Ndugai ni Spika asiye na sifa za kuwa spika
anataka aogopwe na wabunge kama mawaziri wanavyoogopa kwa mwenye nchi
 
Kutokana na Mgogoro ambao umemhusu Mbunge wa kibamba Mhe John Mnyika nimebaini Pasipo na shaka kuwa Job Ndugai ambae ni Spika, hana uwezo kabisa wa kuongoza chambo kikuu cha maamuzi kama Bunge,

Japo kuwa ni Spika Tayari lakini tunatakiwa kujua kuna watu ni Marais lakini hawana sifa za kuvaa uhusika hivyo hivyo Ndugai hafai kuwa Spika na Wala tusitegemee jipya lolote kutoka kwenye Bunge analoliongoza yeye na msaidizi wake Tulia Ackison.

Nimesema hivyo hana sifa yoyote ambayo imetokana na Nadhalia za uongozi ususani skill model of Leadership.

Na hizi ndio sifa za Job Ndugai ambazo zinamfanya kukosa sifa za kuwa Spika japo ni Spika na kwa maana hiyo Bunge la sasa ni Dhaifu sana.

1)-Anajaziba, kutokana na hii sifa siku zote hawezi kutoka maamuzi sahihi sifa hii inaonekana pale alipompiga Mgombea mwezake wa ndani ya chama chake.

2)-Ni Mtu wa kujipendeza, na hii inafanyika ili atete kiti chake cha uspika ndio maana anatumia nguvu nyingi kuwaonea wapinzani ili amfurahishe Rais ambae ndio Mwenyekiti wa chama.

3)-Nimkurupukaji, kutokana na sifa hii inamfanya afanye maamuzi na atoe kauli za kitoto ambazo zinalifanya Bunge kuwa dhaifu sababu linaogozwa na watu dhaifu.

Mfano aliposema Lusinde wewe ni kiboko yao mpaka wote wameondoka hii nikauli ya kitoto haikupaswa kusemwa na mtu kama Spika.

4)- ni kigeu geu, sio mtu wa kuamini au kupanga nae mambo makubwa na hii inasababishwa na yeye kuwa mtu wa kujipendekeza.

5)-Anaongozwa na Mhemko, Hana Busara wala Hekima kwa Suala la Mnyika hajatumia Busara wala Hekima Mropokaji.

Kutokana na madhaifu yake yote hayo mzee Chenge ameonyesha uwezo mkubwa kuliko yeye pamoja na msaidizi wake Tulia Ackison.

Kutokana na wabunge kuonewa katika kipindi chake na Serikali au na yeye Mwenyewe pamoja na Msaidizi wake wamefanya ubunge kutokueshimaka kabisa na watu.

Nilikuwa sijawahi kusikia Kwamba Mbunge anaweza kuwekwa ndani mwezi 4 na hajaua ni kipindi cha Ndugai kwa maana hiyo pale amekaa kuziba nafasi isiwe wazi na sio kuliongoza Bunge kupitisha maamuzi sahihi kwa maslahi ya nchi yetu kama lilivyokuwa Bunge la 2005- 2010 kila mtu alitamani kuwa Mbunge.

Ni Mhere Mwita.
Pamoja na mapungufu yake hayo yoote lakini nimeambiwa pia kuwa effect ya ule ugonjwa wetu huwa unawasumbua saana waathirika katika stage ya mwisho...ahaaa...nywele zoote kushenei...India kila siku...
 
umejua lini?
 
hamjui mnataka nini
mlimtukana Tulia kuwa anabebwa,Ndugai ndio spika anajielewa
Leo Ndugai amekuwa hafai?
 
Mbaya zaidi yale mafiga matatu yasipokuwapo nchini yeye ndiye kingozi mkuu wa nchi.

Yaani, Tanzania huwa hatukosi kuwa na kiongozi hasara.

Tukiwa na rais mzuri lazima kilaza atakuwa mahala fulani atakaye haribu tu mfumo.

Ni kama sasa hivi, nchi iko vizuri kwenye mafiga matatu ila tatizo ni huyo mpiga wagombea wenzake Kwa rungu .

Sasa tabia yake ya kupiga watu marungu , anataka kutufundishia askari wetu wenye weredi kufanya huo upuuzi na unyama.

Kweli, Mungu kama wanaomwamini yupo, Basi amrudishe tu mahala pema peponi huyo jamaa maana hana faida tena.
 
Anafanyakazi kishabiki mno kuliko weledi ndiyo tatizo lake kubwa....muangaline Chenge akiongoza bunge na yeye utaona tofauti kubwa mno,mbali na madhahifu mengine Chenge aliyonayo ila kwa kuliongoza bunge anafaa mno kuliko Job na msaidizi wake....Na ungiangalia matatizo makubwa sana ya nchi hii yanatojana na kutokuwa na bunge imara lenye uongozi imara
 
Nimejaribu kutafakari kwa kina sifa za wanasiasa wetu wa tanzania nabaki sielewi kabisa maana wanachoongea na wanachokitenda ni vitu viwili tofauti.

Spika wa bunge la Jamhuri ya Tanzania Mheshimiwa ndugai ameamua kuwaondoa askari waliochelewa kumchukulia hatua mheshimiwa mnyika. Akiongelea swala hilo kasema mbunge ni mheshimiwa akishindwa kuonesha uheshimiwa wake lazima adhalilishwe. Amesahau yeye kwenye harakati za uchaguzi aliwahi mpiga mgombea mwenzake lakini hakufanywa kitu chechote.

Najiuliza uheshimiwa wa Ndugai uko wapi mpk awaone wenzake hawafai, mpk atake askari wambebe mwenzake kama kaua mtu. Wanasiasa wa Tanzania wanakera sana, hawajisahihishi, wanaona sana kibanzi kwenye macho ya wenzao na si kwenye macho yao.
 
Huu ni wakati wa ngumi kupigwa bungeni, jinsi Ndugai anavyotumia mabavu, kwenye mambo ya hekima, ndio jins ambavyo atasababisha vurugu bungeni, anachokifanya Mh Ndugai ni sawa na kumtishia mtu mzima nyau, mabunge mengine ngumi zinapigwa kama kawa, bunge sio kikao cha mapadri na maskofu.

Natamani ningekuwa bungeni nionyeshe mfano, udikteta wa Ndugai ni mbaya zaidi kuliko ule ukoloni mjerumani
 
Siyo hivyo, neno kudharirisha siyo neno zuri, heri angesema aadhibuwe siyo adharirishwe
 
Kumlaumu Mh.Ndugai ni makosa makubwa katika kipindi hiki..Nani angeweza kusimamia haki ktk nafasi alionayo Mh.J.Ndugai?
Tujifunze kupitia makosa...
 
Back
Top Bottom