Kuoa Single Mama ni sawa na kunywa soda iliyofunguliwa na kuonjwa
Ana mtoto mmoja wa 4 years,kiukweli najiweza hela + nyumba nzuri + gari ninavyo,kibongo bongo hivi ndo viashiria vya mtu anaejiweza, kuhusu historia kwa kweli sijawaambia

Sent using Jamii Forums mobile app
tatizo hawamuhesabu kama mjukuu wao.
ni mtoto wa kawaida kwao.
wazee wanapenda kuibeba damu yako sio damu ya MWENZAKO.pia majukumu wanaona unabeba mzigo usiokuwa wako.
MIMI NINA MWANAMKE ANA MTOTO MMOJA.
ila sintokuja kumuoa.
ntaanzia wapi kumpeleka kwa wazee?
TAFUTA MWINGINE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ana mtoto mmoja wa 4 years,kiukweli najiweza hela + nyumba nzuri + gari ninavyo,kibongo bongo hivi ndo viashiria vya mtu anaejiweza, kuhusu historia kwa kweli sijawaambia

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama huku ndiyo kujiweza basi hujitambui mkuu....na kwa huyo mwanamke ukubali kushare papuchi na mwenye mtoto
 
Ushauri wa wazazi/ndugu kuwa nao makini,sio mara zote wako wrong na sio mara zote wako right,...hivyo utulivu na kumuomba Mungu ni mhm sana...hapa waweza shauliwa lkn majibu ya mwisho unayo ww maana ndio unayeifahamu tabia ya huyo mwanamke....sio wanawake wote wenye watoto wana tabia mbaya na sio wote wasiozaa wanatabia njema...kwa hiyo kupanga ni kuchagua.
 
Hii ishu imekuwa ikinisumbua sana tangu mwaka jana. Kuna mwanamke mwenye mtoto nataka kumuoa, tangu siku ya kwanza nimwambie mama yangu hizo habari alionesha kwa wazi kabisa kutokukubaliana nami. Ananiambia kama yeye hakuniweka tumboni miezi tisa basi nimuoe huyu single mother. Mashangazi nao na dada zangu nao wananisema chini chini.

Mdogo wangu wa kike ndo huwa ananivujishia hizo habari kuwa shangazi huwa anasema mimi ni mwanaume niliyesoma na kukamilika inakuwaje naoa mwanamke mwenye mtoto? Mama mdogo ndiyo ameniita mimi mpumbavu, hiyo nimeinyaka kwenye group lao la Whatsapp kupitia simu ya mdogo wangu.

Baba yangu kaniambia niwe makini sana kuoa mwanamke mwenye mtoto ila uamuzi nichukue mwenyewe.

Hii inaniweka njia panda sana. Najua humu kuna wamama watu wazima na wazee wenye umri mkubwa na busara, naombeni maoni yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pole sana ..akili kichwani mwako..
Kuna mtu ninayemfahamu alikataliwa kuoa mwanamke kama uyo kisa ana mtoto ,jamaa akasikiliza maneno ya familia akasahau ile familia haiendi kuishi na yule mwanamke yeye ndo ataishi nae...jamaa akaachana na yule mwanamke ..akaa kwa mieezi sita hivi akaja kutambulisha msicha mmoja hivi kuwa anataka amuoe huyo hapo wazazi wakafurahia kweli kweli nakumwambia huyu sawa ,hatua zote za utambulisho+ndoa zikafanyika na baraka za wazazi juu lakini kuna kitu kimoja walikikosa katika maisha yao ni MTOTO huu mwaka wa 11 sasa wamehangaika kila mahali lakini hawajafanikiwa.

kwahiyo kazi kwako akili ya kuambiwa changanya na ya kwako
 
kitu gani kinatokea mpka MTU anaoa mwanamke mwenye mtoto na aliezaa nae yupo?
 
"Baba yangu kaniambia niwe makini sana kuoa mwanamke mwenye mtoto ila uamuzi nichukue mwenyewe." Ushauri gani tena unataka.. baba kasema kuwa makini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakubwa ninaamini wote mlioko huku (achilia mbali watoto wa shule) ni watu wazima. Katika kundi hili kuna wanawake na wanaume. Na katika hawa kuna waliooa, kuna waliolewa, na kuna ambao bado hawajaoa/olewa. Katika makundi yote haya ninaamini kuwa kuwa wenye watoto wa kike (mabinti) na wengine hata wameolewa/hawajaolewa au bado wanasoma. Na katika hao ambao hawajaolewa hujui kesho yake ikoje. Likewise hapa kuna wanaume mna dada zenu ambao nao kwa hakika wako ambao hawajaolewa kwa kuwa wanasoma au bado kupata mume na pengine wako ambao wameshazalia nyumbani au ambao kwa hakika ni wagumba (hatuombei hili). Kwa wale ambao hatujaoa hakika unatamani Mungu akupe watoto wa kike na kiume, na hapo sasa hujajua hawa watoto hasa wa kike future yao itakuwaje--- hapa tegemea watakaozalia nyumbani, tegemea watakaoolewa, tegemea ambao hawataolewa kabisa maishani mwao, tegemea pia wagumba (hatuombei). Sasa kwa yote hayo machache nashangaa sana wanaume na wanawake ambao wanabeza sana mabinti waliozalia nyumbani kana kwamba siyo watu, hawa nao ni watu na hatujui circumstances zilizopelekea kuzalia nyumbani. Kwa misingi hiyo hebu tuheshimu hawa single mothers kwa kuwa nao ni watu na wanahitaji kuheshimika.

Sasa ndugu zanguni kuoa na kuolewa ni mapatano.Kesho utaoa ambaye siyo single mother ukaishia kuwa na ndoa ngumu kuliko JIWE au JABALI na ukaoa huyo single mother ukapata mke mwema kabisa na maisha yakasonga mbele. Cha msingi ni wewe kuangalia kwa makini na KUMSHIRIKISHA MUNGU MNO KATIKA MAAMUZI YAKO IWE NI SINGLE MOTHER AU NI FRESH MOTHER (UTAJUA MWENYEWE HOW YOU BRAND THEM).
Kijana ninakushauri kuwa angalia sana maisha yako kwa kuwa kila kitu katika maisha ukishaingia katika ndoa kitategemea sana wewe na mke wako usonge mbele au uingie katika ditch. Wasikilize wazazi na hao ndugu ila maisha ni ya kwako. Ukiona huyo mwanamke ndiyo uliyopewa na Mungu basi kaa na ndugu zako waeleze waziwazi.

Kwa kuhitimisha ngoja nikupe historia moja fupi sana. Yuko kijana mmoja alimpenda mwanamke aliyemzidi umri miaka kama 12 hivi. Wazazi na ndugu wa kijana wakaja juu sana na kumpa kila maneno machafu yule binti. Na kijana alikomaa na akamwambia wazi kuwa hutakiwi ila mimi ninakutaka. Wakaoana kwa taabu sana na Mungu alivyo mwema uzao wa kwanza mapacha, wakaamua wazae tena chapuchapu hivyo ndani ya miaka michache walizaa watoto wanne . Ninavyokueleza yule kijana na mke wake ni billionaires na yule mwananke aligeuka lulu kwa wale wazazi. Nilichompendea hakuna na kinyongo wala kisasi kwa ile familia ila aliwapenda tu. Leo hii ni wanamiliki construction company na mijengo ya maana na biashara kibao. Yaani are well off people. Sasa hapa kama kijana hakukomaa yangetokea hayo? Cha msingi mshirikishe Mungu na jisikilizie wewe na sisi wa pembeni tutakupoteza tu usipokuwa makini.

Kila la heri.
 
Pole sana ..akili kichwani mwako..
Kuna mtu ninayemfahamu alikataliwa kuoa mwanamke kama uyo kisa ana mtoto ,jamaa akasikiliza maneno ya familia akasahau ile familia haiendi kuishi na yule mwanamke yeye ndo ataishi nae...jamaa akaachana na yule mwanamke ..akaa kwa mieezi sita hivi akaja kutambulisha msicha mmoja hivi kuwa anataka amuoe huyo hapo wazazi wakafurahia kweli kweli nakumwambia huyu sawa ,hatua zote za utambulisho+ndoa zikafanyika na baraka za wazazi juu lakini kuna kitu kimoja walikikosa katika maisha yao ni MTOTO huu mwaka wa 11 sasa wamehangaika kila mahali lakini hawajafanikiwa.

kwahiyo kazi kwako akili ya kuambiwa changanya na ya kwako
Asante sana. Umenena bora mno kabisa. Mtu unabeza mtoto na mama yake halafu utegemee kupata mtoto? Wakati mwingine tunafuata ushauri ambao ni majanga tu mbeleni. Hata yale masononeko ya yule mama aliyekataliwa yanaweza kuwa laana pia.
Kuna mama mmoja alikuwa anasema kuwa eti mtoto wa kike kuachika ni malezi mabovu, akaseme eti wale wazazi watoto wao wameokoka au kubadili dini hawana malezi. Ha ha ha ha kwake kuna walokole, waliobadili dini na walioachika n.k na aliwashuhudia kabla wa kufa.
 
Huu ni upuuuzi first class.

Mtu kuwa mama yako haina maana anakumiliki, na wewe kuzaa mtoto haina maana unammiliki.

Huu uzwazwa wa watanganyika kudhani wanawamiliki watoto wao ndo unaokwambisha maisha ya wengine, kila mtu ana utashi na chaguzi zake.

Kwahiyo Mama yako akisema kuwa shoga unakua sababu tu kasema? Akisema usioe maisha yako yote huoi sabbau Mama kasema? Ukomo wa kukuamulia mambo yako ni upi? Ndo nyie ambao mnaoa ila kila kitu ni Hadi Mama aseme.

Hakuna cha laana wala nini kama mama sio muelewa. Hilo ni tatizo lake. Na ndoa ni zaidi ya kulalana
Akili yako kubwa sana mkuu. Keep it up. Eti mama kasema, eti baba kasema, eti dada zangu, eti sijui shangazi. To hell with them. Hao baada ya kufikisha 30 years (kwa waafrika wengi) hutawategemea kamwe. Hapo utakuwa unasomesha na mambo kibao ya maisha yako na mkeo tu. Yaani kabla ya kupelekeshwa ni vizuri mtu kukaa chini na kutafakari sana.
 
Back
Top Bottom