Habari wakubwa!
Niliwaambia msiwaoe single mother Ila sikuwaambia msiwapende, wapendeni na ikiwezekana wahudumieni Kama mtaweza lakini sio kuwaoa. Kumuoa single mother ni kutangaza kuwa hujielewi, umechanganyikiwa na kujidharau. Muoe single mother ikiwa umri wako umeenda, yaani ukiwa na miaka kuanzia 50 huko lakini kijana Mdogo kukimbilia mikosi ni kuonyesha hujaelewa vyema na hujafunzwa Mila.
Mahusiano na single mother yawe long distance relationship, kila mtu aishi kwake.
Ili umfurahie single mother Kama utaamua kumuoa utakubidi ufanye mambo haya;
1. Itakubidi umpende yeye mwenyewe
2. Itakulazimu umpende Mtoto wake kama unavyopenda wakwako, ukishindwa hili umekwisha,
3. Itakubidi umpende mzazi mwenza. Yaani ukubali Ume wenza.
Kamwe usimseme vibaya mwanaume aliyemzalisha hata Kama hawajibiki, kwani kumsema mzazi mwenza ni kumsema Baba WA mtoto uliyemkuta naye.
4. Nyumba yako utakuwa inamihimili miwili inayoongoza familia yako. Kuna mhimili uliojichimbia zaidi ambao anaweza kuwa huyo mume mwenza au wewe. Ila kila mmoja ni Mtawala.
Mkeo anaweza kukukatalia Jambo Fulani kumbe ni Oda kutoka mhimili mwingine.
5. Lazima ukubali ku-share bajeti na kipato chako na huyo mume mwenza.
Aidha akulishe wewe au umlishe yeye. Au mkae meza ya maridhiano muwekeane bajeti.
Huwezi MPA adhabu Mkeo ya kibajeti, Kwa mfano Kama Mkeo hutaki anunue nguo Fulani za Sare Kwa lengo la kumuadhibu Kwa kosa Fulani alilolifanya, basi usishangae akapewa pesa hiyo na mume mwenza
6. Lazima ukubali Siri zako zinafahamika upande wa pili.
Single mother wengi Kama sio wote hutoa Siri za waume ZAO wanaoishi pamoja Kwa ma-ex wao.
Probability ya Siri zako kutoka ni ndogo mno. Na hii itategemea na mshikaji Kama Hana mpango naye. Lakini kama anampango naye au anamtamani bado ujue umekwisha.
7. Lazima ukubali kupata ukakasi wakati unamuadhibu mtoto wake(wa mwanaume mwenzako). Jiandae kutokuwa huru na Nyumba yako mwenyewe.
Huwezi kutenda lolote Kama Baba WA Familia Kwa kuhofia kuwa huyo sio mtoto wako.
Asije akakudanganya mtu kuwa utaadhibu Kwa haki, nature ilivyo ni kuwa kumuadhibu mtoto asiyewako(wa mwanaume mwingine au WA mwanamke mwingine) ni KAZI kubwa mno.
8. Lazima ukubali Mkeo(single mother) uliyemuoa kulinda haki za Baba WA mtoto wake pindi zinapoingiliwa.
Kama wewe haki zako atakavyozilinda Kama Baba watoto wake ndivyo atakavyolinda haki za mume mwenza. Usije ukajidanganya hata kidogo.
Wanawake katika hili wapo Sirius na ni nature yao, iko hivyo.
Mwanamke anajua kupigania haki za mzazi mwenzake ni kupigania haki za mtoto wake(mtoto wako WA kambo).
Mfano ipo Kwa kina Muna Love Vs Castro Dickson Kwa mtoto wao Marehemu Patrick.
Mkeo hatakuonea huruma ambayo huistahili Kwa kisingizio unamlea mtoto huyo au Wewe ni mume wake wa sasa.
Wanawake wanachojali ni Kutoa haki za kihisia Kwa watoto wao na Baba zao.
Je utaweza?
Fikiria kabla ya kutenda, usilete utoto kwenye ishu Sirius.
Ushamba wa wanawake usije ukagharimu maisha yako.
Kama na watu wazima wakushauri ukiona umezidiwa kihisia.
Sana zaidi muulize Mama yako yupo tayari alafu yeye atakueleza hali ilivyo, yeye ndiye kakuzaa, ndiye mwenye uchungu na wewe kuliko yeyote.
Mama ako akikubali uoe single mother, OA.