Kuoa Single Mama ni sawa na kunywa soda iliyofunguliwa na kuonjwa
Kama wote mmemwamini Yesu Kristo na Kuokolewa mbona ndoa yenu inakuwa nzuri tu?
Ili mradi tu ndoa yenu iwe imekidhi Viwango vya Mungu!
Kama Single mother ana hofu ya Mungu hawezi kukusaliti eti kwa kurudia mahusiano yake upya na huyo aliye zaa naye.Unachotakiwa Mwanamme ni kujali mtoto wake maana HUWEZI KUMTENGA MAMA NA MWANA! ni Vigumu kabisa.
Otherwise Single moms wakiwa kwenye ndoa wanatulia kabisa kwa sababu ya mikiki waliyopitia kwa wale waliowazalisha na kuwatelekeza!
Amekuwa "single mother" kwa kutenda dhambi!
 
Kikao tulikubaliana hakuna kuoa singl mother kwa nn huyo kiruu kaoa
 
Hizi mada za Single Mother zilitulia naona sasa zimeanza tena upya, Single Mother ni binadamu kama binadamu wengine acheni kuwaandama ili hali chanzo cha Single Mother ni Wanaume.
Chanzo ni tamaa tu unakuta msichana hana shughuli ya uwakika yakumuingizia kipatato alafu ana zaa nje ya ndoa kwakuona mpenzi wake ana kaz nzuri au biashara kubwa akisha zaanae Ili apate uwakika wakupata pesa na kuolewa
 
Kheri ya Mwaka Mpya

Vijana ambao hamjaoa, Kaka yenu Jokajeusi anasema msioe single-mother hata Kama mmeshikiwa bunduki.

Singel mother hasa waliozaliwa miaka kuanzia ya 90 mpaka sasa hao achaneni nao kabisa. Mkiwaona wapeini moyo, wasapotini kwenye vibiashara vyao na kazi zao ili wapate walau pesa za kujifariji, Ila kamwe msithubutu kuwaoa. Ni shimo refu Sana lenye Giza ambalo kutoka humo ni ngumu.

Ukifikiria kuoa single mother sharti ufikirie Yafuatayo;

1. Mzazi mwenza
Je uutamudu mawasiliano Yao.
Je upo tayari kukubali uwepo wa mzazi mwenza kwenye ndoa yenu?
Je upo tayari kusikia pesa hii imetoka Kwa mzazi mwenza wa Mkeo?

2. Kumtunza Mtoto uliyemkuta
Je upo tayari kumtunza Mtoto asiyewako?
Kama hauko tayari unafikiri Mkeo atafurahi mtoto wako awe anasoma shule nzuri, anavaa vizuri wakati Mtoto wake Kwa mzazi mwenzake (mume mwenza) hapendezi na anasoma shule Mbaya.

Au je utavumilia mtoto wako huwezi kumhudumia anasoma shule Mbaya na anavaa marapurapu alafu wakati huo mtoto wa mume mwenza akiwa anapendeza ndani ya nyumba yako?


3. URITHI
Je unafikiri ukifa Mkeo atakubali mtoto wake aliyempata nje ya ndoa akose Mali Kwa kisingizio chochote kile?

Ikiwa tuu wanawake wanang'ang'ania Mali ambazo wamezikuta Kwa waume zao wakidai wapewe nusu Kwa nusu unafikiri watakubali?
Kama unafikiri hivyo jua wewe bado mtoto Sana kuwafahamu Wanawake.

Wanawake ni wabinafsi kuliko kiumbe yeyote hapa ulimwenguni.
Mwanamke kitu pekee anachoweza kukipenda Kwa moyo wote ni mtoto/watoto aliowazaa MWENYEWE.lakini kamwe hawajawahi kumpenda mwanaume Kwa moyo wao wote.

Wanawake watakupenda Kwa matarajio Fulani, labda kama anaona kuna future zuri mbele yenu basi atakupenda Kwa future hiyo ndio maana wanaume mnashauriwa kuwadanganya wanawake kuwa mambo yatakuwa mazuri wasijali.

Mwanamke hawezi kukupenda kamwe Kama akigundua matarajio yake ya maisha mazuri hayapo. Labda awe mama Yako mzazi.

Msioe single-mother ni hatari Kwa maisha yenu.

Ujanani utateswa na wasiwasi WA mzazi mwenza kisha uzeeni utateswa na karaha za watoto wa kambo hasa wa Zama hizi.

Kikawaida wanawake wengi hupewa mimba na wanaume waliowapenda au wenye hadhi waitakao na kukubali kuolewa na watu wasiowapenda na wenye hadhi ya chini Kabisa.

Kabla hujamuoa single-mother jiulize Kwa jinsi alivyo Kama angekuwa Hana mtoto angekukubalia umuoe?
Au anakubali ili uokoe jahazi?

Wenye mapovu nimeshawazoea
Vijana wengi Wanakurupukq Sana Kwenye Kuoa.
 
Siyo wote walio oa single mothers wanapitia hizo changamoto bhana! Wapo wadau wengine wanafaidi kweli kweli mapenzi ya hao single mothers, huku wakiwa hawana mgogoro wowote ule kwenye ndoa/mahusiano yao.

Hivyo mimi nashauri vijana waoe wanawake wa maisha yao. Utakuwa ni ufala mkubwa sana kuacha kuoa single mother ambaye ni wife material, halafu badala yake ukaenda kumuoa Asha Ngedere ambaye muda wote kyupi iko mkononi! Kisa tu hana mtoto.
We maisha Hujayajua. Toka Lini Mtu akaja Kukusimulia Tabu anazopata. Hao unaosema wanapata Raha na Single mother labda Huyo single mother Bado ana mtoto mdogo ngojawa Wakue vizuri utajua Hujui
 
Mimi sijaongelea bahati mbaya mkuu.

Ila nimeongelea namna single mum wanapigwa vita na kuonekana ni Aina ya wanawake wasiotakiwa kuolewa.

Bahati mbaya au bahati nzuri inategemea sababu iliyosababisha hao single mom wawepo, kuna waliofiwa na waume zao wakawa single mom.

Kuna walioolewa wakaachika wakawa single mom.

Kuna waliobakwa wanakapata ujauzito wakawa single mom.

Kuna hao wa kujitakia pia.

Wote ni single moms.

Ila sasa wasijione wanyonge sana, watoto ni baraka, mimi naamini kwa wanawake waliozaa wanajua mahusiano yalivyo.

Hivyo kuliko kuhangaika na wanaume ambao daily kuwasema ni heri muda huo watumie kulea watoto wao, kujiendeleza kiuchumi , elimu na ujuzi mbalimbali.

Then kwa wakati sahihi Mungu atawaletea watu sahihi.
Ukibakwa unahalali ya kuitoa!!!!!! Hiyo inaruhusiwa acha kutetea upuuzi
 
Tangu Jana na Leo naona mada za single mother humu...halafu some guys wamewaandama hatari.
Sikieni wadau kama unajiona huwezi kuoa single mother we tulia lakin sio kuja kukatisha tamaa wenzio au kulalamika humu ndani kwa vitu ambavyo single mother wengine wafanye Kisha useme wote.

Kuna akina single mother ambao ni werevu, wanye upendo, waaminifu, waliojitolea na kuishi maisha na ya upendo na kumthamini mume ambae sio aliezaa nae and are trying their best to live a full life na hao step-dad. Pia wana confident with their bodies na wako deep into their hearts because they went through a personal growth na experience flan ya maisha katika mahusiano. Sio kama atadai lazima kwanza uhudumie mtoto wake ndo akupende; single mothers anaejielewa won't ask you to jump into fatherhood immediately kwasabab kumbuka kwamba yeye ni zaidi ya mama, yeye ni mlezi, muhudumiaje na mpiganaji kwa mwanae. So anahitaji mwenzi wakua nae katika maishani yake, sio tu baba wakuhudumia mtoto wake.

Usifikiri pesa ama kumpenda mwanae tu ni kitu anachotaka kutoka kwako basi usipo fanya hivyo basi atarudi kwa mzazi mwenzie ama eti atakua na mahusiano ya kimapenzi na baba wa mtoto wake, ama sijui vitu vya ajabu ajabu mnasema, no!, that's not true kwa Kila single mother.

Sikia single mother anahitaji mapenzi, your time na support kutoka kwako kama kweli unampenda. Kwangu mimi ikiwa ninampenda, ninamaanisha hivyo na nitawajibika kwa maamuzi yangu ya kuwa nae yeye na mtoto aliye nae pia. Nani anajua, ninaweza kumuoa na ku adopt mtoto/watoto wake hatimaye. Ndio, itakuwa ngumu haswa ikiwa biological father bado yuko kwenye picha ndani ya simu yake lakin najua inahitaji very strong man kukubali watoto wa mwanaume mwingine ambae haswa yupo hai but kwa upendo wangu kwake ata realize kama sasa amepata mtu wa tulizo ya moyo wake na atatulia tu mbona.
 
Hapo umejisemeaa ww na moyo wako mkuu,mm km mm single mother no nshapenda single mother km watatu wt n nyokoo tu ,kiufupi n HV ukimpenda single mother hakikisha umeliona kaburi la bb wa mtt wake hata kwenye picha utaona hata jina kwenye msalaba la huyo jamaa ,vinginevyo na hapo hawaachanagii
 
Siku hizi tunaoa kusogeza siku tu na kusaidiana mambo madogo madogo.
Huwezi kuwa na mpenzi wako mwenyewe peke yako.
 
Hua najiuliza, what if aina ya huyo single mother was everything I wanted? What if she was thoughtful, intelligent, driven, attractive and successful on her on?. Je, vip kama ana dreams and goals ya mahusiano ambayo na Mimi nipo nayo? What if she educated enough kuweza kujimudu maisha yake na hisia zake? Is she Knowledgable? Does she make me laugh and happy? Do our end goals align? If so… then yeah. I’d probably date her na kisha tutaoana na kuishi maisha ya furaha na karaha lakin yenye upendo ndani yake na kumpenda mwanae as my own child. I’d consider her important enough to accept that she comes with small sentient child-shaped responsibilities.
 
Back
Top Bottom