tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Mimi mkatoliki. Nakubaliana na Waraka.Mimi ni mkristo mkatoliki! Natoa maoni yangu kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya katiba ya Tanzania.
1.With due respect, sijaona wazo la maana la TEC. There is NO substance in it. Dunia ya leo inajengwa na uwekezaji wa kimataifa(international investments).
Hata China, Russia kuna uwekezaji mkubwa wa makampuni toka nje ya nchi. Tanzania siyo kisiwa. Lazima tuendane na sera za kiuchumi za dunia ya leo. Kuendesha mifumo ya uchumi mkubwa kama bandari, kijamaa tumeshindwa na tutaendelea kushindwa. Hata hii SGR tukisema iendeshwe kwa mifumo ya utumishi wa umma tutashindwa pia. Assets zenye sura ya kibiashara kama hii lazima ziendeshwe na private sector ili zilete faida na tija.
2. Findings za hao TEC ziko based on heresay. Wametumia axiom ya vox populi vox dei, Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.Je ni watanzania wangapi wanapinga uwekezaji huu wa DP World? Je kuna wakatoliki wangapi hapa nchini? Je wakatoliki wote wanaupinga mkataba huo? Je wakatoliki waliomo kwenye orodha za wakatoliki bado ni wakatoliki mpaka sasa?(Wengi wameshahamia kwenye ulokole).
Ukijibu maswahi hayo utaona maaskofu wa TEC hawana uhalisia kwenye waraka wao.Ni blah blah tu. No driving facts. It is just FALLACY OF GENERALIZATION. Findings zao hazina supporting data. Wamekurupuka!
3. DINI: Naona ni hofu za masilahi yao ya kidini, wala siyo tatizo la mkataba. Wazungu toka nchi za magharibi walipoingia mikataba ya kuiba madini ya watanzania, maaskofu wa TEC walikaa kimya!!! Leo wakati wa mkataba na waarabu ETI wanajitia kuandika waraka wakijipambanua ETI wazalendo,watetezi wa rasilimali za nchi. UWONGO mtupu!
4. Serikali haina dini na mambo yote ya dini yapo nje ya mifumo ya serikali(Ibara ya 19 ya katiba ya TZ,1977). Huo waraka wao hauna mashiko wala nguvu yoyote mbele ya Jamuhuri. Ni kama makaratasi ya kufungia maandazi tu! Hayo ni maoni yao kama maoni ya mtu yoyote yule.
CONCLUSION: Serikali iendelee na mchakato wa utekelezaji wa mkataba na DP World HARAKA SANA, ili kama taifa tuanze kunufaika na uwekezaji huo HARAKA. Serikali kikatiba ina mizizi mirefu sana na mikubwa sana, isiyumbishwe na kelele za chura ambazo ni nyepesi sana.
Wananchi tuna hitaji pesa ipatikane ili tupate huduma bora za kijamii. Uwekezaji DP world ni LAZIMA ufanyike. Na ufanyike HARAKA iwezekanavyo. Serikali ina legitimacy ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wananchi kwa sababu iliingia SOCIAL CONTRACT na wananchi kwa kushinda uchaguzi,2020.