Unatoka nyumbani kwako unaenda dukani kwa Mangi unaachagua soda iliyofunguliwa na kunywewa kisha ikasazwa? Hivi huoni kinyaa? Soda zilizo na vizibo mbona zimejaa dukani kwa Mangi? Una tatizo gani hadi unaamua kula makombo?
Single mama hana moyo wa kupenda tena. Hapo amekufanya wewe mwanaume kuwa mti wa kivuli cha shida zake za hisia, kiuchumi, kijamii, n.k. Wahenga wanasema "moyo wa mapenzi ni kama glasi, ukipasuka ufa wake hauzibiki". Maana yake kupenda hakujirudii mara mbili, hasa hasa mwanamke akisha zalishwa...ni kana kwamba moyo wa kupenda unatoka pamoja na mtoto kule leba.
Wewe mwanaume uliyekamilika na unajiamini unaanzaje kumuoa single mama?? Ona kinyaa ndugu yangu. Single mama alishapenda tayari na ndiyo maana akaamua kumpa yule mzazi mwenzie mpk akapata ujauzito. Si ajabu alimkuta bikra jamaa akaitoa, kisha akarudia na kurudia na kaurudia hadi mimba. Leo wewe mkolomije unaenda kuoa. Acha uzembe kwenye mapenzi.
Tafiti zinaonyesha kwamba mwanaume wanao oa masingle mama-- wako katika mojawapo ya makundi yafuatayo;-
--hawajiamini
--wanafuata maslahi
--ni washamba washamba Fulani HV
--waliruka stage ktk makuzi yao
WITO; raha ya soda ukute haijaonjwa
Hiyo assumption yako ni ya kitoto na wala hujafanya utafiti wa kutosha kuhusu hili.
Kwanza nikuulize, jee hawa wanawake wameonjwa na kuzalisha na nani?
Jee matatizo mengi ya ndoa hivi sasa yanatokana na wanawake ambao in single mamas? Au wale ambao mnaona kuwa hawajaonjwa [kwa vile hawana watoto].
Suala la kuoa ni maamuzi ya wawili bila kujali mazingira ambayo wametokea.
Mfano mzuri ni mimi mwenyewe.
kwanza mimi ni mtoto wa dar [nadhani unaelewa maana yangu]
pili- nilichelewa sana kuoa[inawezekana kutokana na utundu mwingi ]
Nilioa miongo miwili sasa na mwanamke niliyomuoa aliwahi kuolewa na alikuwa na watoto.
Wakati ninafanya maamuzi ya kuoa, wale wote walionitakia mema walipinga sana.
Kuna wengine walidiriki hata kunitafutia warembo hasa[simba anapenda kuwinda mwenyewe]
Ukweli nilitekeleza azma yangu nikaoa na baadaye wale watoto wakataka waje kuishi na mama yao[sikuwa na kizuizi]. Niliwalea watoto wale na wote wamemaliza chuo kikuu kuna wengine wameshaolewa.
Mke wangu, wangu amekuwa msuluhishi wa ndoa nyingi za rafiki zangu na katika kipindi chote hiki sijajuta uamuzi wangu wa kumuoa.
Kuna wakati mwingine huwa ninatania kuwa hata tukifa na huko kuzimu kama nitaulizwa nataka mke wa aina gani, bado nitamchagua huyu niliyo naye.