We umeona wapi mechii bado haijaanza tayari ushafungwa 1-0??

"[ᴬ ᵍᵒᵒᵈ ᵖˡᵃⁿ ᵛⁱᵒˡᵉⁿᵗˡʸ ᵉˣᵉᶜᵘᵗᵉᵈ ⁿᵒʷ ⁱˢ ᵇᵉᵗᵗᵉʳ ᵗʰᵃⁿ ᵃ ᵖᵉʳᶠᵉᶜᵗ ᵖˡᵃⁿ ᵉˣᵉᶜᵘᵗᵉᵈ ⁿᵉˣᵗ ʷᵉᵉᵏ"
 
Ndugu nikusisitize jambo, katika kuoa msikilize sana Mama. Nikukumbushe tu, mama ndiye mjenzi wa Familia, changa karata zako vyema.
Nami nakusisitiza jambo katika kuoa tumia sana akili wazazi ni watu wa nyongeza katika kuijenga familia yako.

:Utamuacha mama yako pamoja na baba yako utaambatana naye kama mke nanyi mtakuwa mwili mmoja"

Sasa ww kila unachotaka kufanya mshirikishe mama yako tuone uko mbeleni kama hutapangiwa kila kitu cha kufanya kwenye familia yako. Kuwa mwanaume na simama kama mwanaume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi ni mtoto wa mchungaji na nimekulia dini kwa hiyo ni dhambi kwa mwanamke kuvaa suruali

Sent using Jamii Forums mobile app
Zipo dhambi mnafanya kwakuwa azionekani hamzihesabu, mnaanza kuzini toka primary na videm mmevipanga huwa hamuhesabu kuwa mnafanya uasherati, eti mtu akivaa suruali ndo mnaiona dhambi
 
Labda nikushauri kitu embu kuwa naye kwanza usikimbilie kuoana naye kama kwenye mapenzi yenu hamjafikisha miaka mi2 jaribu kukaa mapenzi naye ata miaka4 umsome zaidi usije ingia chakike mda uwo naisi utakuwa umejua yuko vp na mahusiano na mzazi mwezie yakoje na wanawasiliana vp na kipi kilifanya watengane na familia yake ni ya watu gani maana kuna vitu ni vyakijinga sana kufatilia ila vinaumuimu sana kama mama yake kaolewa yani anaishi na baba yake kama haishi naye na hajafariki weka kiulizo? Kingine mtindo wa maisha yake akikasirika anakuaje.

Kumbuka kakupita umri usiangalie pesa na Mali alizonazo kama anazo ila upendo heshima aliyonayo kwako ila kumbuka pia wanawake ni mabingwa wa kuigiza wakiwa wanakitaka kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana anapoint mama yako na anaona mbali, mke mwenye mtoto unaweza kuoa na kama anajitambua mkaishi kwa uaminifu,ila kama Baba mtoto anaweza kuwa anakumbushia cos mtu aliyefikia hatua ya kuzaa na mtu mwingine wanavitu watamisiana tu.

Japo si wote,mkuu changanya na zako
 
Wazazi wako Wana akili Sana. Wapo sahihi kabisa pamoja na ndugu zako. Wote hao wamakutakie mema . Ingekuwa mmoja tungeqestion . Ndugu wote wasikilize. Single mother ni wasumbufu Sana. Huyo ni mke wa mtu yaani mwenye huyo mtoto bado ana access kubwa ya kuwasiliana na single mother. Ni rahisi kupewa mzigo akihitaji . Mtoto ni connection kubwa kati ya mama na Baba. Kwani unapenda kuitwa Baba wa kambo . Mtoto hawezi kukupa full respect kwasababu anajua wewe sio Baba yake. Jinsi ya kumlea ni ngumu mno. Inajibidi kujifunga mkanda unapojitolea kumlea mtoto huyo. Mtoto akililia wembe mpe akijikata ni shauri yake
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utafiti binafsi niliofanya unaonyesha Watoto wakali wengi walio kwenye umri wa kuolewa wana Watoto, au la basi wameshazichomoa.

Kwa Wazazi wako kukushauri usioe Mwenye Mtoto hakika wanakupunguzia pakubwa wigo wa kuchagua maana kwenye kila kumi sita tayari utakuta wana Mtoto/Watoto.

Tofauti na hapo uvizie vile vinavyomaliza darasa la saba, maana vingi vyao ndio vipo fresh...ila ujiandae kusumbuana na dola.
 
Vitu kama kuoa ni lazima wazazi uwashirikishe . Kuna vitu wazazi Wana nafasi ya maamuzi Yao . Biblia inasema mheshimu Baba na mama yako ili siku za kuishi kuongezeka. Wazazi ni Mungu wa pili wamehusika kwenye uumbaji wako. Ndio maana wazazi wanauwezo wa kutoa laana kama Una makosa itakuopa kwelikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hao wazazi wako wanamkataa huyo mwanamke kwa sababu ana mtoto na amekuzidi umri au wanamkataa kwa sababu ya tabia zake mbaya na utaratibu wake mbaya wa maisha yake.
 
Ngoja nifatilie single Mother wanavyowatetea Single Mother mwenzao!

Mtoa Mada kuna Mada nzuri hapa zilishajadiliwa sana hapa kuhusu Single Mothers na Matatizo yao, tafuta hizo Mada utajifunza vingi sana.
 
wazaz n muhimu sana ktk maisha yetu hususan ya ndoa ila hawana uwezo wa kukuchagulia moyo wako wa kumpenda ila wanaweza kuuchagulia mwili wako wa kulala(lugha ya kiutuzima kidogo) nae,kama ni single mother ujue kuna mtu aliezaa nae maana watoto hawapatikan kwa kupiga chafya au kuangaliana,ujue why kaachika ingawaje kuangalia yaliyopita kwa mwenzi wako kuna negative impacts zake ila ujue lengo lako n kutaka kujua nn,yawezekan mwanamme ndo chanzo au mwanamke ndo kunguru,ingawaje single mother weng wanatulia ktk mahusiano mapya maana wanajua past zao walipoharibu au kutomchanganya mtoto kisaikolojia kwa kuwa na mababa weng ktk ukuaji wao,usikulupuke kwanza,tulia,kama vp ishi nae bila ndoa maana najua kama kunanihii nae tayar,vjana wa siku hz hampend kuuziwa mbuz katika kiroba mpaka mumuone,ukikaa nae utamuelewa,waweke wazaz chini nao uwaeleze nia yako ni nin maana hapo wew unatetea moyo wako na wazaz wanamtetea mtoto wao,pima mambo bila kulaumu upande wowote
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie, huyo mama pengine ana binti ambaye anaweza akawa single mother mtarajiwa na hajui hatma yake.

Kubaliana na mwenza wako abebe mimba, Mimba ikiwa changa pitisha ndoa hata km ya mkeka.
Hakuna mwanamke atapenda mwanae aanze na single maza hata Kama yeye Ni single maza.
Wanawake ndio wanajua changamoto zote wanazopitia katika Kila hali.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachosema ni kweli .yani mabinti wote wanaovutia walisha zalishwa na kuachwa sasa ukijichanganya uoe unaoa mke wa mtu
 
Kuvaa suruali na enyewe ni kigezo eti cha kutokumuoa mtu? Labda ungesemea mengine hayo mkuu watu tumevaa suruali toka utotoni mpaka tunaolewa tuna watoto suruali tunavaa haijawai husiana na tabia ya mtu iyo
Kumbukumbu la torati 22:5 Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.
 
Kumbukumbu la torati 22:5 Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.
Lakini suruali huwa ni za kike mkuu sjasema km tunavaa za kiume😛😛😛😛
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…