Hayo yameshatokea tunao ndugu zetu wanaishi huo mfumo ndio mana tunakuja hapa kukemea kila siku maana tunaona madhara yake. Inakuwa ni mzigo kwa ukoo na inaharibu heshima ya familia.
 
Labda MUNGU awe ATHUMAN ila kama ni huyu MUNGU wa kwenye bible na Quran sahau hilo jambo kutokea kwenye kizazi changu mimi. Hicho kirusi hakitaingia katika ukoo wangu kuanzia watoto, wajukuu, vitukuu hadi Vilembwe na vining'ina.
Ok,Yesu ALILELEWA na baba mzazi au baba was kufikia(baba wa kambo)hapa DUNIANI???(rejea kwenye Bible history ya Yesu)
 
Ok,Yesu ALILELEWA na baba mzazi au baba was kufikia(baba wa kambo)hapa DUNIANI???(rejea kwenye Bible history ya Yesu)
Yesu yupo wapi saa hii tukiongea hapa? [emoji23][emoji23][emoji23]

Maana naona unajizima data.
 
Acha kututungia story hapa, leta mstari unaosema hayo maelekezo.
1Timotheo5:8 Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini:Naye amekuwa mke wa mume mmoja 10 Naye ameshuhudiwa kwa matendo mema.
11 Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao,maana,wakizidiwa na tamaa kinyume Cha Kristo,wataka KUOLEWA.
NB:Kasome kwa kirefu kuanzia mstari wa 8 hadi 16
 
Yesu yupo wapi saa hii tukiongea hapa? [emoji23][emoji23][emoji23]

Maana naona unajizima data.
Wewe umesema Mungu was Bible, Quran.
Nimekuuliza TU habari za Bible
Wewe hujui Bible Wala Quran,maana hujui unachokisema🀣🀣🀣🀣🀣
 
UCHUNGUZI; VIJANA HAWA HAWANA TATIZO NA KUOA SINGLE MOTHER ; WANAOA BILA SHIDA YOYOTE.

Anaandika, Robert Heriel

Wimbo wa Single mother ni Wimbo maarufu na Mkongwe Duniani, tulizaliwa tukaukuta na bila Shaka tutakufa na kuuacha ukiendelea kuimbwa.

Lakini uchunguzi wangu unaonyesha kuwa Single mother sio tatizo Kwa baadhi ya wanaume. Ninaweza kusema Kwa hapa nchini 80% ya wanaume hawana shida wala tatizo la kuoa single Mother. Wao wanauwezo WA kuoa na ikawa Fresh tu. Hiyo 20% iliyobaki ndio hawa Vijana wanaopiga kelele humu mitandaoni.

Uchunguzi wangu unaonyesha kama ifuatavyo;

A; WANAUME AMBAO HAWANA TATIZO KUOA SINGLE MOTHER NI KAMA IFUATAVYO;

1. Wanaume wa vijijini ambao hawajasoma au wanaelimu ndogo.
Uchunguzi wangu unaonyesha kuwa Vijana wengi wa vijijini hasa ambao hawana elimu kabisa ya shuleni au wenye Elimu ndogo wao hawana tatizo la kuoa Single mother, hiyo kwao sio changamoto kabisa. Kwa bahati nzuri kulingana na Sensa ya mwaka jana, 2022 asilimia 80 ya Watu walioko Tanzania wanaishi vijijini, ikimaanisha pia 80% ya Vijana wapo vijijini.

Hivyo kama Mwanamke ni single mother na anataka kuolewa basi target yake ya Kwanza afikirie kijijini.
Tatizo linaanzia pale ambapo Wanawake wengi wanapenda Vijana wenye hadhi Fulani, Vijana Wasomi na wenye mambo ya mjini au ya kimataifa.

2. Wanaume Watu wazima na Wazee na Wagane!
Wanaume wenye umri kuanzia miaka 45 kuendelea wao hawaoni shida kuoa Mwanamke mwenye Mtoto. Kwao hiyo sio shida kabisa. Shida itabaki Kwa Waolewaji.

Uchunguzi wangu unaonyesha kuwa Single mother wengi wapo Chini ya udhamini WA wanaume Watu wazima aidha Kwa kugeuzwa nyumba ndogo, au kuolewa kabisa.

Tatizo linakuja Wanaume wa umri huu sio wote waliofanikiwa kimaisha, na umri huo Kwa mwanaume inatakiwa awe ameshafanikiwa kimaisha. Sasa waliofanikiwa kimaisha Kwa nchi yetu Kwa umri huo ni wachache Kutokana na nchi yetu ni Maskini.

Single mother wanalipenda Soko hili lakini Kwa bahati Mbaya solo hili kulingana na Sensa ya mwaka 2022 ni wachache Sana ukilinganisha na Vijana walio katibya umri wa miaka 18-44.

Kundi Hilo ni wachache na katika hao wachache waliofanikiwa ni wachache zaidi Hali hiyo inafanya kundi hili lisiwe best target.

3. Wanaume wa uswahilini na wasio na Elimu
Uchunguzi wangu Kwa maeneo ya uswahilini kama Tandale, manzese, mwananyamala, Buza, magomeni, Mbagala n.k. Single mother anaweza kuolewa hata mara tano ilhali Asiye-single mother akiwa hajapata hata ndoa moja.

Kuoa single mother uswahilini sio tatizo, Vijana wengi nimewaona wakioa single mother wa Huko uswahilini. Tatizo linakuja kuwa Vijana hao wengi Hawana Elimu na Maisha Yao ni Duni. Na wengi wanaoa Wanawake single mother wenye kazi kama Umama ntilie, na vibiashara vidogodogo ili nao wapatemo.

Single mothers wengi waliosoma na wenye Daraja la Kati kamwe hawatokubali kuolewa na aina ya Vijana wa uswahilini Kutokana na mitazamo na Maisha waliyoyachagua. Hivyo kundi hili pia sio chaguo sahihi Kwa single mothers wengi.

4. Wazungu
Wazungu wanaokuja Tanzania na kuondoka baadhi Yao Hawana shida kabisa kuoa single mother. Nina Rafiki zangu wengi ambao ni single mothers wameolewa na Wazungu. Kwao hilo sio tatizo. Changamoto ni kuwa kiwango cha wazungu wanaokuja Tanzania ni Kidogo Sana na hakikidhi idadi ya single mother ambao watataka kuolewa.

B: WANAUME WANAOKATAA SINGLE MOTHERS
1. Wanaume wanaoishi mijini wenye age 20-40.
Iwe Dar, Morogoro mjini, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Moshi n.k
Wanaume wa mjini wengi hawataki kabisa kuoa single mother, Ila wanataka kuwatumia.

2. Wanaume wenye Elimu kubwa wenye age 20-40
Hawa wengi hawataki kusikia habari za single mother. Kati ya wanaume kumi basi Tisa hawataki kuoa single mother.

3. Wanaume ambao tayari walishazalisha Wanawake lakini bado hawajaoa
Kundi hili halitaki kuoa single mother licha ya kusababisha Wanawake kuwa single mothers. Yaani hawa wengi wao ndio wanaopiga kelele mitandaoni kuwa hawataki kusikia habari za single mothers na kijana akitaka kuoa single mother wanamshangaa.

Unajua ni Kwa nini?

Hawa ndio wanajua ukweli kuhusu single mother Kwa sababu ndio wanaowasiliana nao kama Wazazi wenza,
Uchunguzi wangu unaonyesha kuwa, Wanaume waliozalisha Wanawake na kuwaacha huendelea kuwasiliana huku Wanawake ndio wakiwa wanalazimisha mawasiliano na Wanaume waluowazalisha.

Jambo hili ndilo linawafanya wanaume hao kukosa Imani ya kuoa single mother kwani wanajua Kwa hakika bado kuna mawasiliano ya Siri yanayoendelea baina ya Mwanamke na Mzazi Mwenza.

NINI KIFANYIKE;
1. Mwanamke usizae Kabla ya Ndoa, na kama utaamua kuzaa basi uache lawama.
Elewa kuwa kwenye Hii Dunia Mwanamke anatawala mambo Mawili tuu ambayo ni SEX na REPRODUCTION.

2. Vijana acheni kuchezea Watoto wa Watu. Kama unajua Binti haumpendi ni Bora utumie kinga.

3. Single mother msiwasiliane na Wanaume waliowazalisha ikiwa mmeshaachana. Mbona wao hawawapigii simu. Kama ni ishu ya mtoto, wapelekeeni Watoto wao. Kama huwezi kuwapelekea na hawawatafuti basi Achanani nao.

SIngle mother eleweni kuwa kila mnayowasiliana na hao babydady wenu taarifa zote wanaume wanazo kwani hao mnaowasiliana nao ni washikaji zetu, Kaka zetu, wadogo zetu na watoto wetu.
Hakuna mwanaume yeyote ambaye atavumilia wewe kuwasiliana na Mzazi mwenzio. Iwe Kwa Siri au Kwa wazi.

Mwisho, uzinzi sio mzuri na unamatokeo Hasi kwenye jamii.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
ubarikiwe sana
 
2. Vijana acheni kuchezea Watoto wa Watu. Kama unajua Binti haumpendi ni Bora utumie kinga.
Mkuu, kutumia kinga isiwe option.

As long as Mwanamke uliyenaye hujamuoa, hakikisha unatumia Kinga wakati wote.

Usisikilize Mwanamke yeyote atayesema Condom zinamuwasha, mara sijui hajisikii utamu ukitumia Condom, au Condom inamuumiza. Huo ni MTEGO.

Once utakapotia bila Kinga, hakikisha upo tayari kwa Matokeo yeyote na uwe responsible.

Be a Man & Thank me Later
 

Ni kweli Kabisa
 
Single mother wawekwe kwenye lasimu yakatiba mpya wanazid kua wengi kila leo
 
kama ana hela sina tatizo nae kabisa yani, mapema tu jiko linawekwa ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…