Wanabodi,
Salaam;
Nimesikitishwa sana na kitendo kilichofanywa na ofisi ya spika juu ya kujiuzulu mh. Nyalandu.
Ni wazi ofisi ya Bunge imejidhalilisha mno!
Baada ya taarifa ya Nyalandu kuenea ktk mitandao ya kijamii na ktk vyombo vya habari, alijitokeza msemaji wa CCM asiye na uwezo wa nafasi yake, akimshangaa Nyalandu kukihama chama cha mapinduzi chenye itikadi ya ujamaa na kuhamia ktk chama kisichokuwa na Sera. Huyo aliyeyasema hayo ni kiongozi wa ngazi ya juu kabisa ya CCM.
Kwa taarifa tu na kwa faida ya wengine wasiofahamu, katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi, anaingia katika vikao vyote vikuu vya kikatiba kuliko hata mwenyekiti wa CCM taifa. Mwenyekiti siyo mjumbe wa sekretarieti ya chama ambayo inaundwa na watendaji tu. Yaani katibu mkuu(ambae ni mwenyekiti wa kikao), manaibu katibu wakuu, katibu wa itikadi na uenezi, katibu wa uchumi na fedha, makatibu wa jumuiya za chama yaani UWT, vijana na wazazi.
Hicho kikao ndo kinaandaa ajenda za kikao cha kamati kuu na huyo Polepole ni mjumbe pia wa kamati kuu. Kama Nyalandu alifukuzwa, ina maana Polepole angekuwa anajua na kwa sababu ni mropokaji, lazima angekuwa ameropoka tu!
Kwa hiki kilichofanywa na ofisi ya spika ni kitendo cha aibu mno na kama kitavumiliwa na wabunge, tutaonana 2020 msitufanye watanzania wote majuha..!