hawana haki ya kusema lazima wazuie kwa sababu tu hawakubali.

Sasa ikifikia hatua watu wanakutishia nyau, vyombo vya ulinzi vinafanya majukumu yao; halafu wewe kiongozi unatetemeka na pressure za media au sijui taasisi uchwara na kuingilia kazi zao unajitafutia matatizo.

We unadhani huko ulaya wangekuwa wanajali sana eco-warriors, sijui environmentalists na arguments zao tena zina nguvu; North Sea na Gulf of Mexico mafuta na gas yasingechimbwa.

Nimekupa mifano ya hayo maeneo mawili hapo juu maana yapo nchini U.K. na US kwenye jamii ya watu wenye midomo mirefu kama chuchunge na kujifanya wanajua kila kitu na wana majawabu ya kila kitu. Serikali zao ingekuwa inawasikiliza hakuna vitu vya maana wangefanya.

Piga kelele wewe siku kazi ikianza ilimradi ni maamuzi ya serikali wapingaji awataki kuelewa somo sijui wapo wapi wana protest. Jamaa wakiingia watu wanasombwa na polisi kama mifugo vile si kwa sababu wametumwa na wanasiasa ila wanatekeleza majukumu yao.

IGP keshasema jeshi la polisi halina shida na kupinga hoja za bandari hila wabaki kwenye mistari hiyo habari za kujifanya unatishia serikali na kutoa ultimatums huko sasa ni kununua ugomvi na polisi.

Sasa sijui mpuuzi gani huko serikalini kapindua maamuzi. Nchi ya kuchekeana chekeana sana ndio maana watanzania hawana discipline kabisa popote duniani ukikutana nao wao kila kitu poa; matatizo haya msingi wake ni serikali isiyoweka culture ya watu kuweza kuheshimu mipaka ya wengine kwenye jamii, makazini mpaka serikalini.

Hovyo kweli
 
Ujinga mtupu, yaan Hadi mahakama inashangaaa ,mahakama inakubali madhaifu makubwa ya Mkataba

Alafu lijinga limoja ma wahuni wenzio kisa ni wavaa visuruali vifupi, ndio uone Mkataba uko sawa...
Wakati tundu lissu na mbowe wanadai haki zao mlisema mahamaka zetu hazina haki.

Leo mahakama hio hio imekuwa inajali haki za raia!

Hivi nyie viumbe lini mtaamka na kumtambua ADUI WA HAKI ZENU?
 
We umeuona huo mkataba?

au unabeba tu story km zile story za ibada za weekend ambazo hao watoa story hawaruhusu hata wana kondoo kuuliza maswali
Ni mkataba wa maajabu sana kiasi uniulize kama nimeuona?
 
Usikute hata mkataba wenyewe hawajausoma wala hawahujui cha ajabu eti nao wanatoa tamko. ila dini hizi...mmmh!! Basi tu
Na wewe umelisoma kweli tamko hili mpaka mwisho au umesoma heading tu kama ilivyo kawaida yenu na kutoa hukumu?

Kwa maelezo haya unadhani yametoka kwa watu wasiosoma na ambao hawaujasoma mkataba wenyewe kabla hawajaamua?

I really feel very sorry for you..
 
Nilikuwa nakuona una akili ila nimegundua kuwa wewe ni mjinga sana? Kwa hiyo unataka kusema kuwa Tanzania inaongozwa na Roma?

China nako Roma wakisema wamesema?

..kama Maza anawapenda sana Dp World basi mshaurini awalete kama Ticts ya kina Karamagi.

..lakini mkataba unaotulazimsha mpaka tubadili sheria zetu, tena tulizoandika juzi tu 2017, unatia mashaka makubwa na haukubaliki.
 
Wakati tundu lissu na mbowe wanadai haki zao mlisema mahamaka zetu hazina haki.
Leo mahakama hio hio imekuwa inajali haki za raia!
Hivi nyie viumbe lini mtaamka na kumtambua ADUI WA HAKI ZENU?
Tatizo hujielewiz unaruka ruka na Kila jambo ili mradi tu ulete tafuran za kijihadi..


Jikite kwenye lililopo mbele Kwa Sasa

Oyaa Nchi hii waislam ni wachache mnooooooooooo yaan ni wachache mnoo.
 
..kama Maza anawapenda sana Dp World basi mshaurini awalete kama Ticts ya kina Karamagi.

..lakini mkataba unaotulazimsha mpaka tubadili sheria zetu, tena tulizoandika juzi tu 2017, unatia mashaka makubwa na haukubaliki.
Mwambie
 
Wana JF.

Hili ni jukwaa pekee ambalo tunathubutu kusema ukweli wazi wazi.

Naamini kabisa kuna wanajukwaa humu wanaujua ukweli. Hebu tufunguke, kwanini viongozi wa Kanisa hasa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) wanapinga sana suala la serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushirikiana na Dubai kupitia Kampuni ya DP World katika uboreshaji na uendelezaji wa bandari zetu?

Kuna masilahi gani ambayo Kanisa linafaidika kupitia mfumo wa uendelezaji bandari uliopo sasa?

Kweli kabisa Great Thinkers wa Jamiiforums tunaamini viongozi wa Kanisa wamesukumwa na maoni ya wananchi? Kwamba Kanisa limeamua mpaka kutoa waraka kuhusu suala la bandari kwa sababu wananchi walio wengi hawataki?


[mention]FaizaFoxy [/mention] [mention]Pascal Mayalla [/mention] [mention]Lord denning [/mention][mention]JUMA JUMA [/mention]
 
Tatizo hujielewiz unaruka ruka na Kila jambo ili mradi tu ulete tafuran za kijihadi..
Sasa nani anae ruka ruka humu zaidi yako.
Issue ya waislamu kuwa wachache au wengi imetoka wapi?

Na kwa akili yako ilivyo finyu unadhani Wingi wa Pumba ndio uzito mkubwa?
Hizo ni Pumba tu. Chuma kidogo lkn damage yake ni kubwa kuliko pumba fuso nzima.

ONYESHA ubaya wa huo mkataba. Acha kujidai na wingi wa mapumba.
 
Mtanzania gani mwenye elimu yenye mashiko na asie mfia dini au mpenda wazungu ameukataa huu mkataba?
Usilete habari ya kina lissu na Huyo muhaini SLAAA au wale vibaraka wa wazungu ndani ya CCM.
KABLA Hujapinga kitu tumia muda kidogo kuisoma Profile ya hio Kampuni inayotaka kuwekeza hapa.

Hao ni Multi billion dollars company. Imewekeza kwenye bandari zaidi ya 40 na inafanya kazi hizo za bandari kwa miaka mingi kulikounavyofikiri wewe.

Jiulize. Je! Kampuni au nchi yenye sifa mbaya ya kukandamiza watu inawezaje KUKUBALIWA NA NCHI ZAIDI YA 40 DUNIANI KUWEKEZA KWAO?
Hiyo kampuni ni nzuri zaidi hata kuliko ulivyoieleza,ila kwenye mkataba kuna vipengele kadha wakadha k.m ilivyoelekezaa na TLS vinapaswa kurekebishwa
 
Tamko hilo limetolewa leo na Padri Kitime

Kwa Mujibu wa Padri kitime ,TEC imeamua kusimama na wananchi kwenye suala la bandari

Padri kitime amesisitiza kwa sasa serikali inataka kuligawa Taifa kwenye pande mbili wanaokubaliana na wasiokubaliana,lakini wengi wanaokubaliana wanahofi tu kwa kuwa wamepewa dhamana ya uongozi

Padri kitime amesisitiza kuwa wameita wataalamu wote mpaka watu wa wizara wamewaita hivyo wamejiridhisha kuwa mkataba wa serikali na Dp world haufai

TEC inashangazwa na serikali kutaka kuanza kuwazuia watu wasiongelee mambo ya Taifa lao

Padri kitime anahoji kama mkataba unafaa kwanini serikali inahangaika kutaka kubadili sheria lukuki ili ziendane na mkataba wa bandari na kumruhusu Dp world ya Dubai

======


"Ndugu zangu nawasihi mjihadhahari na wote wanaoleta mafarakano na vipingamizi kinyume cha mliyopokea (mapokeo). Waepukeni.Kwa maana watu kama hao wanatumikia tamaa zao kwa kutumia maneno matamu ya kudanganya kupotosha mioyo ya watu wanyofu" (Warumi 16:17-18). Sisi Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania,

1. Tunatambua kuwakwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo - (a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii; (b) lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi; (c) Serikali itawajibika kwa wananchi; (d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba" (Rejea Ibara 8, ibara ndogo 1); hivyo ni lazima Serikali iwasikilize wananchi.

2. Kwa kutambua kwamba mamlaka ya Serikali yanatoka kwa wananchi, sisi Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Tanzania, tumezisikiliza sauti zao, tumeisikiliza Serikali, na wadau wengine wa maendeleo,tukasali na kutafakari, na hivi tunatamka ifuatavyo:

2.1. Tukizingatia yaliyojiri na yanayoendelea katika jamii ya Tanzania tangu Mkataba huu uwekwe hadharani, taharuki kutokana na mijadala ya hadharani, mijadala ambayo imeligawa Taifa.

2.2. Na tukizingatia kuwa si mara yetu ya kwanza kutoa matamko kama hili kuhusu masuala yanayohusu jamii yetu;

2.3. Na kwa kurejea ibara za Mkataba tajwa hapo juu ambazo zina utata kwa uwekezaji wenye tija kwa Watanzania wa sasa na vizazi vijavyo;

2.4. Na tukiwa tunayashuhudia mashinikizo ya marekebisho ya sheria yanayokusudiwa kufanywa ili kuulinda Mkataba huu ambao Bunge la Tanzania limeuridhia hali tukiona ukiukwaji wa utawala wa sheria.

KWA HIYO:

3. Tukisukumwa na dhamiri iliyo na lengo la kulinda rasilimali, mshikamano, amani, uhuru, na umoja wa kitaifa; tunathubutu kusema kuwa baada ya miaka 63 ya uhuru wa nchi hii, wananchi hawajapenda kuiachia bandari ya Dar es Salaam apewe mwekezaji mmoja aiendeshe,kwa vile Watanzania wenyewe wana uzoefu wa kuiendesha.

4. Tunaona kuwa ni muhimu sasa kuendelea kujenga uwezo wa KITAIFA, kwa sekta zetu za umma na binafsi za Kitanzania tukiweka ubia na makampuni yenye ubobezi wa kiteknolojia kutoka sehemu mbalimbali duniani, na siyo ubia wa kutoka nchi moja, tukitumia mikataba yenye tija tuliyoandaa wenyewe juu ya mashirika yetu ya kibiashara.

5. Tunakiri kuwa utaratibu wa Serikali kuweka wawekezaji kutoka nje tu katika njia kuu za uchumi umetukosesha uendelevu wa vitega uchumi vyetu hasa pale wawekezaji wanapoondoka. Hivyo, bandari ikiwa ni moja ya njia kuu na ya asili ya uchumi inayotuwezesha kufanya biashara kubwa na mataifa mbalimbali, ni lazima iendelee kuwa biashara ya Watanzania wenyewe na ibaki mikononi mwetu hata kama tunaingia ubia wenye tija.

6. Kwa kurejea jitihada tulizofanya kuelewa Mkataba huu na kutoa ushauri wetu ambao haujazaa matunda mpaka sasa,na tukirejea mikutano yetu na Serikali katika ngazi za juu, ya tarehe 12 na 26 Juni mwaka huu 2023:

6.1. Tumefuatiliakwa umakini mijadala, maoni, mapendekezo na vilio vya wananchi walio wengi, ambao ni wamiliki wa bandari na rasilimali zote, na tumetambuakuwa wananchi walio wengi hawautaki Mkataba huu ambao unampa mwekezaji wa nje mamlaka na haki ya kumiliki njia kuu za uchumi kama zilivyobainishwa kwenye Mkataba huu.

6.2. Tumebaini kuwa kama nchitumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli, na bandari kavu huku tukiziendesha wenyewe.Hii ndiyo shauku ya wananchi, kusudi tuendelee kujenga uwezo wetu. Hali kadhalika, tumegundua mapungufuyetu ya uendeshaji wa bandari;vile vile tunao uwezo wa kuendelea kujizatiti kurekebisha mapungufu yanayojitokeza, wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu.

6.3. Kuna mifano tosha jinsi Watanzania tulivyoweza kujenga uwezo katika kuendesha mabenki kama vileNMB na CRDB, taasisi nyeti za umma na za binafsi na kadhalika.

7. Sasa kwa vile wananchi walio wengi hawataki uwekezaji wenye masharti mabovu kama haya katika bandari zetu zote; na kwa kuwa Serikali inawajibika kwa wananchi, lazima viongozi wasikilize sauti ya watu, kwani sauti yao ni sauti ya Mungu.

8. Historia imetufundisha kuwa kupuuza sauti ya wananchi kuhusu mikataba kwa siku za nyuma, kumeisababishia nchi hasara kubwa za kiuchumi, ukosefu wa ajira, na mapato ya kuendeshea huduma muhimu kama vile afya, maji na elimu. Tunashuhudia sasa Serikali kutokuwa na uwezo wa kuajiri na kulipa wafanyakazi wa kutosha katika sekta za elimu na afya ijapokuwa wahitimu wa fani hizo wako mitaani bila ajira. Hii ni kwa sababu vyanzo vikubwa vya mapato, mathalani migodi ya madini, vimemilikiwa na kuendeshwa na wawekezaji kutoka njekwa mikataba mibovu.

9. Kupuuza sauti ya wananchi juu ya uwekezaji usiosikia sauti yao. kumewaletea pia wananchi wa maeneo wanayoishi mateso, kama inavyoonekana kwa jamii za Wamasai wa Loliondo, ambao haki zao za kiutamaduni na kijamii zimekiukwa. Uwekezaji umepewa kipaumbele kisicho na tija na raia wa Kimasai wameachwa wakiteseka.

10. Tumeutafakari kwa makini Mkataba huu. Mkataba huu umechochea mgawanyiko wa wananchi katika kupambana na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa sheria, kutozingatiwa uhuru wa taasisi za kidemokrasia na mwingiliano wa mihimili yadola hasa Serikali na Bunge na sasa Mahakama inanyemelewa. KamaWatanzania tunapenda kusema kwamba bila uhuru wa taasisi hizi na utawala wa sheria tutaliangamiza Taifa.

11. Ikumbukwe kwamba, kutokana na mjadala mpana wa suala hili la mwekezaji mmoja kwenye bandari za Tanzania, wananchi wenye mawazo tofauti hawajui wamwendee nani ili misimamo yaoiweze kusikilizwa na kuzingatiwa; kwani Wabunge ambao ni wawakilishi wao wamewatelekeza kwa kufungamana na mwekezaji mmoja, kutokana na Bunge kuridhia Mkataba huu mnamo tarehe 10 mwezi Juni, 2023.

12. Hivyo, sisi Maaskofu Katoliki Tanzania wenye jukumu la kusimamia ustawi wa kila mwanadamu tunamwomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka aliyo nayo asitishe wasilisho la ridhio hili kwa upande wa pili,na vile vile Bunge nalo lifute ridhio la Mkataba huu unaolalamikiwa.

13. Makubaliano haya ya Kiserikali (Inter-Governmental Agreement IGA yana hatari zifuatazo kwa nchi yetu:

13.1. Kuharibu umoja na amani ya nchi yetu. Tukumbuke amani ikivunjika, yaweza kurudi tena baada ya jitihadi ya vizazi vingi. Nchi jirani kadhaa zimethibitisha hili.

13.2. Rasilimali za nchi zinazolindwa kwa pamoja kuwanufaisha baadhi ya raia na hivyo kuleta ubaguzi wa kiuchumi kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 27

Ibara ndogo ya 1, inayosema "Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya mamlaka ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi..."

14. Ibara zifuatazo za Mkataba huu zina matatizo yatakayosababisha nchi kutofikia uhuru wa kiuchumi (economic independence):

14.1. Ibara ya 2 (1): inayohusu lengo la Mkataba huu ambalo ni kuweka utaratibu unaoibana Tanzania kisheria katika kuendeleza, kuboresha na kuendesha bandari zote za bahari na maziwa, maeneo maalum ya uwekezaji, maeneo ya usafirishaji wa mizigo, na maeneo mengine ya kiuchumi.

14.2. Ibaraya 4: inayohusu wigo wa Mahusiano na Utekelezaji unaoitaka Serikali ya Tanzania kuwajibika kuijulisha Dubai kila fursa ya uwekezaji inapojitokeza.Hiiinakinzana na baadhi ya sheria za nchi yetu, kwa mfanosheria ya ushindani na ile ya manunuzi.

14.3. Ibaraya 5: ambapo DPWorldimepewa haki ya kuendeleza, kusimamia na kuendesha miradi pekee yake, wakati Tanzania inabaki na wajibu wa kumwezesha kufurahia haki hiyo.

14.4. Ibaraya 6:inayoitaka Tanzania kuwajibika kuipatia DP World vibali na vivutio vya kutekeleza miradi yake kama Serikali. Hii inapingana na baadhi ya sheria za kiutaratibu.

14.5. Ibaraya 7: inayoitaka Serikali kuwajibika kutoa mamlaka yanayotakiwa na mwekezaji bila ucheleweshaji.

14.6. Ibaraya 8: Haki ya kutumia ardhi ambapo Mkataba unasababisha uvunjifu wa sheria za ardhi na sheria zinazohusu masuala ya ardhi.

14.7. Ibaraya 10: Usiri wa Mkataba ambapo Mkataba unazuia mamlaka nyingine kama TAKUKURU /BUNGE kufuatilia mikataba.

14.8. Ibara za 23 na 24: zenye ugumu wa kujitoa kwenye Mkataba.


HITIMISHO:

15. Ni vyema, ni busara na ni hekima Serikali kuwasikiliza wananchi, maana kutowasikiliza ni kujiletea matatizo makubwa zaidi siku za usoni kwani wananchi hawahawa watavitaka vizazi vijavyo kuondokana na unyonywaji huu, kama tunavyoona kwenye kesi nyingi zinazoendelea sasa hivi katika mahakama za kibiashara za kimataifa dhidi ya mikataba iliyovunjwa na Serikali ya Tanzania. Tukumbuke mikatabaya madini miaka ya '90 viongozi wa dini na asasi za kiraia walipinga uwekezaji wa namna hii, na Serikali ikatumia mamlaka zake kuridhia mikataba hii na tunashuhudia ikivunjwa na nchi kulipa fidia kubwa. sasa hivi

16. Tunasisitiza kwamba SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU, hivyo basi kuwasikiliza wananchi na kufanya maamuzi kadiri wanavyotaka kutailetea serikali heshima kubwa ya kuwa sikivu kwa watu. Kinyume cha haya, Mwenyezi Mungu anatuonya kupitia Nabii Yeremia anaposema: "Kama kapu lililojaa ndege walionaswa, ndivyo nyumba zao zilivyojaa mali za udanganyifu. Ndiyo maana wamekuwa watu wakubwa na matajiri, wamenenepa na kunawiri. Katika kutenda maovu hawana kikomo hawahukumu yatima kwa haki, wapate kufanikiwa, wala hawatetei haki za maskini" (Yeremia 5:27-28).

17. Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.

Ni sisi Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania:

1. Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga - Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania, na Askofu Mkuu wa Mbeya
2. Askofu Flavian Kassala - Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania, na Askofu wa Geita
3. Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya OFMCap - Askofu Mkuu wa Dodoma
4. Askofu Mkuu Paul Ruzoka - Askofu Mkuu wa Tabora
5. Askofu Mkuu Yuda Thadei Ruwa'ichi OFMCap - Askofu Mkuu wa Dar es
Salaam
6. Askofu Mkuu Damian Dallu - Askofu Mkuu wa Songea
7. Askofu Mkuu Isaac Amani - Askofu Mkuu wa Arusha
8. Askofu Mkuu Renatus Nkwande - Askofu Mkuu wa Mwanza
9. Mwadhama Protase Kadinali Rugambwa - Askofu Mkuu Mwandamizi wa
Tabora
10. Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa - Askofu wa Iringa
11. Askofu Severine NiweMugizi - Askofu wa Rulenge-Ngara
12. Askofu Augustine Shao CSSp - Askofu wa Zanzibar
13. Askofu Michael Msonganzila - Askofu wa Musoma
14. Askofu Ludovick Minde ALCP/OSS - Askofu wa Moshi
15. Askofu Method Kilaini - Msimamizi wa Kitume wa Bukoba
16. Askofu Joseph Mlola ALCP/OSS - Askofu wa Kigoma
17. Askofu Agapitus Ndorobo - Askofu wa Mahenge
18. Askofu Rogath Kimaryo CSSp - Askofu wa Same
19. Askofu John Ndimbo - Askofu wa Mbinga na Msimamizi wa Kitume wa Njombe
20. Askofu Salutaris Libena - Askofu wa Ifakara
21. Askofu Almachius Rweyongeza - Askofu wa Kayanga
22. Askofu Liberatus Sangu - Askofu wa Shinyanga
23. Askofu Titus Mdoe - Askofu wa Mtwara
24. Askofu Eusebius Nzigilwa - Askofu wa Mpanda
25. Askofu Bernadin Mfumbusa - Askofu wa Kondoa
26. Askofu Prosper Lyimo - Askofu msaidizi wa Arusha
27. Askofu Edward Mapunda - Askofu wa Singida
28. Askofu Beatus Urassa ALCP/OSS - Askofu wa Sumbawanga
29. Askofu Anthony Lagwen - Askofu wa Mbulu
30. Askofu Filbert Mhasi - Askofu wa Tunduru Masasi
31. Askofu Lazarus Msimbe SDS - Askofu wa Morogoro
32. Askofu Simon Masondole - Askofu wa Bunda
33. Askofu Henry Mchamungu - Askofu msaidizi wa Dar es Salaam
34. Askofu Stefano Musomba OSA - Askofu msaidizi wa Dar es Salaam
35. Askofu Wolfgang Pisa OFMCap - Askofu wa Lindi
36. Askofu Christopher Ndizeye - Askofu wa Kahama
37. Askofu Mteule Thomas Kiangio - Askofu mteule wa Tanga

Imetolewa Dar es Salaam,
Tarehe 18 ya Mwezi Agosti Mwaka wa Bwana 2023.

Mhashamu Askofu Mkuu Gervas Pd. Charles Kitima
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Katibu Mkuu wa Baraza.
Nimekuja mbio nikishani ni wananchi, kumbe ni baraza la wanaowakilisha dini yao.
 
Back
Top Bottom