Ugomvi wa wanaume na single mother haupo sana kwenye tabia zao kama ambavyo tunaaminishana ila ugomvi huu una historia ndefu kdg.Jamii nzima inashiriki hapa.
Toka zamani enzi za babu zetu wanaume walikuwa wanapenda kuoa bidhaa brand new na kipindi mwanamke alitunza bikra kweli kweli na hata siku ya fungate mashangazi walikuwa wanaenda kupima kama kweli binti alikuwa brand new..
Sasa ugomvi unaanza hapo,deep down wanaume wanapenda mwanamke ambaye hajatumika...maendeleo yalivyokuja kizazi kijeuri kikaingia katikati basi wanaume wakakata tamaa basi wakahamia kwenye binti ambaye hajatumika sana kwa maana ya kwamba atakuwa walau hana mambo mengi kiukweli wote tuliooa saivi krb 95% hatujaoa bikra tutafanyaje zama zimebadilika sana.Leo kuna watu wanakwambia sitaki mwanamke bikra.sasa ki stage mwanamke bikra JAMII imempa thamani kubwa sio tu kwetu wanaume hata wanawake wanajua hilo,anafuata mwanamke aliyetumika bila mtoto na kwanini single mother wanakuwa attacked ni kwasababu jamii inaamini huyu atakuwa katumika kwelikweli hadi kapata mtoto bila kujali ilikuaje kuaje.(No one wants the truth,people are looking for someone to blame.)
Tukumbuke huu ni mtazamo wa jamii nzima sio tu wanaume leo hii ukimwambia dada/mama ako nataka kuoa mwanamke mwenye mtoto,anaweza kukubali kama kakuzoea atakuuliza ina maana wanawake wote hawa hujawaona mpk huyu???na huyo ni mwanamke sio mwanaume...mtaani utasikia wadada wanaongea yule si alizalishwa,mwanaume akamtelekekeza kwa sauti flan km ya kumdharau hivi mwanamke mwenzake,haya wote tunayasikiaga.
Niseme tu jamii ipewe mda kuzoea wanawake wenye watoto kama ambavyo mtazamo ulitoka kwenye bikra ukaenda kwenye aliyetumika napo sawa tu basi na jamii inabidi ikubali kwamba mwanamke mwnye mtoto si alama ya kwamba eti alilala na kijiji kizima ndo mana hadi kapata mimba,Noooo huku mikoani mabinti wengi sana wanapewa mimba na wanaume waliowatoa bikra tena baada ya hapo wanatelekezwa in fact mabinti hawa walishika mimba sababu hawana mdg meaning hawakuwa vicheche..Tusisahau zmn mwnamke akipewa mimba alikuwa anafukuzwa nyumbani ni kama wanamtupa lakini leo,we ulisikia wapiiiiiii?binti kafukuzwa!!!
Picha ya pili sasa kwanini wanaume wanaogopa single maza ni sababu wana historia mbaya na wanaume,Binti aliyempenda mwanaume kwa dhati hlf mwanaume akampa mimba na kumtelekeza lzm ana historia flani chungu sana kuhusu wanaume sasa binti huyu asipojua ku make peace na past yake lazima tu atakuja kuingia kimachale machale sana kwenye mahusiano.Ni hayo machale na mtazamo wake dhidi ya wanaume ambao wanaume wanaogopa...
Dada zangu hii new trend yenu ya kuforce usingle maza eti ukiwa single maza na kazi nzuri ndo unakuwa strong woman siwashauri.Deep down hizi jinsia zetu zinavutana km sumaki kama utaweza kupata mwanaume wakufanya nae maisha bora ufanye nae maisha.Mama angu aliniambia mtunze mkeo hata kama unaona hana thamani sababu utajua thamani yake mkianza kuzeeka..na nyie wadada ukigonga 45 utaelewa why unahitaji kampani pembeni yako sijamwambia mtu ajitongozesheee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]