Habari wana jf?
Oyaaaa vijana wapanbanaji acha niwape mnara iko hivi:
Kiburi, jeuri, Nyodo, kisirani, ujuaji, Midomo na kutoridhika na wanachopewa na wanaume wao hizi ni changamoto za single mothers wa Tanzania kwa 90% ni single mothers wachache sana wasio na hizi tabia na huwezi kuwakuta wanabwatuka hovyo humu mitandaoni,,
Single mothers wa humu wote wanasema wanaume ndio chanzo Cha situation zao lakini Kuna walioachwa kwa ajili ya usaliti na umalaya na hawatakwambia na wenyewe wapo humu bila aibu nao wanatulaumu wanaume
Ukiona lijanamke linashinda mtandaoni kujisafisha makosa yake na kurusha lawama kwa wanaume ujue hilo ni jini kisirani usijichanganye mwamba utaisha vibaya,
hapa mtandaoni anajifanya ye malaika, ye ndio kaonewa sasa we jichanganye,, single mothers wa aina hiyo wengi hawanaga shukrani siku maisha yako yakiyumba halafu baba wa mtoto wake ndio kapata hela my friend utalia kichina...[emoji28]
Ni single mothers wachache sana tena wachache sana nasisitiza wachache sana wanaojielewa na huwezi kuwakuta wanachamba watu humu mitandaoni, wako busy na maisha hawana muda wa kupoteza sio hawa wawindaji haramu kijana mwenzangu kuwa makini na hawa viumbe..
Kuna wapanbanaji wenzetu wako jela sasa hivi na wengine wamekufa kwa ajili ya humiliation za hawa single mothers wa kuokota okota mitandaoni..
Mpambanaji mwenzangu ukipata single mother humu usikurupuke kuoa nenda nae taratibu hatua kwa hatua hakikisha unapata taarifa zake sio zile alizokupa bali zile ambazo hajakupa , muhimu sana kuijua familia yake anayotokea, ndugu na marafiki zake wa karibu hii itakusaidia kujua uko na mtu wa aina gani maana ndege wanaofanana huruka pamoja..
Usiamini kila story mbaya atakayokupa kuhusu baba wa mtoto wake, mama zetu huwa hawasemi mabaya yao kamwe siku zote huwa wanasema mabaya ya baba zetu tu! usibebe picha mbaya dhidi ya mwanaume mwenzio huwezi kujua nini kilimkuta kwa huyo mwanamke we kaa kwenye nafasi yako, mchunguze mtu wako utaujua ukweli tumia akili sio hisia..
Usianze mahusiano na single mother halafu ukaanza kuwekeza kwenye maisha yake moja kwa moja hilo kosa litakugharimu kumbuka nimekwambia wengi wao hawana mioyo ya kuridhika wala shukrani.. we msaidie kwenye kile ulichomkuta nacho wakati huo na wewe endelea na ratiba zako za utafutaji ulizokuwa nazo, usibadili malengo Wala mfumo wako wa utafutaji kwa ajili yake we msaidie kwa kile unachoweza ila usimuingize kwenye mifumo yako wala usiingie kwenye mifumo yake, ukiingia tu kwenye mfumo wake anakuunganisha na marejesho utaimba kikorea mwanawane,,
Kama ni single mother anayejielewa utaona siku zinavyokwenda anajiset kuendana na mfumo wako wa maisha kuanzia kwenye mambo ya fedha, nidhamu hadi chumbani yani anaacha anaji sacrifice kwa ajili yako hata kabla hujatangaza ndoa na wala hana uhakika wa hiyo ndoa ila anafurahia uwepo wako kwenye maisha yake na anafanya jitihada za ziada ili uendelee kuwepo kwenye maisha yake my brother huyo ndio single mother wa kuoa sasa sio hawa wawindaji haramu utawapa jasho lako lote na bado hawataridhika watatafuta mwingine awape zaidi kumbuka nature ya mwanamke ni kiumbe kisichoridhika,
MUNGU aliweka matunda ya kila aina bustani ya edeni lakini bado mwanamke hakuridhika akafuata lile moja alilokatazwa na bado leo wanatutupia lawama sisi kwamba haturidhiki wamesahau ndio walitufundisha kutoridhika pale bustani ya edeni [emoji28]
Tuishi nao kwa akili wanangu TUWAPENDE ila TUSIWAAMINI[emoji1666]
Sent from my SM-A115F using
JamiiForums mobile app