Watoto wa single parent sio mme au mke bora wanakuwa wamekosa balance ya malezi pili hawana Upendo, tatu hawawezi jua maana ya ndoa sababu hawajaishi kwenye misingi ya ndoa. Hata wakiolewa ni lazima wataishia kama wazazi wao
Maana yake tuendelee wazalisha tu
 
Kwa ujumla wanawake ni wakatili sana.
 
wanaume tuko na busara katika kuyatreat mambo, mwanamke akili yao inategemeana na moment alizospend na mtu husika kipindi cha mahusiano yao, wanaume tukishafanya maamuzi kutoka hatua moja kwenda nyingine tunaweza simamia bila kujali changamoto, mwanamke hata aki move on but ikitokea changamoto ni rahisi kukumbuka mahusiano ya nyuma na kuyaona yanathamani zaidi kuliko aliyonayo, mwanamke anaongozwa na mapenzi zaidi na ci mwepesi wa kuunda logics zitakazo msaidia kuto kufanya maamuzi mabaya yakaaribu future yake, mwanamke mwenye mtoto kama mzazi mwenza yuko karibu kwa tricks zilezile alizotumia kumjaza mpaka mimba endapo akizitumia tena hata kipindi yuko nawe ni rahisi sana kukucheat wakakumbukiza ya nyuma yao.
 
Habari za Asubuhi wanajamvi na wapenzi wa habari moto moto za Mahusiano na Mapenzi. Niende kwenye maada. Kuna haka kakasumba au kamtego wanakatumia sana dadaz hasa single mothers au wale mile zimesogea.

Mtego huu watoto wa kiume wengi wamenasa na wengine wanajuta kwanini hawakushituka mapema. Ninao washikaji kama wanne hivi wamekamatika na leo wanahangaika na kusumbuliwa na kesi kwenye madawati kijinsia. Kwa wale ambao mtego hu mliwahi ushitukia na kuuruka hongereni sana wakuu.

Mtego huu wadada wanautumia sana kujinufaisha na hata pia inapelekea wengine kuvurugiwa malengo yao. Ni ukweli usiopingika kuwa huu mchezo sio mzuri na inabidi vijana wa kiume wote tuufahamu na mwisho tuukatae kwa kufanya maamuzi sahihi.

Hawa wadada wamekuwa na gear ya pekee sana katika kuuweka huu mtego na hasa hasa akiona mkaka una maisha yako, kula na kulala hakukusumbui na ukute una ajira rasmi au Biashara yako ya kueleweka.

Natambua wote mmeshaijua hata kabla sijaitaja. Najua unatamani kujua ni mbinu ipi hiyo, basi tulia nikujuze. Single mazaz au wale Number A au B, wamekuwa wajanja sana. Ukianzisha nao mahusiano wanakuweka karibu sana halafu ikifika muda atakuambia mie ninataka mtoto, na ukimwambia kuwa mie sijajipanga atakuambia huyo mtoto nitalea mwenyewe kwanza nina kazi au biashara zangu hivyo sitakusmbua chochote.

Wengi wetu tumekamatika sana. Ukishampa mimba au ujauzito atakuacha mwezi wa kwanza then baadae sarakasi huja na unajikuta unashangaa imekuaje wakati tulikubaliana kabisa. Utafikishwa kwenye madawati kijinsia na kuwekewa masharti na utaratibu wa kutoa pesa ya matumizi ili hali hata hukuwa umejiandaa.

Kuna jamaa yangu anahangaika na huyo dada daah. Kwahiyo tuweni makini, mimi kuna huyo mdada game moja tu anataka mtoto, nimekataa wazi wazi naona kishaanza kupunguza ukaribu na mimi na hata akija nimle natumia mpira. Shituka kaka, shituka mjomba amka usingizini.

Nawasilisha🙂
 
Mkuu umeandika maneno mazuri, tatizo umesahau kweka japo ' aya ' ili ivutie kwa msomaji
 
Kwa uandishi huu nakuombea hata wewe ukamatike tu na hao masingo maza maana hakuna namna [emoji16]

On a serious note, wewe mwanaume mzima na akili zako unakubalije kuleta kiumbe hapa duniani wakati unajua kabisa kuwa hutashiriki kwa namna yo yote ile katika malezi na makuzi ya kiumbe hicho?

Hata huyo singo maza asingekuwa mtata na akatimiza ahadi yake asikusumbue kamwe kuhusu malezi ya mtoto, kama mwanaume uliyekamilika, hicho kweli ndicho unachokitaka? Mtoto wako mwenyewe akue bila malezi ya baba yake? Bila father figure katika maisha yake na dunia hii iliyoharibika hii? Na wewe upo mzima wa afya na una uchumi mzuri kama unavyosema? Mawazo gani haya nyinyi vijana wa siku hizi?

Be responsible. Kama huwezi kutunza mtoto atakayezaliwa basi acha kupelekea moto watoto wa watu (haijalishi kama ni singo maza ama la!) au tumia kinga. Janaume zima eti umerubuniwa na singo maza kwa ahadi kuwa atalea mwenyewe wakati na wewe upo mzima huna tatizo lo lote na wewe ukakubali. Ni Umario na ukwepaji wa majukumu wa kinyama!

Hopulesi kabisa yaani! [emoji2211][emoji2211][emoji2211][emoji2211]

 
Vijana wamekuwa mlenda mlenda sana. Wanateleza tu. Jinga jinga.
 
sasa mwanaume unakubalije ujinga wa kuzaa na mtu usie na malengo nae kwa kigezo kuwa hautailea damu yako? mi damu yangu siwezi kuiacha hivyo hivyo siwezi kumbebesha mimba mwanamke nisie muhitaji awe karibu na maisha yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…