Habari za mida hii... i hope Wana jf mpo salama kabisa...twende kaziii

Kwenye king'amuzi cha azam saizi kuna channel mpya Zamaradi tv haina miezi mingi tokea iwe on air rasmi.
Kuna kipindi kinaitwa single mothers ni kipindi kizuri kiasi Kama hao masingle mothers wataongea point jinsi walivyotoka kwenye 0 mpaka kuwa hero.

Kisa mpaka nikaandika huu uzi....Jana mida ya saa tisa mchana ilikuwa ni marudio ya kipindi cha single mothers na mgeni or single mother alikuwa ni Nakaya ni msaani wa hip-hop wa zamani kidogo kwa sasa hafanyi muziki(vijana wa amapiano mtuache kidogo😄) nikaona ngoja niwatch hiki kipindi namuamini Nakaya ni mwanaharati anatoa madini hapa jinsi alivyopitia kuwa single mother mpaka kufika hatua nzuri za kulipa bills za mtoto na maisha yake kwa ujumla kwa kiasi chake alitoa madini ambayo masingle mothers ukiangalia kipindi kile utajifunza.

Wakati anazidi kuulizwa maswali na Zamaradi, kuna swali aliulizwa kuhusu baba wa mtoto, Nakaya alitumia muda mwingi kuongelea mabaya ya mume aliyezaa nae akimuita majina mbalimbali yasiofaa mara alikuwa marioo or mwanaume asiye na future yeyote, nikaona hiki kipindi kimeletwa kwa dhumuni la kumsema mwanaume, kwanini kila likija swala la mtoto masingle mothers lawama zote kwa mwanaume wakati wote tuna haki ya kumtunza mtoto

Kwa leo naishia hapa
It's me Mohammed wa 5 mtoto wa kanali mtata
 
Nadhani kuna aina nne za single mothers:

(1) Waliokuwa wameolewa lakini waume zao wakafariki

(2) Waliopewa mimba na wanaume waliokuwa wakitaka kuwaoa lakini mazingira yakabadilika wanaume hao wakahama au wakahamaishiwa sehemu nyingine na mawasailiano baina yao kukatika kabla hawajaona,

(3)Waliorubuniwa au kudanganywa kuwa wanaolewa na kupewa mimba kabla ya ndoa kisha kuachwa njiani,

(4) Waliozaa bila kujua wamezalishwa na nani au walizaa na mtu ambaye hakuwa mme wao na hakuwa commited bali ilikuwa one time chap-chap.

Nawaheshimu sana wale wa aina ya kwanza na aina ya pili lakini hawa wengine nawapa heshima ya hivyo hivyo tu
 
Huyo namba moja anaitwa MJANE...

Singo maza ni wale wanawake wanaolea watoto peke yao ijapo baba wa mtoto yupo hai..
 
Mjane ni mwanamke aliyefiwa na mume wa ndoa...
Sijapinga hilo, ila anakuwa anelea watoto wake akiwa hana mme. Single mother ni mwanamke anayelea watoto peke yake bila kuwa na mme. Ninajua kuna wanawake wajane na watalikiwa wanachukia hiyo label ya single mothers lakini ndiyo hivyo. Mjane mwenye watoto ni single mother kwa sababu analea watoto peke yake na jimbo liko wazi.

Ni kama ambavyo wajane wa Kiume wanaolea watoto pia walivyo single fathers.
 
Ongezea hii
1. Ma House girl waliopewa mimba na mabosi zao
2. Wanafunzi wa Primary au Sec waliopewa mimba na wenzao au bodaboda katika umri mdogo.
 
5. Waliotegeshea mimba kwa makusudi
 
Acha mawenge mkuu,nilitegemea kukutana na kitu tofaut na icho ulichosema may be alikua anamu-harass ama kumpiga ,sasa mwanaume kuwa marioo ukisemwa kuna shida gan?!
 
Acha mawenge mkuu,nilitegemea kukutana na kitu tofaut na icho ulichosema may be alikua anamu-harass ama kumpiga ,sasa mwanaume kuwa marioo ukisemwa kuna shida gan?!
Ina shida mkuu ata kwa future ya mtoto badae,ata nakaya Ana mabaya yake jamaa kaamua kuchill kimya tu, kwenye swala la usingle mother mwanaume anashambuliwa sana wakati 50/50 ya malezi ni baba na mama .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…