Una uhakika kuwa Tz hawapo??
 
Ngoja nitoe story moja labda inaweza kumuinua somebody here. Kuna ndugu yangu flani tumpe jina Abshir. alikuaga na mdada tumpe jina Rosina. Abshir na Rosina were so in love, mahaba ya njiwa kama yote. Wakiwa mahali wanaonyesha mapenzi mpaka sisi watazamaji tunaona. Miaka miwili ikapita hapo Abshir hana pesa, mwenye kimango ni Rosina. So Rosina alikua kama bread winner kimtindo.

Baadae Abshir akampa mimba Rosina. Baada ya Rosina kubeba ujauzito, Abshir akawa kama anajiengua flani ivi. Rosina akanotice, akaja kusema nyumbani kwamba mimi siumuelewi ndugu yenu, mbona kanibadilikia. Basi Abshir akawa anasema "mimi sikupanga nimuoe huyu dada so kaamua kubeba ujauzito kwa lazima. So Abshir akaachana na Rosina. Mtu mzima mmoja tu upande wetu ndie aliekuwaga intouch na Rosina kuuliza maendeleo lakini Abshir yeye na ndugu wengne tukajikataaga completely. So basi bwana, Rosina akajifunguaga mtoto wa kiume akapambana mwenyewe mpaka mtoto akakua.

Huku nyuma Abshir alistruggle kivyake, akaja akaoa mwanamke mwingine. Wakaishi pamoja kama miaka miwili, Abshir akaanza kuugua then akaja kufariki. Kwenye msiba ndipo movie iliponoga. Abshir alikua na mtoto wa kiume mmoja tu ambae alimtelekeza kwa Rosina. Rosina alishapataga mwanaume akaolewaga. Kuna ndugu viherehere wakawa wanadai eti mtoto wa Abshir wa kiume apelekwe kwenye msiba wa baba ake. Mtu mzima yule aliekuwaga in contact nae akampigia simu Rosina na kumwambia bwana bwana. Huku wanasema A B na C. Rosina akamwambia naongea na wewe kwa sabbu weww ndo pekee ulienipa support all this time. Waambie nawaheshimu sana. Please sitaki kelele na mtu. Nina amani kwenye ndoa yangu, just leave me alone. Alishaniacha huyu mtoto ni wa huyu mume wangu. Akakata simu.

Basi mtu mzima huyu akafikisha ujumbe na akasema she is very correct. Miaka yote mmekaa kimya kama ndugu leo mnamuulizia wa nini. Mumuache mtoto wa watu kaolewa na ana amani kwenye ndoa yake. Basi bwana watu sura zikawashuka wakakituliza. Msiba ukaisha..and by the way Abshi hakuwahi kupata mtoto na huyu mwanamke mwingine and nae alikuaga single mother mwenye watoto wawili. It is what it is.

My point hasa ni kwamba, incase yameshatokea ya kutokea kila mtu ashinde mechi zake. Wewe ni mwanamke lea m/watoto wako mwenyewe. Do not try to force yourself kwenye maisha ya huyo mwanaume. Akifanya sawa asifofanya kufa na Yesu wako. Because ukizidi kujisumbua nae sanasana wewe ndo utawaste your life. Ukija kuzinduka miaka 10 imeshaisha na ulikua busy unacheza games za back and forth.

Na wewe mwanaume incase tayari yameshatokea, ni jukumu lako kulea mtoto wako. Kwanini ugongewe hodi lakini. Tuma fedha, kata bima ya mtoto wako ili kuepuka usumbufu. Kama amefika 7 years na unaona kuna drama sana kwa mama mtoto basi fata taratibu mchukue ishi nae au sort it out. Lakini msitumie hiyo nafasi ya kumlea mtoto kama chachu ya kumfanya mama mtoto sex machine. Na wewe unazidi kujipotezea muda na kukaribisha hasara na nuksi kwenye maisha yako. Maana unakuta umeshaoa mwanamke mwingine na huku mnatafunana na huyo mama mtoto sijui mnakua mnafikiria nini.

Lets all be emotionally mature and grow up. Back and forth sex games and drama ni hasara tu. Mistake zikishatokea zimetokea why tunazidi kuzipalia makaa na kuwa wapumbavu kiasi hiki? I really hope and pray kila mtu ajifunze kuwa responsible kwa choices anazozifanya kwenye maisha yake.
 
Pole mkuu,haya masingle mother ya hovyo ndo yanawaharibia wengine wenye heshima na wanaojielewa, shame on them[emoji57]
 
Ukiona mwanaume wa hivyo anataka tu akuharibie kwa mtu wako mwenye future na ww,hakikisha mkiachaha mnaachana kweli na sio reja reja,na single mother mnatakiwa kuwa na misimamo.
 
Duh,umeandika kwa uchungu sana mkuu[emoji120]
 
Nakuibia tu siri ndogo......hao wanawake mliowaoa kwenye nyumba za ibada ndo tunawafaidi sisi sasa

Unaona jinsi ulivyo mjinga, hapa tunazungumzia umiliki, hatimiliki.
Kwani MTU ukiwa na shamba Wezi hawawezi kukuibia?

Unazungumzia mambo mawili tofauti. Ndio maana Wanawake wanawaona Vijana WA siku hizi ni vichwa panzi.
 
Single mother chenga mi hata sishauri kwa kijana ambaye hajaoa kuoa single mother , hao wanatakiwa wapambane na madanga ya mjini , ukioa single mother hakikisha ana pesa chafu yani weww uwe kibenten
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…