Kuoa Single Mama ni sawa na kunywa soda iliyofunguliwa na kuonjwa
Kuna single mother ni vyuma haswa,kuna mmoja wa kirangi alikuwaga mwembmba akamvaa mume wa mtu kamzalisha akamwacha. Sasa baada ya kujifungua nyonga imetanuka bonge la shape.

Akawa anauza juice,sasa hapo hao wateja wake wa juice wakawa wanajipigia bahati nzuri katokea mwana anaduka la nguo akaamua kujibebea mzigo.
 
Kiukweli hakuna ubaya kumchumbia single mother na kumuoa huyo mama asiye na mwenzi. Hata kama amezaa, mtoto aliyemzaa na mwanaume mwingine ni baraka kabisa.

Cha muhimu ni kwamba nyote wawili mnapendana na mmejitolea kufanya uhusiano wenu ufanye kazi. Hivyo ukimpata single mother na mkapendana nyote muoe tafadhari hata kama ana watoto watatu oa tu.

Mtume Muhammad ni mfano wa kuigwa hakumuogopa bi Khadija. Jifunzeni kwa huyu mtumishi.

Enyi wanaume waoga acheni ushamba.
jidanganye tu
 
Kiukweli hakuna ubaya kumchumbia single mother na kumuoa huyo mama asiye na mwenzi. Hata kama amezaa, mtoto aliyemzaa na mwanaume mwingine ni baraka kabisa.

Cha muhimu ni kwamba nyote wawili mnapendana na mmejitolea kufanya uhusiano wenu ufanye kazi. Hivyo ukimpata single mother na mkapendana nyote muoe tafadhari hata kama ana watoto watatu oa tu.

Mtume Muhammad ni mfano wa kuigwa hakumuogopa bi Khadija. Jifunzeni kwa huyu mtumishi.

Enyi wanaume waoga acheni ushamba.
Heti bora ya mume wangu alie kufa kuliko wewe ukimkwaza hiyo ndio kauli yake
 
UKIOA SINGLE MOTHER HAKIKISHA MWANAUME ALIYEMZALISHA UMEMZIDI MAMBO HAYA!

Anaandika, Robert Heriel

Usije ukajichanganya, wala asije akakudanganya mtu yeyote. Single mother sio good match kwenye mahusiano hasa Kwa kijana mdogo mwenye umri Chini ya miaka 40.
Single mother wanahitaji mwanaume aliyekomaa kama Simba Bob Junior.

Elewa kuwa asilimia 90 ya single mother wanamajeraha makubwa na maumivu ya mapenzi, na tayari wanaathari za kisaikolojia katika mapenzi. Hivyo wengi ni wagonjwa wa kisaikolojia.
Hii ni kusema, Kabla hujamuoa single mother ni lazima uhakikishe unamtibu ugonjwa wake wa Kihisia Baada ya kuwa Disappointed na Mwanaume wa awali.
Sasa wewe jichanganye uone yupo Sawa Kwa vile anakuchekea, mnaongea vizuri, sio kweli, wengi ni wagonjwa.

Bila kupoteza muda, Kabla hujamuoa single mother hakikisha mwanaume aliyemzalisha umemzidi mambo yafuatayo;

1. Haiba, Mvuto na mwonekano.
Usije ukajichanganya hata siku Moja, Haiba na mwonekano wa mwanaume ni moja ya mambo ambayo Wanawake wote Duniani wanajivunia. Hakuna mwanamke asiyependa mwanaume asiye na Mvuto. Wasije wakakudanganya na unafiki wao.

Wanawake hawanaga ujanja Mbele ya wanaume wenye haiba, Mvuto na mwonekano mzuri. Tena huyo Mwanaume ATI ndio aliyemzalisha, hapo ndio kabisaa!

Ni lazima umzidi Mwanaume aliyemzalisha Haiba, Mvuto, na mwonekano.
Asije kukudanganya ati hawawasiliani, Huko ni kuzidiwa Akili na Mwanamke.
Elewa kuwa Single mother hata kama atakuwa anachuki vipi Kwa aliyemzalisha lakini kamwe hatoweza kujilaumu kuzaa na Mwanaume mwenye haiba, Mvuto na mwonekano.
Na sio ajabu akawa anajivunia Mbele ya ndugu, rafiki na watoto wake kuwa Mwanaume Fulani alistahili kuwa naye katika safari ya Maisha, hata kama haikuwa riziki kuoana.

Kingine, elewa kuwa ikiwa haujamzidi Aliyemzalisha Kwa haiba, Mvuto na mwonekano Kwa Mwanamke ataihesabu kama aibu kwake, na atakuona wewe sio hadhi yake, hivyo lazima akutese.
Yaani aache kuwasiliana na Mwanaume aliyekuzidi kisa wewe umemuoa😂😂 huwajui Wanawake wewe,

2. Umzidi kiuchumi na kifedha.
Wanawake hawajawahi kujuta kuzalishwa na wanaume wenye uchumi mkubwa na matajiri. Hata kama waachane na kugombana vipi. Bado Mwanamke atajivunia na kuona Sifa kuwa anamahusiano na Mzazi mwenza.
Uliona wapi Mwanamke akamsumbua mwanaume masikini aliyemzalisha? Uliona wapi?

Elewa kuwa Wanawake kwao ni ufahari kuchukua majina ya wanaume wenye sifa Fulani kubwa kama matajiri, Watu mashuhuri, Watawala n.k.
Elewa kuwa utakapomuoa mwanamke aliyezalishwa au aliyewahi kuachwa na Mwanaume mwenye uchumi mkubwa, kwake atataka kutambulika kwa jina la Yule mwanaume mwenye Pesa au tajiri kuliko wewe kapuku.

Kabla hajaoa single mother, jihakikishie kabisa mwanaume aliyemzalisha umemzidi kiuchumi, kifedha na kiutajiri.

Mwanamke hajawahi kuacha kitu Kizuri, fedha, na utajiri hata siku Moja.

Kitendo cha kuona Mwanamke uliyemuoa anawasiliana na Mwanaume aliyemzalisha Kwa kisingizio cha mzazi mwenza kitaalamu Sisi kina Taikon tutakuambia huyo Mwanaume anavigezo Fulani alivyokuzidi aidha ni Mzuri/handsome boy, anahaiba au mwonekano mzuri kukushinda au anafedha kukushinda.

Mwanamke akimpata Mwanaume wa hadhi anayoitaka yaani mzuri/handsome boy au mwenye kipato cha juu automatically ataleta dharau Kwa aliyemzalisha, yaani atataka ajitenge naye na kukata mawasiliano kabisa ili asijeharibu mahusiano yake yenye tija.

Single mother wanahitaji wanaume Heavy weight iwe kiuchumi au kimwonekano au kihadhi.

Na sio single mother tuu, hiyo ni kawaida na asili ya Wanawake wote Duniani.
Mwanamke hata ambaye hajazalishwa, ikiwa yupo sehemu nzuri na Mwanaume wa uchumi wa juu au mwenye mwonekano automatically huwadharau Watu wa hadhi ya Chini.

Ni kawaida mwanamke kwenda kushiriki kwenye matukio ya mwanaume aliyemzalisha kama matukio ya misiba, harusi n.k. ikiwa mwanaume huyo anauchumi mzuri.
Yeye naye atataka ajulikane naye aliwahi kuwa na umiliki Kwa huyo mwanaume.

Mwanamke haishii hapo, hata Watoto aliowazaa kwake ni Sifa kuitwa jina la tajiri au mwenye mamlaka ikiwa tuu alimzalisha.
Lakini wewe kapuku na usiye na Mbele wa Nyuma, sio ajabu Mwanamke hata jina la mtoto asiitwe ubin wako.

Nasisitiza, Mwanamke hajawahi kususa na kuacha kitu Kizuri na utajiri. Haipo hiyo.
Kama umezidiwa na aliyemzalisha Mwanamke uliyenaye alafu anakuambia hawasiliani naye. Jua anakudanganya.

Na hapo ndipo mnapoambiwa Wanawake wanawazidi Akili Kwa sababu ya kuamini maneno Yao kama wajinga wajinga.

Mwisho, Mwanamke anasikia aibu kuoelewa na wewe ikiwa aliyekuwa naye awali alikuwa amekuzidi Kwa mbali Mno.
Kudharauliwa katika mazingira hayo ni Constantly.

Sabato NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mkuu, as long as aliyemzalisha bado atakuwa yupo hai. hata umzidi vitu vyote vya hii dunia bado akitaka kukugongea, atagonga safi tu.

Mwanaume, kwamwe hutakiwi kuoa Mke wa mtu.

Hapana Mkuu.
Kama aliyemchukua kakuzidi wewe Kwa kila kitu iwe kifedha na kimwonekano nakuhakikishia hata umshawishi vipi hatoweza kukubali.
Kwanza ataona alipoteza mwelekeo, yaani atakuona kama mkosi na ulimbahatisha.

Wengine mpaka wanafikia hatua na watoto wanabadilisha majina yao, yaani wewe Watoto wako lakini hawaitwi ubin wako.

Ukiona umemshawishi mwanamke uliyezaa naye alafu ameolewa ukamlamba tena ujue huyo aliyemuoa hamtofautiani Sana. Yaani mpo level moja tuu. Au kama kakuzidi ni Kidogo Mno.

Hivyo ndivyo Wanawake wanavyofanya mishe zao.
 
Back
Top Bottom