Kuoa Single Mama ni sawa na kunywa soda iliyofunguliwa na kuonjwa
Kijana kuwa makini sana, hawa wanawake waliozaa waweza kuoa ila wanamatatizo makubwa sana, saivi unaona ni sawa kwa kuwa mpo katika kipindi cha uchumba ila ukishaanza kuishi naye furaha yako itakata.

Mwanamke aliyezaa anaheshimu wanaume wawili aliyezaa naye akimpigia simu atamjibu kwa heshima kwa kuwa ana mtoto wake, wewe pia akimpigia simu atakujibu kwa heshima kwa kuwa unaishi naye, na katika maisha mwenye wivu zaidi huwa ni Sisi wanaume kwa kuwa tumeagizwa upendo kwa wake zetu, tafakari na uchukue hatua.
 
Shida ni mtoto wake? kabla hamjakutana huyo mtoto alikua analelewa vipi? na je mtoto wake ataathiri vipi mahusiano yako na yake au yake na familia yako??

Shida ni umri wake? je anakua anakubeba mgongoni na kutangazia uma kua amekuzidi umri au umri wake unaathiri nini mahusiano yako na yake au yako na familia yako?

Kuna anko wangu alipingwa vikali kuoa single mom, anko akaziba masikio kaweka kitu ndani, huu ni mwaka wa 9 wapo wote, na watoto wao.

Be crazy, Be Weird, Be whatever coz life is too short to be anything but HAPPY.
Umejenga hoja vizuri sana Mkuu
 
Hii ishu imekuwa ikinisumbua Sana kutoka mwaka jana,Kuna mwanamke single mother nataka kumuoa,tangu siku ya kwanza nimwambie mama angu hizo habari alionesha kwa wazi kabisa kutokukubaliana nami, ananiambia yeye Kama hakuniweka tumboni miezi Tisa Basi nimuoe huyu single mother,mashangazi nao na dada zangu nao wananisema chini chini,

mdogo wangu wa kike ndo huwa ananivujishia hizo habari kuwa shangazi huwa anasema Mimi Ni mwanaume niliyesoma na kukamilika inakuaje naoa single mother,mama mdogo ndiyo ameniita Mimi mpumbavu,hiyo nimeinyaka kwenye group lao la whatsapp kupitia simu ya mdogo wangu

Baba yangu kaniambia niwe makini Sana kuoa mwanamke mwenye mtoto ila uamuzi nichukue mwenyewe,hii inaniweka njia panda Sana ,najua humu Kuna wamama watu wazima na wazee wenye umri mkubwa na busara,naombeni maoni yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza baba yako hakubaliani na wewe ndo maana anasema uwe mwangalifu. Mama yako anakutakia mema maana anajua mateso utakayopata ukioa single mother. Msikilize mama yako tafuta asiye na mtoto
 
Ndugu yangu,
Hakuna mzazi anayependa kuona kijana wake anoa single mother hata siku moja. Tatizo huanza tu unapowashirikisha.

Ukitaka kuoa single mother, shtukiza tu. Na ikiwezekana wafiche kwamba hajazaa ili baadae hata wakijua nawe useme hukujua lolote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nimepata vigezo vya mtu mwenye kujiweza.....
Hela
Nyumba nzuri, ikoje nzuri?
Gari....
Ngoja nijitahidi nikiwa mkubwa....
Ana mtoto mmoja wa 4 years,kiukweli najiweza hela + nyumba nzuri + gari ninavyo,kibongo bongo hivi ndo viashiria vya mtu anaejiweza, kuhusu historia kwa kweli sijawaambia

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuelewa mkuu tafuta wazee wa hekima muelezee mkasa wote,waombe wakawaelezee wazazi...amini mambo yatakua poa..
Labda kama huyo single mother alizaa na ndugu yako au ni mchepuko wa baba

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawatomwelewa ng'o ....wanaweza kuitikia kuanua ngoma juani ila hakuna atakaempenda huyo mwanamke....

Hawa .....;
mama mkwe
Mawifi
Mashangazi
Mama wadogo

Ni kichefuchefu muda mwingine


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nirudie tena usemi wa mzee mwenzangu

Kuwa makini saana kuoa mwanamke mwenye mtoto, lakini uamuzi ni wako.

Kuna kila uamuzi kwenye hiyo kauli. Nikupongeze kumpata baba mwenyebusara na mama mwenye hekima, vile vile hukufungwa kuwa na maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja nilitaka kuoa,akanzia keep niletea mambo yake pamoja na kutaka kujua mshahara wangu,nifanye haraka nipeleke mahali kwao,amezoea kuvaa jeans aina ya suruali na mambo mengi,

Nikasema asante mungu huyu umenionesha tabia yake mapema ,mwanaume nikapiga kimya ila bado ananiomba ela

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka icho kitendo hakijaribiwi wazazi wameona mbali kiumri kakuzidi tayari ni mke wa mtu huyo anachofata kwako ni unafuu wa maisha ila kurudi kwa mume wake ni lzm unapotea shida ya vijana wakikutana na mwanamke mkubwa sbb anaweza kumpa kila siki anaona ndo kayapatia maisha maisha ni zaidi ya kufanya mapenzi
 
Moja nilitaka kuoa,akanzia keep niletea mambo yake pamoja na kutaka kujua mshahara wangu,nifanye haraka nipeleke mahali kwao,amezoea kuvaa jeans aina ya suruali na mambo mengi,

Nikasema asante mungu huyu umenionesha tabia yake mapema ,mwanaume nikapiga kimya ila bado ananiomba ela

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuvaa suruali na enyewe ni kigezo eti cha kutokumuoa mtu? Labda ungesemea mengine hayo mkuu watu tumevaa suruali toka utotoni mpaka tunaolewa tuna watoto suruali tunavaa haijawai husiana na tabia ya mtu iyo
 
Back
Top Bottom