SEHEMU YA KWANZA
[emoji1630] *KWANINI SINGLE MOTHERS WANAONGEZEKA DUNIANI?*
*BY MR. GODFREY EDWARD*
*Single Mothers* na mahusiano mengi kuvunjika mara kwa mara kwa maono mapana naona inasababishwa na tatizo moja kuu.
Watu wengi wanaingia kwenye *Mahusiano* na wenza ambao sio sahihi kwao.
Kitaalamu unaweza kusema *Mwanamke* anaanzisha mahusiano au anazaa mtoto na *Mwanaume* ambae sio *Soul Mate* wake.
*Soul Mate* kwa tafsiri ya kitaalamu ni mpenzi mmoja tu ambae utakuwa na hisia nae za ndani kabisa *(Deep love)* za kimwili na za kiroho *(Body and Soul connection)* na utampenda kwa moyo wako wote na kwa maisha yako yote *(Eternal love)* haijalishi mtu huyo atakuwa na hali gani ya kimaisha.
Naamini kwamba Kila binadamu aliumbwa kwa ajili ya kumpenda mtu mmoja tu.
Yani kila binadamu aliumbwa kuwa na Hisia za Mapenzi za kweli *(Deep love)* na mtu mmoja tu hapa duniani.
[emoji3519] Naamini pia Sababu kubwa inayosababisha Mahusiano mengi kutodumu au Ndoa nyingi hazidumu ni kwasababu watu wengi wapo kwenye mahusiano na watu ambao hawana hisia nao za dhati *(Deep love)*
ila wapo nao tu kwenye mahusiano kwasababu zingine ambazo hazihusiani na mapenzi ya dhati
yani sio *Soul Mates* wao.
[emoji3519] Wengi wapo kwenye mahusiano kwasababu ya,
[emoji3591] *Fedha.*
[emoji3591] *Umaarufu wa mtu husika.*
[emoji3591] *Cheo cha mtu husika.*
[emoji3591] *Muonekano wa mtu husika.*
Lakini sio kwasababu za mapenzi ya dhati kwa mtu husika *(No Deep Love).*
Kutokana na sababu hii kubwa ndio maana mahusiano mengi na ndoa nyingi zimekuwa hazidumu kwa muda mrefu.
[emoji3519] Mbaya zaidi kama *Mahusiano* yataanzishwa kwasababu ambazo *sio za mapenzi ya dhati (Not Deep love)*
Au kama utaingia kwenye mahusiano na mtu ambae haukupangwa kuwa nae *(Undestined Soul Mate)* na ukazaa nae mtoto.
Uwezekano wa kuachana ni mkubwa na hivyo *mwanamke* anaweza kubadilika kuwa *Single Mother* au kama malezi ya mtoto ataachiwa mwanaume basi na yeye atabadilika kuwa *Single Father.*
*Soul Mate* wa kweli kwa kila mtu duniani huwa ni mmoja tu na anaweza kuwa katika nchi yako au nchi nyingine.
[emoji3519] Mfano, *Soul mate* wako wa kweli anaweza kuwa ni *Mtanzania* au anaweza asiwe ni raia wa nchi yako.
Labda *Soul Mate* wako anaweza kuwa ni *Mjerumani, Mhindi, Chinnesse, American* au hata nchi nyingine ya *Afrika*.
[emoji3519] lakini haijalishi nchi anayotokea mwenza wako wa dhati uliepangiwa *(Destined Soul Mate)* huwa yupo mtu mmoja tu duniani ambae ndio aliumbwa kwa ajili yako.
[emoji3519] Kitaalamu wanasema kwamba kila binadamu atakuja kuyafurahia mapenzi ya dhati kwa asilimia kuanzia *90%* na kuendelea pale tu atakapofanikiwa kumpata *Mwanaume* alieumbwa kwa ajili yake au kumpata *Mwanamke* alieumbwa kwa ajili yake kitaalamu yani *Soul Mate.*
Huyu ndio mtu pekee ambae utakuwa umeunganishwa nae *kimwili* na *kiroho (Body and Soul Connection)* na sio rahisi kuja kutenganishwa nae kwasababu zozote za kidunia labda kifo tu ndio kiwatenganishe.
[emoji3519] Matatizo yanayoendelea kutokea kwenye jamii zetu yanayohusiana na mapenzi kama,
[emoji3591] *Mwanamke Kuzalishwa na kuachwa Single Mother*
[emoji3591] *Wapenzi kufumaniana.*
[emoji3591] *Wapenzi kuuwana kwa tamaa za mali au hasira za mapenzi.*
[emoji3591] *Wapenzi Kudharauliana kutokana na tofauti za kipato au vyeo.*
Na matatizo mengine mengi kama haya yanatokea kwasababu watu wengi wanaingiza kwenye mahusiano na watu ambao *sio Soul Mates* wao.
[emoji3519] Ukija kumpata *Soul Mate* wako hauwezi kuja,
[emoji3591] *Kumsaliti*
[emoji3591] *Kumpiga.*
[emoji3591] *Kumdharau.*
[emoji3591] *Kumuongelea vibaya asipokuwepo.*
[emoji3591] *Kumzalisha na kumuacha Single Mother.*
Na mambo mengine mabaya kama hayo kwasababu *Mapenzi ya kweli* yana nguvu sana.
[emoji3519] Ikitokea ukaja kumpata *Soul Mate* wako wa kweli hata kama ni,
[emoji3591] *Maskini.*
[emoji3591] *Sio maarufu.*
[emoji3591] *Hana mvuto Sana.*
[emoji3591] *Hana elimu kubwa.*
Bado utampenda vile vile kwasababu *Soul Mate* wako unaunganishwa nae *kiroho (Soul Connection)* na sio *kimwili* tu.
[emoji3519] Mtu ambae umempenda kwa dhati yani *Soul Mate* wako
Hakuna tatizo lolote duniani ambalo litaweza kukufanya upunguze mapenzi yako kwake.
[emoji302] Ukiona kuna mtu mwanzo ulikuwa na hisia nae alafu ghafla zile hisia kwake zikaanza kupungua au zikaisha kabisa basi fahamu huyo mtu hakuwa *Soul Mate* wako.
[emoji302] Ukiona mtu mwanzo alikuwa *Anakujali* na *Anakusikiliza* lakini ghafla amebadilika
anaanza kuwa *Mkali kwako, Anakupiga* na kukufanyia mambo mengine mabaya basi tambua mtu huyo hakuwa *Soul Mate* wako.
[emoji3519] Siku zote *Soul Mates* huwa na *Mapenzi ya dhati* tena kwa pande zote mbili ambayo ni sawa.
Yani *Mwanamke* na *Mwanaume* wote wanapendana sawa na kwa dhati *(Deep love and connection of two lovers equally).*
[emoji3519] *Mapenzi ya upande mmoja hayo sio mapenzi ya kweli.*
*Mapenzi* ambayo *Mwanamke* pekee yake ndio kampenda sana *Mwanaume* husika.
Au *Mwanaume* pekee yake ndio kampenda sana *Mwanamke* fulani hayo *sio mapenzi ya dhati (Not Deep love).*
*Deep love* huwa ni *Mapenzi ya watu wawili* tu yani *Mwanamke Mmoja* na *Mwanaume Mmoja* kupendana kwa dhati na hakuna tatizo au sababu yoyote inayoweza kuwatenganisha zaidi ya *Kifo* tu.
Na *Deep love* huwatokea wapenzi ambao ni *Soul Mates* tu.
Ingawa *Deep love* huwatokea *Soul Mates* tu lakini sio kitu rahisi sana kumpata yule ambae aliumbwa kwa ajili yako tu na wewe uliumbwa kwa ajili yake tu.
[emoji302] Lakini ukimpata *Soul Mate* wako wa kweli ndio mtu pekee ambae utafurahia nae mapenzi ya milele hapa duniani.
Na sio rahisi kukuacha uteseke pekee yako kama single mother.