Kuoa Single Mama ni sawa na kunywa soda iliyofunguliwa na kuonjwa
Kuna single mother Mmoja nilikuwa niponae kwenye mahausiano ya mapenzi Mimi nilikuwanae kwaajir ya kuzuga tu Yani demu wangu akisafiri namtafuta yeye single mother huyo. Sasa kuna siku tuna piga Stori nikamuuliza nionyeshe picha ya Baba mtoto wake nimuone tu akakubali akachukua simu akanionyesha picha yake nilivyo muona nikijana tu tunalingana lika moja. Sasa baada ya miez 8 kupita akanitumia SMS Baba mtoto wake kafariki Mimi nikampa pole kwenye status akaweka picha za mwanae na video fupi fupi za kupokea mwili wa Baba mtoto wake na siku za ya kuzika video akaweka Sasa Jambo nililokuja kugundua Baba mtoto wake ni mtu mzima umri analingana na Baba yangu 68 na huyo Baba mtoto alishakuwa mwakilishi wa wananchi mjengoni na mjumbe wa Halmashauri ya mkoa kichama!! Kumbe picha ya mwanzo ya Baba mtoto wake aliyo nionyesha ambaye tuna umri Sawa siyo Baba wa mtoto inaonekana kabambikiwa mtoto na inavyo onekana jamaa kashajua mtoto siyo wake na kamkataa hatoi Huduma, kwaiyo single mother alizaa na mume wa mtu na mtu mzima kwa tamaa ya pesa kwaiyo vijana wakiume tuwe makini tunapo kuwa kwenye mahsiano na wapenzi wetu wasichana wengi wasasa Wana kuwa na mahusiano na waume za watu kwa Siri kwaiyo akipata mimba ya mtu mzima Mzee anakubambikia kijana mwenzake, Msichana wa umri wa miaka 24 Una zaa na mzee wa miaka 68 tena mume wa mtu kisa pesa kwanini usiwe single mother.
Duh! Single mother wanapewa vitasa tu leo...
 
Kuna baadhi ua wanawake hawajielewi tuh!hiyo inakuwa system yao ya maisha ya kuja kuwa single mother!
Wengi wao hawa jielewi Una zaa na mzee mwenye familia yake Sawa na mzaz tena nje ya ndoa wakitegemea watapata matunzo na urithi wa Mali kupende nitofauti mwishoe wana bakia kukimbiwa na kutelekezewa mtoto mzee wa miaka 68 ana mzalisha binti wa 24 kwa akili ya kawaida Mzee kama huyo lazma atakuwa na watoto wengi ndan ya ndoa na nje ya ndoa na hawezi kupata muda wa kutoa Huduma kwa watoto wote wa nje ya ndoa
 
#Jokajeusi kwann unaalazimisha kutuaminisha single mother wanakua na mahusiano ama ukaribu ama any connection na mwanaume walio zaa nao!!!?? Mbona huku mtaani haiko hivyo Kila mara...mbana wako ambao tena majority hawana maelewano mazuri na watu waliozaa nao tena wengine hata kupotezana kabisa. Wengi wanaume hawahudumii watoto wao wala hao wanawake waliozaa nao, wengi hawana mpango wa ukaribu wowote binafsi zaidi labda kwa ajiri ya mtoto tena hii itokee huyo mwanaume anajali mwanae, wengi ya hawa wanaume wakiona mzazi mwenzie kapata mwanaume basi hukata kamba mazima na kumuachia huyu mwanaume majukumu ya kulea.

Habari ya kutaka watu wasioe single mother ni kuonyesha weakness kama mwanaume, huo sio uwanaume... single mother ni binadamu kama binadamu mwingine, usitake kuwa label hawa watu eti wako hivi sijie vile NO! Don't do that mkuu... Single mother kama binadamu na wao wako na hulka tofauti na wanakosea kama binadamu wengine kama imetokea uliekua nae kakutenda basi usitake kuwaandama wengine...
 
Kwani kupigana mashine lazima . Unaweza ugulia tu na kuwa serious na mahusino upate wa kupeana nae mzigo kiuhalali kukwepa mimba haramu.
Mkuu hapo kwenye kuwa serious ndiyo tatizo, vidume tunajua sana kuigiza u-serious na tunawaingiza chaka watoto wa watu.
 
Tusiwalaumu single mothers. Hawakujitia mimba wenyewe.

Slogan yetu iwe 'USIZAE NA MWANAMKE USIYE NA FUTURE NAYE'.

Kama huna lengo la kuishi naye baadaye, usimtie mimba. Kwa sababu hakuna mwanaume atakayekuwa tayari kuoa mwanamke aliyezalishwa.

Tukishajizatiti katika hilo, hata single mothers hawatokuwepo. Kwa sababu tutawazalisha wale ambao tunajua tutadumu nao.

Kwako Studio.
Na vipi kwa wale wanawake ambao huwa wanaomba wenyewe kuzalishwa ili hali mwanaume huna mapango naye?,Vipi kwa wanawake ambao huwa wanategeshea ili uwatie mimba ili hali anajua fika kuwa huna mpango naye?.Haya mambo wee acha tu.
 
Kheri ya Mwaka Mpya

Vijana ambao hamjaoa, Kaka yenu Jokajeusi anasema msioe single-mother hata Kama mmeshikiwa bunduki.

Singel mother hasa waliozaliwa miaka kuanzia ya 90 mpaka sasa hao achaneni nao kabisa. Mkiwaona wapeini moyo, wasapotini kwenye vibiashara vyao na kazi zao ili wapate walau pesa za kujifariji, Ila kamwe msithubutu kuwaoa. Ni shimo refu Sana lenye Giza ambalo kutoka humo ni ngumu.

Ukifikiria kuoa single mother sharti ufikirie Yafuatayo;

1. Mzazi mwenza
Je uutamudu mawasiliano Yao.
Je upo tayari kukubali uwepo wa mzazi mwenza kwenye ndoa yenu?
Je upo tayari kusikia pesa hii imetoka Kwa mzazi mwenza wa Mkeo?

2. Kumtunza Mtoto uliyemkuta
Je upo tayari kumtunza Mtoto asiyewako?
Kama hauko tayari unafikiri Mkeo atafurahi mtoto wako awe anasoma shule nzuri, anavaa vizuri wakati Mtoto wake Kwa mzazi mwenzake (mume mwenza) hapendezi na anasoma shule Mbaya.

Au je utavumilia mtoto wako huwezi kumhudumia anasoma shule Mbaya na anavaa marapurapu alafu wakati huo mtoto wa mume mwenza akiwa anapendeza ndani ya nyumba yako?


3. URITHI
Je unafikiri ukifa Mkeo atakubali mtoto wake aliyempata nje ya ndoa akose Mali Kwa kisingizio chochote kile?

Ikiwa tuu wanawake wanang'ang'ania Mali ambazo wamezikuta Kwa waume zao wakidai wapewe nusu Kwa nusu unafikiri watakubali?
Kama unafikiri hivyo jua wewe bado mtoto Sana kuwafahamu Wanawake.

Wanawake ni wabinafsi kuliko kiumbe yeyote hapa ulimwenguni.
Mwanamke kitu pekee anachoweza kukipenda Kwa moyo wote ni mtoto/watoto aliowazaa MWENYEWE.lakini kamwe hawajawahi kumpenda mwanaume Kwa moyo wao wote.

Wanawake watakupenda Kwa matarajio Fulani, labda kama anaona kuna future zuri mbele yenu basi atakupenda Kwa future hiyo ndio maana wanaume mnashauriwa kuwadanganya wanawake kuwa mambo yatakuwa mazuri wasijali.

Mwanamke hawezi kukupenda kamwe Kama akigundua matarajio yake ya maisha mazuri hayapo. Labda awe mama Yako mzazi.

Msioe single-mother ni hatari Kwa maisha yenu.

Ujanani utateswa na wasiwasi WA mzazi mwenza kisha uzeeni utateswa na karaha za watoto wa kambo hasa wa Zama hizi.

Kikawaida wanawake wengi hupewa mimba na wanaume waliowapenda au wenye hadhi waitakao na kukubali kuolewa na watu wasiowapenda na wenye hadhi ya chini Kabisa.

Kabla hujamuoa single-mother jiulize Kwa jinsi alivyo Kama angekuwa Hana mtoto angekukubalia umuoe?
Au anakubali ili uokoe jahazi?

Wenye mapovu nimeshawazoea
Licha ya ukweli katika andiko lako lakini nimefurahi zaidi jinsi ulivyochambua mada kwa hoja. Uandishi wa kujenga hoja iwe positive au negative ni mzuri kuliko ule wa kuunga au kupinga jambo kishabiki.
 
Tusiwalaumu single mothers. Hawakujitia mimba wenyewe.

Slogan yetu iwe 'USIZAE NA MWANAMKE USIYE NA FUTURE NAYE'.

Kama huna lengo la kuishi naye baadaye, usimtie mimba. Kwa sababu hakuna mwanaume atakayekuwa tayari kuoa mwanamke aliyezalishwa.

Tukishajizatiti katika hilo, hata single mothers hawatokuwepo. Kwa sababu tutawazalisha wale ambao tunajua tutadumu nao.

Kwako Studio.
Unachozungumzia wewe ni siasa na hilo ndio kosa kubwa wanaume hasa wa mijini wanafanya kwa kuingiza siasa katika masuala ya ndoa . Unapotaka kuoa unatafuta mwanamke mwenye sifa za kuwa mke basi hayo mengine ya kulaumu kuwa wanaume ndio chanzo hayakuhusu.
 
Hizo ni sababu zako wewe,nitaoa single mother mke wa kwanza,nitaoa single mother kama mke wa pili hadi wafike wanne.
Single mother wengi wanajitambua kikubwa kama mwanaume timiza wajibu wako,kama ameachana na mwanaume wake jua kuna kitu kilikua hakipo sawa,na mpaka anakubali kuolewa na mwanaume mwingine basi kuna kitu ameona kipo sawa,
Nchi za wenzetu wanawake wanaolewa kwa mikataba,anaweza olewa na wanaume hadi kumi na kuachika.
Siku mzazi mwenzie akimpigia simu mkeo saa 7 usiku na upo kifuani akitaka kujua maendeleo ya mwanae anayesumbuliwa na homa ndo utawajua single mother wewe.
 
Back
Top Bottom