Kheri ya Mwaka Mpya
Vijana ambao hamjaoa, Kaka yenu Jokajeusi anasema msioe single-mother hata Kama mmeshikiwa bunduki.
Singel mother hasa waliozaliwa miaka kuanzia ya 90 mpaka sasa hao achaneni nao kabisa. Mkiwaona wapeini moyo, wasapotini kwenye vibiashara vyao na kazi zao ili wapate walau pesa za kujifariji, Ila kamwe msithubutu kuwaoa. Ni shimo refu Sana lenye Giza ambalo kutoka humo ni ngumu.
Ukifikiria kuoa single mother sharti ufikirie Yafuatayo;
1. Mzazi mwenza
Je uutamudu mawasiliano Yao.
Je upo tayari kukubali uwepo wa mzazi mwenza kwenye ndoa yenu?
Je upo tayari kusikia pesa hii imetoka Kwa mzazi mwenza wa Mkeo?
2. Kumtunza Mtoto uliyemkuta
Je upo tayari kumtunza Mtoto asiyewako?
Kama hauko tayari unafikiri Mkeo atafurahi mtoto wako awe anasoma shule nzuri, anavaa vizuri wakati Mtoto wake Kwa mzazi mwenzake (mume mwenza) hapendezi na anasoma shule Mbaya.
Au je utavumilia mtoto wako huwezi kumhudumia anasoma shule Mbaya na anavaa marapurapu alafu wakati huo mtoto wa mume mwenza akiwa anapendeza ndani ya nyumba yako?
3. URITHI
Je unafikiri ukifa Mkeo atakubali mtoto wake aliyempata nje ya ndoa akose Mali Kwa kisingizio chochote kile?
Ikiwa tuu wanawake wanang'ang'ania Mali ambazo wamezikuta Kwa waume zao wakidai wapewe nusu Kwa nusu unafikiri watakubali?
Kama unafikiri hivyo jua wewe bado mtoto Sana kuwafahamu Wanawake.
Wanawake ni wabinafsi kuliko kiumbe yeyote hapa ulimwenguni.
Mwanamke kitu pekee anachoweza kukipenda Kwa moyo wote ni mtoto/watoto aliowazaa MWENYEWE.lakini kamwe hawajawahi kumpenda mwanaume Kwa moyo wao wote.
Wanawake watakupenda Kwa matarajio Fulani, labda kama anaona kuna future zuri mbele yenu basi atakupenda Kwa future hiyo ndio maana wanaume mnashauriwa kuwadanganya wanawake kuwa mambo yatakuwa mazuri wasijali.
Mwanamke hawezi kukupenda kamwe Kama akigundua matarajio yake ya maisha mazuri hayapo. Labda awe mama Yako mzazi.
Msioe single-mother ni hatari Kwa maisha yenu.
Ujanani utateswa na wasiwasi WA mzazi mwenza kisha uzeeni utateswa na karaha za watoto wa kambo hasa wa Zama hizi.
Kikawaida wanawake wengi hupewa mimba na wanaume waliowapenda au wenye hadhi waitakao na kukubali kuolewa na watu wasiowapenda na wenye hadhi ya chini Kabisa.
Kabla hujamuoa single-mother jiulize Kwa jinsi alivyo Kama angekuwa Hana mtoto angekukubalia umuoe?
Au anakubali ili uokoe jahazi?
Wenye mapovu nimeshawazoea