KWA NINI SINGLE MOTHER WANAOGOPWA KULIKO SINGLE FATHER?
Anaandika, Robert Heriel
Baadhi ya Wadada wamekuwa wakiniuliza iweje Single mother pekee Yao wanaogopwa na Vijana wakiume lakini Single father hawaogopwi na Vijana wakike? Aidha ni Kwa nini Mwanamke mwenye mtoto anapata changamoto kubwa Kupata Mwenza wa kumuoa ukilinganisha na Single father?
Kwa kuongezea, ni kwanini kijana akitaka kuoa single mother atapata upinzani mkubwa kutoka Kwa Wazazi na Ndugu zake na jamii Kwa ujumla? Maswali hayo leo tutaenda kuyajibu Kwa kifupi.
Single mother ni mwanamke mwenye mtoto au Watoto ambaye hajaolewa au aliyepewa Talaka. Huyo ndio single mother. Wakati Single Father ni Mwanaume mwenye mtoto au Watoto ambaye hajaoa au aliyekwisha kupeana Talaka.
Zifuatazo ni sababu za Kwa nini single mothers wanaogopwa zaidi kuliko Single Father;
1. Upendo
Wanawake asilimia 90 wanabeba mimba Kwa wanaume wanaowapenda iwe kwa upendo halisi au upendo wa Mali,
Mwanamke hawezi kuzaa na Mwanaume asiyempenda, Wakati Sisi wanaume suala la kuzaa halipo Chini ya maamuzi yetu.
Sisi wanaume tunaweza bebewa mimba na Mwanamke yeyote hata tusiyempenda, na bahati nzuri au Mbaya wale Wanawake tusiowapenda ndio wepesi kushika MIMBA.
Mwanaume anaweza kutelekeza Mama na mtoto Kwa sababu Hakumpenda Mama na bila Shaka mtoto hakuwa kipaombele chake. Mtoto hawezi kumfanya mwanaume ampende Mwanamke, Ila Kwa upande wa mwanamke mtoto anaweza kumfanya Mwanamke ampende Mwanaume.
Mwanamke analazimika kumpenda mzazi mwenza Kwa MASLAHI ya mtoto, Wakati Sisi wanaume hatunaga kitu kama hicho. Hatulazimiki kumpenda Mwanamke Kwa sababu ya Watoto.
Hii inafanya Single mother kuogopwa Kwa sababu bado wengi wao huwa na bond na Wanaume waliozaa nao Kwa MASLAHI ya mtoto.
Ni nadra Kwa mwanaume kumtafuta Mwanamke aliyezaa naye lakini ni Jambo la kawaida Kwa Wanawake single mother kutafuta Mababa wa watoto Kwa sababu nyingi tuu.
2. HUDUMA KWA MTOTO/WATOTO
SIngle mother wanaogopwa zaidi Kwa sababu wanakuwa wasumbufu kupiga piga simu Kwa wanaume waluowazalisha Kudai Huduma za Watoto. Lakini Hii ni tofauti na single father, mtoto akikaa na Baba yake atahudumiwa na Baba pasipo Mama yake kusumbuliwa.
Yaani haiwezekani single father adai Huduma ya mtoto Kwa mzazi mwenza.
Single mother wengi wanajua ni hasara kubwa kwao kumpa Mwanaume mtoto kwani watakosa mawasiliano na pili wapo wanaopatiemo huduma kupitia Watoto.
Wanawake wengi wanaoolewa na Single father hupendelea huwashauri Waume zao kuwachukua Watoto waishi NAO palepale nyumbani ili kukata mawasiliano baina ya mumewe na Mzazi mwenza, na kama atataka kuwasiliana na mwanae basi simu itapokelewa na atapewa simu mtoto aongee na mama yake.
3. SINGLE MOTHER WENGI KIPAOMBELE CHAO NI WATOTO.
Hii ni tofauti na Single father, wanaume wengi Watoto sio kipaombele Sana ikiwa tuu ataona Mkewe anamheshimu na kumtii. Ndio maana ni kawaida Kwa wanaume kutelekeza watoto. Hilo wala halina mjadala.
Mwanamke yupo connected na watoto wake automatically tofauti na Sisi wanaume.
Single mother wengi kipaombele Chao ni Watoto wao, kila kitu atakiangalia katika jicho la kumlinda mtoto wake, na yupo tayari kufanya lolote kwaajili ya mtoto wake. Hii ni tofauti na Single father, yeye atadili na Familia Kwa ujumla Kwa kumpenda Mkewe na kumpa kipaombele Mkewe kwani yeye ndiye mlezi wa watoto na familia Kwa ujumla.
Single mother hawezi kukupenda kama anavyompenda mtoto au Watoto wake Ila SIngle father anaweza akampenda Mwanamke/Mkewe Mpya kuliko anavyowapenda Watoto wake.
4. DRAMA
Single mother wanadrama nyingi mno ukilinganisha na Single father. Waliooa single mother wamekuwa Watu wanaoripoti visa na mikasa ya kusisimua na kushangaza, tofauti na wanawake walioolewa na single father.
Tabia ya mwanaume ni ileile haijalishi ni single father au sio single father. Haijalishi ni kijana au Mzee. Wanaume Tabia zetu ni zilezile.
Hii ni tofauti na wanawake, Wanawake wapo tofauti tofauti kulingana na umri, maumbile, Elimu, hadhi, mwenye Watoto n.k
I) Mwanamke Bikra hafanan na Mwanamke asiyebikra,
ii) Mwanamke single mother hafanani kabisa na Mwanamke asiyesingle mother, yaani ni jinsia moja lakini wapo tofauti kihisia, Kiakili, kimtizamo na kimaamuzi.
iii) Mwanamke mwenye umri wa miaka 15-25 hafanani na Mwanamke mwenye umri miaka 25-40 na pia hawafanani na Wanawake wenye miaka 41-60 linapokuja suala la mahusiano.
Lakini kijana wa miaka 15-25, 25-40, MTU mzima wa miaka 41-60 wanafanana linapokuja suala la mahusiano.
5. SINGLE MOTHER HUPENDA KUPEWA HESHIMA ILEILE UNAYOMPA MKEO HATA KAMA MMEACHANA. WAKATI SINGLE FATHER HUO MUDA HANA NA SIO AJABU AKAWATELEKEZA HATA NA WATOTO.
Ukioa single mother elewa kuwa kama aliyemzalisha anampa heshima yote kama Mkewe(Kwa jina la Mzazi mwenza) na akawa anawahudumia Watoto wake basi kazi yako kama mume Kwa huyo Mwanamke ni kubwa Sana. Utapata tabu Mno.
Elewa kuwa Mwanamke single mother ndio hulazimisha ukaribu wa mzazi mwenza naye Kwa mgongo WA mtoto. Ila ni ngumu mwanaume single father kutafuta ukaribu na Mwanamke aliyemzalisha. Hakunaga kitu kama hicho.
Ingawaje single mother wanaweza kukuambia kuwa hawasiliani na Mzazi mwenza lakini Kwa Sisi wakulungwa tunasema huo ni Uongo.
Lakini single father akikuambia hajawasiliana na Mzazi mwenza muamini kabisa Kwa sababu Sisi wanaume tunaathiriwa zaidi na MTU aliyekaribu kuliko aliyembali, sio ajabu Mwanaume anauwezo wa kukaa hata mwezi au miezi sita bila kuwasiliana na Wazazi wake lakini Kwa Mwanamke ni tofauti.
Sasa ikiwa mwanaume anauwezo wa kukaa muda mrefu bila kuwasiliana na Mzazi aliyemzaa sembuse Mwanamke aliyemzalisha au sembuse Mtoto?
Lakini Kwa Mwanamke hilo hataweza tena akijua Mwanaume aliyemzalisha anauwezo wa kiuchumi.
Eid Mubarak
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam