Kunawatu Ni ma Idd Amin dada sema tuu hawajapata nafasi!! Roho nyeusiiiiiii....
 
Ametawaliwa na jazba hafai kuongoza muhimli kubwa kama bunge na alipoteza sifa zaidi alipo mpiga mgombea mwenzake fimbo ya kichwani hadi akazimia.
 
Mlimshangilia sana kawageuka mmeanza kumtukana mtamsifia tena Tulia. Wabunge wakijiheshimu hayawezi kutokea haya
 

Ndio hata mwislamu safi atakuambia bora mbuzi kuliko nguruwe.

well said bro! Mwita
Yaani ni ngumu sana kwa wananchi kuwaelewa na kuwaamini hawa jamaa. Ni vigeugeu wa hatari..
Hata katika kesi, washinde wao tu utasikia mahakama imetenda haki, tunaimani na mahakama.
Ila wakishindwa kesi...matusi yake kwa mahakama hayasemeki.
 
Nyie jamaa huwa hamna akili!! Au kama mnazo basi mnawendawazimu... Kila siku mlikuwa mnamsifia hapa Na kumtukana hadi matusi ya nguoni naibu spika Tulia. Leo mnamgeuka Ndugai wakati mlimchagua kwa wingi wa Kura! Mkapimwe akili
 
SPIKA WA BUNGE HATOSHI; ANAWASALITI WANANCHI. HADHI NA UKUBWA WA BUNGE KUDHOOFIKA.

Kwa mujibu wa Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, askari hawa kama waonekanavyo katika picha, walikuwa wanambembeleza MHE John Mnyika (Mb) aende nje ya ukumbi wa Bunge.

Kwa utashi wa kawaida (common sense), yawezekana askari hawa walitakiwa kutoa bastola kumnyooshea mhe. Mnyika, au kupiga risasi juu, ndiyo wangemridhisha Spika Ndugai kuwa wametekeleza amri aliyowapa, na kwa kosa la kutokufanya hivyo ameamua kuwahamisha kabisa na kuleta askari wengine.

Bunge ni chombo pekee cha kuwatetea wananchi dhidi ya serikali, lakini hivi sasa Bunge limekuwa kama wizara ya serikali au idara mojawapo ya serikali, uongozi wa Bunge hauna tofauti na uongozi wa serikali, ukubwa wa Bunge (supremacy of the parliament) haupo tena, na badala yake Kuna umoja wa Bunge na serikali, hii ni hatari kubwa kwa nchi na wananchi.

Tanzania hi inaelekea wapi? Utumwani tena?

Sasa watanzania mtakubaliana nami kwamba, tunahitaji uongozi wa Bunge usitokane na chama Cha siasa, kuanzia Spika, Naibu Spika na wenyeviti wa Bunge. Pia, tunahitaji mawaziri wasitokane na wabunge, na Mwanasheria Mkuu wa serikali asiwe sehemu ya wabunge. Bunge lifanye majukumu yake ya kibunge, na serikali iwajibike kwa upande wake. Ndipo tutakapoweza kuuondosha Ubatili huu.

 
Nyie jamaa huwa hamna akili!! Au kama mnazo basi mnawendawazimu... Kila siku mlikuwa mnamsifia hapa Na kumtukana hadi matusi ya nguoni naibu spika Tulia. Leo mnamgeuka Ndugai wakati mlimchagua kwa wingi wa Kura! Mkapimwe akili
Mnachoshangaa ni nini, hata kama walimkubali mwanzo ni wao na leo wamegundua wamebugi master ni wao pia and they are right, acheni kukariri majibu.
 
Keshasahau alimtandika mwenzake bakora na akasamehewa!
 
Nyie mna matatizo kweli si mlisema bora ndugai kuliko huyo tulia ackson
Kuwa bora sio bora zaidi kuliko bora.....hata bora huweza kupoteza ubora.....co kuwa bora ukipoteza ubora ubaki kuwa bora.

Tulisema bora kulko yule mama ....lkn hatuulnganisha ubora huo ns vchwa bora vya upinzani.

Hv umeewahi kujiuliza bila upinzani maisha yako yangekuaje mtaaani!!?
 
Mfyuuuh yaani kuna comments mbili humu nimeziona zahovyo haijawahi kutokea. Sjui walikula nini Jana hao.
 
Huyu jamaa hana spear kibogo ya Machadema ... wewe mtumwa wa wazungu utaendelea hivyo hivyo kuosha vitaulo mambo ya bongo tuachie wabongo. Ukoloni mambo leo peleka kwa wakimbizi wenzako.
 
Nikweli kabisa hauwezi kuongoza bunge kishabiki naupendeleo wabunge wa upinzani wanapotoa hoja za msingi wanapingwa sijapenda hakuna usawa
 
Bunge hili la sasa limejaa vituko, chuki na kufitiniana kwa kiwango ambacho hakijapata kutokea huko nyuma. Sasa imefikia wabunge wanaombeana mabaya na kufikia kutaka kuzichapa kavukavu.

Hii ni dalili mbaya kuwa uongozi umeshindwa kuliweka pamoja Bunge kwa manufaa ya wananchi. Na kitendo cha wabunge kumsusia futari spika ni salamu kuwa amekuwa adui yao.
Ndugai, toka urudi kwenye matibabu umekuwa na mambo ya ajabu ajabu jee kuna shida?

Kama hali sio nzuri sii ujipumzishe ili kulinda heshima maana haya ufanyayo hayajawahi kutokea kwa watangulizi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…