Nasoma comment za Single Mother humu nabaki nacheka tu....Yaani mtu amepigwa mimba hakuolewa na aliyempa Mimba leo hii unataka ujiingiza kichwa kichwa, au unakutana na Mwanamke alishindwa kujenga ndoa yake au mahusiano yake akamua kufunga virago leo hii unadhani utamuweza kweli? Ninachojua Aliyewahi kula Nyama ya Binadamu hawezi acha kamwe..

Case Study, Flora Mbasha ile ndoa ya pili ya Mbwembwe nayo ipo chali ..Single Mothers are very complicated to any new relationship
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie, huyo mama pengine ana binti ambaye anaweza akawa single mother mtarajiwa na hajui hatma yake.

Kubaliana na mwenza wako abebe mimba, Mimba ikiwa changa pitisha ndoa hata km ya mkeka.
Familia zetu za kiswaili ni balaa aisee...mtu hataki nduguze waoe wanawake wenye watoto wakati huo huo akija mtu anataka kuoa ndugu zao wenye watoto hata watatu huwa hawakatai kwamba ndugu yao ana mtoto.

"hii inaitwa "spear for pig"..."mkuki kwa nguruwe......"
 
Hawa mama zetu ni wa kwenda nao hivo hivo ndugu. Mdogo wangu me ameoa mwanamke ambaye alishazaa na mwanaume mwingine na ndoa yao ina zaidi ya mwaka wa saba huu hatujawahi hata kusikia malalamiko miongoni mwao.

Jambo la kushangaza sana mama yetu mkubwa ambaye alizaa na mwanaume mwingine akaja kuolewa na na baba yetu mkubwa ambaye sio baba wa yule mtoto wa kwanza, yeye ndio alikuwa pingamizi namba moja kwa maneno na kashfa kibao kwamba oooh kusoma kote huko utaoaje mwanamke aliyezalishwa na mwanaume mwingine? maneno chungu nzima ya kuudhi na kukera, mimi binafsi nilishindwa kumvumilia ikanilazimu kumuuliza kwamba mama mkubwa kwani wewe mbona umeolewa na huyu baba yetu mkubwa ilhali yeye sio baba wa huyu mwanao wa kwanza?! Jopo zima katika kikao kile walibaki kimyaaaaaaa akiwemo na yy na hadi leo hasemi maneno ya kukarahisha kuhusu single moms
 
"Single Mothers are very complicated to any new relationship"uko sahihi sana...
 
Wajomba na ndugu zangu wote wa kiume wameniambia hivyo hivyo,kama tulikuwa wote vile

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nina experience na hao watu, nimejifunza mambo mengi sana kuhusiana na single mother, na hapa ninvyokueleza ni karibuni tu tangu nimeachana naye, namshukuru Mungu koz sikufikia hatua ya kufunga naye ndoa, suala la kuoa ni sensitive sana siyo la kukurupuka, ili ninyi muweze kuoana na kuishi mjue ni matokeo ya agreement ya wazazi wa pande zote mbili, tofauti na hivyo baada ya miaka utakuja kuitwa single father na itakugharimu maisha.
 
Hii yako ni safe kama anakupenda na umeliona hilo. Asijekuwa naye anaolewa kutimiza masharti tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
hapo ndo pananipaga maswal asee mana miaka kadhaa nyuma alikuwa na mashauz flan kuwa haez kuwa na mtu mwenye mwil mdgo mdgo ila later baada ya umr kusogea akaanza kulia lia kuwa familia wanamuulza ataolew lin

Sent from my GT-I9505 using JamiiForums mobile app
 
Yap,kaniambia hivyo hivyo,kasema anawajua sana wanawake kwasababu yeye mwenyewe Ni mwanamke

Sent using Jamii Forums mobile app
Najua hutapendezwa na hilo ila ndiyo uhalisia. Kwanza mwanamke kakuzidi umri, pili ana mtoto wa mtu. Hawa wanawake wa JF wanashinikiza kuwa usimsikilize mama yako ni wale wale. Achana nao. Wanaume wa JF wanaokushauri ati sikiliza moyo wako, ni wanafiki wanataka uoe na yakikufika wakucheke. Mwanaume kuoa mke ambaye anakuzidi kipato, urefu, umri, kisomo hata akiwa na kiumbe cha mwanamme mwingine muogope kama ukoma.

Usisahau girlfriend ni wako tu ila mke ni wa familia ndo maana tukitaka kuoa tunaulizia maoni ya walio karibu nasi ila kutafuta mchepuko au girlfriend huwa tunaangalia sura na michura peke yake.
 
Una uhakika? Kwani ulimpima DNA? Kwani kuna tatizo gani akikueleza baba yake alikufa ili aolewe na akishaolewa baba anafufuka!!!
ha ha ha,, noma sana asee, kuna wakt alivonambiaga jamaa ake alivuta skumuamin nkahis labd ana hasira nae tuu, ila pia sijawah pata uthibitisho wowote asee

Sent from my GT-I9505 using JamiiForums mobile app
 
"Single Mothers are very complicated to any new relationship"uko sahihi sana...
Mkuu single mother hawajutii Kuchukuwa Umazi wa kucancell aina yoyote ya mahusiano, pia ni wepesi wa kulinganisha matukio ya Nyuma yaliyomkuta kwenye mahusiano mama na hayo Mapya aliyomo. In short ile dhambi ya kukimbia mahusiano yake ya kwanza yanakuwa kama laana kwake hivyo haoni hofu tena kuachika na kuwa kama alivyokuwa Mwanzoni.

Kwa kuongezea pia ni wagumu kubadilika maisha waliyoishi kipindi kile waalichoachana na huendelea kuhitajia kushi kiuhuru zaidi kuliko mbaya zaidi Hawawi na heshima kwa kuwa wanachoamini kuwa Wanaume ni wamoja.

We love them but very complicated
 
Naunga mkono hoja. Halafu asilimia kubwa ya Single mother ni wepesi wa kutamka nioe au tufunge ndoa. Yaani unashangaa haraka haraka tu analitamka hilo neno. Hapo akili kumkichwa! Yapasa mwanaume kutafakari hapa.
 
Jiulize mwenzio alishindwa nn hadi akasepa zake? Hakuna mwanaume anaacha mwanamke anayejielewa hata siku tena baada ya kuzaa nae
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie, huyo mama pengine ana binti ambaye anaweza akawa single mother mtarajiwa na hajui hatma yake.

Kubaliana na mwenza wako abebe mimba, Mimba ikiwa changa pitisha ndoa hata km ya mkeka.
Wanawake sisi jamani, huwa tunawalaumu tu wanaume humu kusimanga single moms ila wazazi pia ni changamoto haswa wa kike. Nililishuhudia hili wakati kaka yangu fulani alipotaka kuoa mwanamke mwenye mtoto, mama yake ndio alikuwa wa kwanza kunyanyua mdomo.

Bahati nzuri nae alikuwa na binti mwenye mtoto tayari. Nilimuuliza tu "je unapenda binti yako siku moja aolewe na awe na familia yake?" Alijibu "ndio" bila kufikiria kwanza. Nikamuuliza tena "utajisikiaje akinyanyapaliwa na wakwe kwasababu ana mtoto tayari?"

Hapo ilibidi awe mpole na aibu juu. Ndoa ilifungwa na maisha yanasonga vizuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…