Hayashangazi haya! Ikiwa "mtu" alitumwa India kutibiwa na watu hawakushangaa iweje hili la mtu kujiuzulu ikasemwa kafukuzwa pasina kikao!!!???
 
Kiukweli haingii akilini pale spika anapokuwa hayupo na kisha bunge kuendeshwa na yule mwanadada halafu wabunge wanasema huyu mwanamama hafai anawaminya na kisha kumtaka huyu mzee kifimbo cheza kuongoza!
Huyu mzee kifimbo alipokuwa ughaibuni kwa matibabu wabunge walikuwa wakichukizwa sana jinsi ambavyo huyu mwanamama alivyokuwa akiongoza, hivyo wakawa wanamuombea sana kifimbocheza apone ili aongoze!
Baada ya kifimbo kupona, yaliyotokea yamekuwa tofauti sana...
Kwa kweli hii haikubaliki wapinzani kuendelea kuwasifia hawa watu kwa matendo wanayofanyiwa...
Pia hata wabunge wa chama tawala wanaojali na kutambua demokrasia ya kweli huu ni wakati wa kuungana na wale wote wenye mapenzi mema kuinusuru demokrasia yetu!
Hawa watu wawili wanapaswa kujirekebisha, ama kuondolewa kwenye viti vyao!
 
Suluhu ni kuondolewa.

Je, nani atawaondoa?
 
Spika atakuwaje upande wenu wakati waliompa uSpika ni Wabunge wa CCM
 

Kwa nafasi ya USPIKA na UNAIBU SPIKA au uenyekiti wa Bunge ukishakaa kwenye kile kiti unatakiwa kuwa very neutral na kama huwezi jiweke 75% neutral maana ukishakuwa Bungeni hatuangalii chama kule ni watanzania wanakaa kuifunga kengele serikali.

Hivyo Spika anaongoza wananachi na si serikali.Bunge si la serikali bali la wananchi bila kujali itikadi zetu.Ujinga wa kufanya upendelea matokeao yake ni kutokuenedelea kwa taifa
 
Katiba za ki Africa ktk swala la democracy ni pasua kichwa!! Na kwa Tz ni dhambi kushirikiana mtu wa chama cha upinzani. Ila inatakiwa wa upinzani yeye ashirikiane na chama tawala ajabu!!!

Ndugai analifanya bunge jumuia ya chama. Katiba zetu mbovu.
 
Kwa mfululizo wa mambo na matukio anayoyafanya mheshimiwa sana ya kujichukulia madaraka na kujigeuza yeye ndio kila kitu,nina hakika ingekuwa ni katika nchi za wenzetu wabunge wangeshachachamaa na pengine kuanza mchakato wa kikatiba kumshughulikia.

Kwa mfano,ingekuwa ni hapo Bondeni kwa mzee Madiba saa hizi pangekuwa hapatoshi na kina Julius Malema wangekuwa wameshamtolea uvivu ila hapa kwetu tumelala usingizi na yeye ana-take advantage ya uzembe wetu.

Binafsi ningekuwa mule ndani ningeshalianzisha ingawa najua ningekamwisha lakini nisingejali kwani lengo ni ujumbe ufike na umma uelewe.
 
Binadam ni viumbe wa ajabu sana.
Mwaka jana wakati Spika alipokuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu na nafasi yake kuchukuliwa na naibu spika, kulikuwa na malalamiko mengi sana dhidi ya N/S na wengi walikuwa wanasema ni bora mwenye kiti chake arejee mapemba maana huyo aliyekuwepo alikuwa hatoshi.
Leo hii mnaanza kusema kuwa huyo ambaye mlikuwa mnamsifia sasa naye amekuwa hafai.
 
Hii kauli ilimkasirisha sizonje, ndio maana siku ya kupokea ripoti ya madini ya tanzanite, aliamua kumpasukia live spika kwa kuwa aliona kama anawalea lea wapinzani, akamwambia wakilopoka, i mean wakipishana kwa kauli awatoe nje na jamaa anatekeleza tu bila aibu!:,(
 
Nahisi Ndugu Ndugai Bado anapwaya sana katika nafasi yake ya uspika, ni mwaka wa tatu sasa hatujaona hata meno ya Bunge kuiwajibisha serikali katika masuala nyeti na Muhimu,

Nakumbuka kipindi cha jamaa Kikwete Bunge limewajibisha serikali Mara kibao sana na nashangaa mpaka Leo tuna mengi ya kuhoji lakin Bunge linaiogopa serikali,

Kuna masuala nyeti sana lakin Bunge Lipo kimya,

Naona viatu vya Makinda vinampwaya ndugai,

Hata wakati wa mwalimu Nyerere ambaye tunaamini ndo alikuwa mkali na ndo alikuwa rais kweli, lakin Bunge lilihoji na kuisimamia serikali ipasavyo mpaka saa nyingine kuikataa miswada na Nyerere ku surrender

Kipindi hicho Adam Sapi Mkwawa akiwa spika bunge lake lilikataa muswada wa Rais na kuurudisha na Rais akabwaga manyanga. Tena siyo hawa marais wa kuja bali ni Rais anayeheshimiwa hata miaka 200 ijayo yaani Rais Julius Nyerere. Je, ilikuwaje? Ilikuwa hivi.

Mwaka 1969 Waziri wa Elimu, Solomon Eliufoo aliugua na ikaonekana anaweza asiendelee kuwepo serikalini. Serikali kwa ku-panic ikapeleka muswada bungeni unaohusiana na mafao au maslahi ya mawaziri hasa wanaougua.

Muswada huo ulileta mgawanyiko bungeni ukizingatia kwamba ni miaka miwili tu tangu siasa ya Ujamaa na Kujitegemea itangazwe pia miiko ya uongozi.

Bunge likaukataa muswada ule likamrudishia Rais Nyerere ili ikiibidi afanye lolote na kama ni kuurudisha tena basi na iwe ili hatimaye wavunje bunge na nchi irudi kwenye uchaguzi.

Rais Nyerere mwenyewe alipohojiwa na waandishi alinywea na kusema "the parliament had a point" yaani bunge lilikuwa na hoja na hakuthubutu kuupeleka tena bungeni.

Haya, niambieni ni bunge lipi tena lililowahi kufauluujasiri kama huu. Wote waliobaki na mnaowataja wafyata mkia watupu, tena kukiwa na hatauwezekano wa kuhama vyama.

Leo hii Viatu vya Makinda ni vikubwa mno kwa ndugai
 
tatizo viongoza wetu wanatamba na gpa za 32 walizopata sua ya dom

ben.big.boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…