Ni kweli kuna wanaume wenzetu wana vichwa vigumu aisee usiombe.
Mimi nina shemeji zangu wawili naona mifano dada zangu wanavyoteseka kuibeba familia.
1.Kuna mmoja yeye alimuoa dada yangu ni mtu anaongea sana,maneno mengi,mipango mingi yaani ukikaa naye kwa mara ya kwanza unaweza kusema baada ya mwaka tu huyu jamaa anakuwa kama Mo Dewji lakini matekelezo ni zero.
Yeye alikuwa ni mtu wa kulelewa tu na mwanamke yaani inapita wiki nzima hajaacha hata buku 5 na anategemea akirudi jioni akute chakula ale.
Mke kila akimfundisha jamaa haelewi kesi ikafika kwa familia tukafundisha wee lkn wapi jamaa haelewi anachoongea hata hakieleweki yaani mbele nyuma,nyuma mbele basi mwisho wa siku wakashindwana.