huo ndo ukweli, vingine vyote ni ubinadamu tu
 
Duuh!!! Kwa hiyo
Matokeo bado 2-1
 
Naomba ntakujibu kwa visa Joka maana kuishi kwingi kuona mengi:

1. Kuna polisi kaibiwa mke ambaye alimuoa akiwa vizuri tu, ila akatokea mtu huko akamuiba na mke akahamia kwake. Jamaa kaelekezwa alipo mkewe kamfata kampata ila maelezo ya mke ni kwamba, nifanye itakavyokupendeza ila sikutaki tena. Polisi sasa hivi kakubaliana na hali kaachana nae amemove on ila hakuamini kabisa kilichotokea maana mwanamke alimkuta akiwa vizuri
( Ila nina Ndugu yangu yupo tu na single mother wake hawaachani miaka na miaka)

2. Mzee mwenzangu aliwekewa mtego akanaswa, alishikiwa bastola kwa kosa la kutembea na mke wa mtu, akabebwa mkuku mkuku chini ya ulinzi na njemba mpaka dukani kwa mke wa jamaa, mke kaulizwa unamfahamu huyu akajibu namfahamu ndio na hajui kama nimeolewa ila natembea nae ndio, akamgeukia mumewe akamwambia wewe si upo busy, utajua mwenyewe. Mwenye mke akaona hapa ntaua wangapi? Mzee akaachiwa kuna siku akatafutwa akaombwa msamaha na fidia juu za usumbufu na mwenye mke akakiri mkewe hajatulia amebadilika na kuwa malaya. Tupo na mzee mtaani tukila mvinyo na jamaa mwenye mke kabla ya fumanizi alijua ana mke kweli.
(Ila nina Ndugu yangu yupo tu na single mother wake na kamwongezea mtoto hawaachani miaka na miaka)

3. Kuna mtu yupo na mwanamke aliyezaa watoto 3 alimnyang'anya jamaa huko alikuwa njaa njaa hawezi kuimudu familia.
Jamaa kazaa na mkewe watoto 3, sio kamkuta na mtoto, la ha sha, kamzalisha watoto 3 akajua ila katokea mwamba huko kamtongoza mke wake mpaka kakubali kaanza kumuhudumia mpaka mke akaona ya nn shida, akamkimbia jamaa na kuhama nyumbani.

Watoto wa jamaa wapo nje huko wanasoma kwa fedha za mume mpya.
jamaa ukimpa hii hadithi ya single mama ndo wenye tatizo hatakuelewa maana mkewe(Shemeji yake kwa sasa) ni mwanamke na nusu ila ameshawishiwa na ametulizwa na mwanaume mwingine.
(Ila nina Ndugu yangu yupo tu na single mother wake na kamwongezea mtoto hawaachani miaka na miaka)

HITIMISHO
Vijana ambao hamjaoa tafuteni ukwasi muweze kuzitunza familia na mwanamke akuheshimu lakini la muhimu ni kuomba sana usikosee kuoa.

Achana na formula, hakuna formula ingekuwepo kila mtu angeandikiwa aifuate. Sio kila mwenye matatizo ya ndoa alioa single mother.
 
Ukweli ni kwamba, mwanaume hana maamuzi hata chembe ya kumzalisha mwanamke, na mwanamke asipotaka kuzaa hata ufanye nini HATAZAA...

Wanaoshikilia uskani wa maamuzi ya kuzaa au kutokuzaa ni wanawake, mtu anakaa bila kuzaa miaka yote ya shule, then baada ya kumaliza shule/chuo na kuona age inasogea anadaka mimba na kusema ni bahati mbaya, hakuna bahati mbaya hapo...AMEAMUA KABISAAAA
 
Kama una miaka chini ya 35 na wewe ni wa kwanza na una wadogo zako hata 6 amini nakuambia kuna wanaume wanaweza kumuoa mama yako mzazi na akatulia kwenye ndoa na kumsahau kabisa baba yako kama baba yako ni mwanaume suruali. Hapa siongelei mama mwenye tabia za umalaya wala, Namuongelea mwanamke wa kawaida tu anayejiheshimu akakuzaa wewe kijana below 35 na wadogo zako hata wakiwa 6 na kuwalea ila kaolewa na mwanaume suruali unayemuita baba.

MWANAUME = UKWASI + SAUTI YA MAMLAKA.
 
Kwani kati ya mwanaume na mwanamke ni nani yuko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuhakikisha mimba haipatikani? Wanawake wengi wanajibebesha mimba kwa maksudi kama njia ya kumbana mwanaume ili amuoe, kwa hiyo usiwahurumie sana single mothers wengi wamejitakia, wana misemo yao wanaambizana "mwanamke leba" kisha wanabeba beba mimba tu bila mpangilio.
 
Pesa ndo kila kitu mkuu umenena
 
Reactions: Tsh
Ha ha ha ukiona hivyo ujue imepigwa mshono

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Umri ungeruhusu ningehudumia single mama wengi sana halafu watoto napeleka canada huko wakasome, wana raha sana wasivyotaka kuwasikia baba zao hata kwa kulazimishwa. Nani anataka baba jina? Tena hawa wenye vitoto vya kike unamuongezea viwili avitunze kudumisha undugu.
 
Sawa umemuoa, siku akikuomba kwenda kukutana na mzazi nwenzake ili kupanga maendeleo ya mtoto utamnyima? Hilo ni tatizo la kunywa soda iliyofinguliwa ila kizibo kimeegeshwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fafanua point mojamoja kama alivyoeleza hapo juu mtoa mada ili kusupport maelezo yako,otherwise utakuwa unapinga kwa kuhisi tu...
 
Hivi vitu kwa nyakati tulizonazo ni kuomba tu Mungu..hali ni mbaya sana
 
Nyie ndiyo mnaochochea matumizi ya P2 na abortion.
 
Umezungumza ukweli, nakumbuka kuna siku nimewahi changia mada kama hii nikawa kunyume.

Kuna watu walifikia kunambia najikosha kwa hal single mothers wa humu ilhali hata siwajui.

Single mothers wengi wanajitambua na wanajua thamani ya ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…