Sababu za kutengana hazijulikani lakini kuna mtu tayari umeshamtwisha lawama
Ndoa zina Siri nyingi wanaojua ukweli ni wao waliooana ila wa nje hawajui ko wanapendelea kutoa lawama bila kujua undani wake.
 
Kuachana ni jambo la kawaida siyo jambo jipya wala siyo kwa mjomba wako tu.
 
Mada za kuponda single mothers humu JF hugeauka vita.

Mtoa mada omba samahani maana umechokoza watu.

Hata Mimi ninawaunga mkono single mothers kwa kweli.

Single mothers hutokea kwa sababu tofauti na siyo kweli kwamba wote hawaaminiki.

Ukisema single mothers hawaaminiki ni kuwakosea adabu wale single mothers wazuri.

Mimi ninasema hivi, mleta mada ni mpumbavu kiasi fulani.

Hata post yako mwenye inaashiria kwamba ulichokiandika hukiaamini maana umesema mjomba kaachana na mkewe kwa sababu zisizojulikana lakini kwichwa Cha habari unadai tusiwaamini single mothers.
 
Muda wa kujibu swali lako la kejeli ni heri nikautumia kumpeti peti mume wangu,[emoji57][emoji57][emoji57]

Jitahidi sana kumpeti maana siyo wote wanaweza kulipia ma school fees ya watoto wa mabwana zako wengine
 
Jitahidi sana kumpeti maana siyo wote wanaweza kulipia ma school fees ya watoto wa mabwana zako wengine
Mil 3 kwa kila mtoto na wako watoto 3 na hiyo ni kwa mwaka una lingine!!

ukiwa kapuku usifikiri wote wako hivyo
 
Ndugu mwanaume akiachwa au akisalitiwa inauma sana tena sana kuliko hata mwanamke,,Hakuna mwanaume atakaye kubali mke wake achukuliwe na mwanaume mwingine never
 

Tunapojipanga kurejesha mtu Chatto tuweni na mioyo ya huruma na nafsi zingine ambazo kwa sababu zozote zile zinateseka. Huo ndiyo ubinadamu.

Single mother single mother hawa ni binadamu tena wengi wao wanyonge hohehahe. Wengi wanahangaika na watoto waliotelekezwa nao.

Tusiwe kama Mi-CCM, watu hawa (ma single mother) wanahitaji haki, uhuru na maendeleo pia kama ilivyo kwake mleta mada na hata walivyo wachangiaji.

Si sawa kuwanyanyapaa hivi wamama hawa kwa sababu ya unyonge wao tu. Kuwa na staha nao hata na watoto wao ndiyo utu wenyewe huo ambao labda baada ya jiwe kuukiuka wetu ndiyo maana sasa hapatoshi na hatuna suluhu naye tena.

Chuck Norris atoke wapi kuwapigania wanyonge masingle mother hawa wasiokuwa naye wa kuwatetea hata humu JF?

Obama alikuwa mtoto wa single mother lakini akaja kuwa rais wa marekani.

Wakuu single mothers ni wa kuwahurumia badala ya kuwabeza. Kwa maana imeandikwa: "heri wenye huruma ...." Vinginevyo case yetu washupavu sisi na jiwe nini basi?

Nipendekeze kwa MODs, mada hizi zenye kutweza utu wa watu wengine, ni muda sasa wa kuziondoa na kuzitia kufuli.

Haki, uhuru na maendeleo kwa wote wakiwamo single mothers tafadhali.
 
...Ila ukweli ni kwamba 80% ya single mom ni wadangaji wakubwa,coz they have nothing to lose...wanatumia kila njia ili wajihimarishe kiuchumi uku mtaani tunayaona.

Ila wachache sana wenye kujitambua.
 
Mi bado hata sijaona tatizo lipo wapi?

- Alimkuta na mtoto ambaye hakuzaa naye, alizaa na mwanaume mwingine
- Licha ya kumkuta na mtoto alimpenda hivyo hivyo ... ''Licha'' means pamoja na taa nyekundu kuwaka, he decided to take the risk
- Tangu ayumbe kiuchumi
- Anaishi na mwanaume wake wa mwanzo ... Its obvious, ukichukulia mtalaka hatongozwi mkuu

Mungu ni mwema, atavuka tu
 
Si dhambi kuoa Single mother, Si dhambi kabisa, ila ni fedheha kukimbilia Single mother na kuacha Vigori wenzako bila kujua A, B, C in intense research, Kuoa Single mother ni sawa na kununua Nyumba iliyokuwa inakaliwa na mtu mwingine lazima ujue sababu za kuinunua na sababu za aliyeiuza. Ila jitahidi kutokupenda vitu used vina gharama zake kama hukagui vizuri kwa matumizi yako.
 
Why so much hatred kwa hawa wadada /wamama?

Yaani wote wana tabia moja?
Hivi hakuna aliyeoa Single mother na wakaishi vizuri kabisa.
 
Ugomvi wa wanaume na single mother haupo sana kwenye tabia zao kama ambavyo tunaaminishana ila ugomvi huu una historia ndefu kdg.Jamii nzima inashiriki hapa.

Toka zamani enzi za babu zetu wanaume walikuwa wanapenda kuoa bidhaa brand new na kipindi mwanamke alitunza bikra kweli kweli na hata siku ya fungate mashangazi walikuwa wanaenda kupima kama kweli binti alikuwa brand new..

Sasa ugomvi unaanza hapo,deep down wanaume wanapenda mwanamke ambaye hajatumika...maendeleo yalivyokuja kizazi kijeuri kikaingia katikati basi wanaume wakakata tamaa basi wakahamia kwenye binti ambaye hajatumika sana kwa maana ya kwamba atakuwa walau hana mambo mengi kiukweli wote tuliooa saivi krb 95% hatujaoa bikra tutafanyaje zama zimebadilika sana.Leo kuna watu wanakwambia sitaki mwanamke bikra.sasa ki stage mwanamke bikra JAMII imempa thamani kubwa sio tu kwetu wanaume hata wanawake wanajua hilo,anafuata mwanamke aliyetumika bila mtoto na kwanini single mother wanakuwa attacked ni kwasababu jamii inaamini huyu atakuwa katumika kwelikweli hadi kapata mtoto bila kujali ilikuaje kuaje.(No one wants the truth,people are looking for someone to blame.)

Tukumbuke huu ni mtazamo wa jamii nzima sio tu wanaume leo hii ukimwambia dada/mama ako nataka kuoa mwanamke mwenye mtoto,anaweza kukubali kama kakuzoea atakuuliza ina maana wanawake wote hawa hujawaona mpk huyu???na huyo ni mwanamke sio mwanaume...mtaani utasikia wadada wanaongea yule si alizalishwa,mwanaume akamtelekekeza kwa sauti flan km ya kumdharau hivi mwanamke mwenzake,haya wote tunayasikiaga.

Niseme tu jamii ipewe mda kuzoea wanawake wenye watoto kama ambavyo mtazamo ulitoka kwenye bikra ukaenda kwenye aliyetumika napo sawa tu basi na jamii inabidi ikubali kwamba mwanamke mwnye mtoto si alama ya kwamba eti alilala na kijiji kizima ndo mana hadi kapata mimba,Noooo huku mikoani mabinti wengi sana wanapewa mimba na wanaume waliowatoa bikra tena baada ya hapo wanatelekezwa in fact mabinti hawa walishika mimba sababu hawana mdg meaning hawakuwa vicheche..Tusisahau zmn mwnamke akipewa mimba alikuwa anafukuzwa nyumbani ni kama wanamtupa lakini leo,we ulisikia wapiiiiiii?binti kafukuzwa!!!

Picha ya pili sasa kwanini wanaume wanaogopa single maza ni sababu wana historia mbaya na wanaume,Binti aliyempenda mwanaume kwa dhati hlf mwanaume akampa mimba na kumtelekeza lzm ana historia flani chungu sana kuhusu wanaume sasa binti huyu asipojua ku make peace na past yake lazima tu atakuja kuingia kimachale machale sana kwenye mahusiano.Ni hayo machale na mtazamo wake dhidi ya wanaume ambao wanaume wanaogopa...

Dada zangu hii new trend yenu ya kuforce usingle maza eti ukiwa single maza na kazi nzuri ndo unakuwa strong woman siwashauri.Deep down hizi jinsia zetu zinavutana km sumaki kama utaweza kupata mwanaume wakufanya nae maisha bora ufanye nae maisha.Mama angu aliniambia mtunze mkeo hata kama unaona hana thamani sababu utajua thamani yake mkianza kuzeeka..na nyie wadada ukigonga 45 utaelewa why unahitaji kampani pembeni yako sijamwambia mtu ajitongozesheee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sindio utadhani waliambiwa kuwa wasipooa watakufa πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚

Ndoa zimekuwa Ni sehemu ya mateso na jehanamu ya duniani 80% ya waliopo kwenye ndoa wanalia vilio vya mbwa koko na kusaga meno '' Lakini bado tu watu wana ng'ang'ania kuingia katika hilo gereza πŸ˜‚

Tatizo wengi wanaolea genye ..ikiruhusu akili yako iendeshwe na genye utapata shida sana hapa duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…