Habari za weekend wakuu?
Kwanza kabisa bandiko hili halihusiani na wale wanaume ambao sio wawajibikaji wanaokwepa majukumu yao wakishawazalisha wanawake na halihusiani na wanawake waliozalishwa na waume za watu(hii inaitwa single mother by choice).
Kuna mambo yanahuzunisha sana kwenye jamii zetu ikiwemo hili wimbi la dada zetu/ wanawake kuzalishwa bila ya ndoa na kuachwa. Kuna muda wanaume tunabebeshwa lawama kuhusu hali hii kwa kuwaacha ambao tumewazalisha na kuoa wanawake wengine lakini chanzo kikubwa ni wao wenyewe.
Kwa hali niliyoishuhudia ni dhahiri single mothers watazidi kuongezeka kila uchwao. Kuna dada(huyu sio shemeji jamaa hataki kabisa nimwite shemeji) kazalishwa na jamaa yangu (wapo mikoa tofauti), huyu jamaa bado mambo sio freshi ila anajitahidi sana kumhudumia mwanae na huyu dada kwa kumlipia kodi, chakula n.k(ni wajibu wake).
Kinachonishangaza ni namna huyu dada anavyomtreat baba mtoto wake na kila tukikutana/kuonana hachoki/hakomi kusema mume wangu/baba fulani akinioa nitafanya hivi mara nitafanya vile(jamaa hana mpango nae zaidi ya kulea mtoto alishafanya uamuzi wa kutokumuoa kutokana na tabia zake), kiukweli huwa nabaki namsikitikia tu maana mwanaume mwenye utimamu wa akili hawezi kuoa mwanamke mwenye tabia za hovyo kiasi hiki. Umezaa na mwanamke lakini kila siku ni matukio, ukinyanyua simu kumpigia au kupokea ni matukio tu hayaishi leo hili kesho lile . Kwa tabia hizi baadhi kama za huyu dada naziorodhesha hapa chini kwanini usiwe single mother milele?
- Unamgeuza mtoto kuwa njia ya kipato chako&mtaji, hii ipo sana kwa wanawake wengi wanatumia watoto kama chanzo cha kupata pesa. Mahitaji ya muhimu ni haki kwa mtoto ila ukizidisha miamala ni upigaji kama upigaji mwingine. Kila siku ni kuomba hela wiki nzima unadanganya mtoto anaumwa na haumwi na sababu nyinginezo nyingi na hela ikishapatikana ni bando tu kucha kutwa kushinda tiktok na instagram. Hapa hata nilipwe mshahara ili nimuoe mwanamke wa hivi sioi.
- Unamtukana na kumfokea baba mtoto wako, huku ni kukosa heshima. Hili ndio lililonifanya nilete ili bandiko, hivi mwanamke mwenye heshima na unaitaka ndoa unaanzaje kumtukana mwanaume? Unamwambia mwanaume acha Useng3 we ms3nge tuma hela mtoto anaumwa na ni mzima kabisa kisa tu umelala huna bundle alafu unategemea huyo baby dady ndio aje akufanye mke? Kuna wanaume wanataabika sana kisa hawa watoto.
- Hutaki kufanya chochote/ kujishughulisha, mwanaume anajibana anakufungulia biashara hutaki kufanya mpaka inakufa unachotaka ni kukaa tu kuwa goli kipa. Ni kushinda mtandaoni tu na kuzurura kwenye events ambazo hazina umuhimu wowote ule.
- Wivu wa kipuuzi uliopitiliza, ukipiga simu isipopokelewa au ikiwa inatumika ni ugomvi na maneno ya hovyo kama vile ulikuwa na wanawake zako wengine wa huko na kujinunisha wiki nzima.
- Mazoea na wanaume, hii ni kujirahisisha kila mwanaume unamlilia shida zako tena kwa kumkandia baba mtoto kuwa hajali na haudumii chochote.
- Endeleza tabia nyinginezo zinazochangia wimbi la single mothers
Kwa tabia hizo nambariki mwamba kwa uamuzi aliouchukua nitoe angalizo kwa wanaume wenzangu tuwe makini starehe ya siku moja isijetugharimu maisha yetu yote, sio kila mwanamke ni wakupita nae tena pekupeku.
Kwenu wanawake mnaofanya haya ya kufanana na hayo alafu mnategemea kuolewa hivi mtu uko timamu kabisa unafanya mambo ya hovyo kama hayo alafu unakaa unasubiri kuolewa kabisa na unamuomba Mungu kabisa akubariki kwenye hilo?
Swali fikirishi. Kwa tabia alizonazo dada yako/zako ukiambiwa uoe mwanamke mwenye tabia zinazofanana na zake utaoa? Au ndio utajoin group la KATAA NDOA?
NAWASILISHA....
View attachment 2688750