There is so much judgement ya ma-single mother humu ndani sijui waliwakoseaga nini maskini ya Mungu... kama kweli au sio kweli kuhusu hizi tabia zao mkumbuke some of u ndo mmewazalisha wadada wa watu bila ndoa na mkawaacha... hawa ni mama wa watoto wenu despite it all wao bado ni binadam na hawajakamilika. Sidhani kuna mtu anaamuaga tu kua single mother ni circumstances hutokea na naamini kila mwanamke angetamani mwanae alelewe na mapenzi ya both parents ila ndo hivyo. Hizi tabia zao nyingine (kama ni za kweli) ni kwasababu ya frustrations za failed relationships na majukumu ya watoto sometimes tujaribuni kuvaa viatu vyao...
Tunapojipanga kurejesha mtu Chatto tuweni na mioyo ya huruma na nafsi zingine ambazo kwa sababu zozote zile zinateseka. Huo ndiyo ubinadamu.
Single mother single mother hawa ni binadamu tena wengi wao wanyonge hohehahe. Wengi wanahangaika na watoto waliotelekezwa nao.
Tusiwe kama Mi-CCM, watu hawa (ma single mother) wanahitaji haki, uhuru na maendeleo pia kama ilivyo kwake mleta mada na hata walivyo wachangiaji.
Si sawa kuwanyanyapaa hivi wamama hawa kwa sababu ya unyonge wao tu. Kuwa na staha nao hata na watoto wao ndiyo utu wenyewe huo ambao labda baada ya jiwe kuukiuka wetu ndiyo maana sasa hapatoshi na hatuna suluhu naye tena.
Chuck Norris atoke wapi kuwapigania wanyonge masingle mother hawa wasiokuwa naye wa kuwatetea hata humu JF?
Obama alikuwa mtoto wa single mother lakini akaja kuwa rais wa marekani.
Wakuu single mothers ni wa kuwahurumia badala ya kuwabeza. Kwa maana imeandikwa: "heri wenye huruma ...." Vinginevyo case yetu washupavu sisi na jiwe nini basi?
Nipendekeze kwa MODs, mada hizi zenye kutweza utu wa watu wengine, ni muda sasa wa kuziondoa na kuzitia kufuli.
Haki, uhuru na maendeleo kwa wote wakiwamo single mothers tafadhali.