Hii ishu imekuwa ikinisumbua Sana kutoka mwaka jana,Kuna mwanamke single mother nataka kumuoa,tangu siku ya kwanza nimwambie mama angu hizo habari alionesha kwa wazi kabisa kutokukubaliana nami, ananiambia yeye Kama hakuniweka tumboni miezi Tisa Basi nimuoe huyu single mother,mashangazi nao na dada zangu nao wananisema chini chini,
mdogo wangu wa kike ndo huwa ananivujishia hizo habari kuwa shangazi huwa anasema Mimi Ni mwanaume niliyesoma na kukamilika inakuaje naoa single mother,mama mdogo ndiyo ameniita Mimi mpumbavu,hiyo nimeinyaka kwenye group lao la whatsapp kupitia simu ya mdogo wangu
Baba yangu kaniambia niwe makini Sana kuoa mwanamke mwenye mtoto ila uamuzi nichukue mwenyewe,hii inaniweka njia panda Sana ,najua humu Kuna wamama watu wazima na wazee wenye umri mkubwa na busara,naombeni maoni yenu[/URL]