sintokuja kuoa mwanamke mwenye mtoto mtu asiguse coment yangu.
 
kuna wengine hawana shida mkuu na kaburi la mumewe lipo anakuoneshah! Ila walio wengi hawajatulia usije ukajaribu

kuna wengine hawana shida mkuu na kaburi la mumewe lipo anakuonesha
ndo mpaka tufanye uhakiki maana wengi tabia zao hatuzijui mwanzo wanakuwaga wapole mno oa sasa uone kazi ilivyo.
 
Leo nilikuwa instagramu kwa wanaotumia huu mtandao, kwenye page ya wasafi FM wameongelea mada ya wanawake wanaozaa na waume za watu, nikataka kujua maoni ya watu juu ya hili ikabidi nisome comments….. mh!

Kama tunadhani kuna wanawake wanafanya efforts zozote kuepukana na hili wimbi la usingle mother then tunatakiwa tufikirie tena.

Kwa ujumla ni kuwa hawajali, na hawana mpango wa kujali, labda tuko kwenye dunia ya hivyo, tunawafikiria wasiojifikiria, wasiofikiria future ya watoto wao, wasiofikiria mustakabali mzima wa malezi ya watoto wao…….etc

Mtu anasema kabisa kuwa nikimpenda mwanaume nazaa tu, tukutane kwenye urithi 😂 unamfikiria huyu anaelewa kweli anachokiongea?
 
kuna baadhi ya single moms wamejitakia kuwa hivyo na hawajali chochote kwa kuwa n maamuzi yao hasa hao wanaozaa na waume za watu, hao wanachowaza ni mali tu sio kingine sasa hapo mtoto atapata malezi gani kama sio ya hovyo?
sasa hivi hili ni janga kubwa nafanya kazi na wadada wa5, wa4 ni single moms na vitabia vyao ni vya hoooovyo kweli hata mimi nisingeweza kuvumilia.
 
Hili nalo lina ukweli wake

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 


Binafsi huwa sipendi kabisa kabisa mno mwanamke mwenye mazoea na wanaume hata akiwa ni girlfriend tu achana na mke. Eti mwanamke ana rundo la male besties; na wote anabebishana nao; na hata kuwatembelea/kutembelewa na kuonana nao physically pamoja na kupewa pesa.

Hizi ni red flags ambazo ukizipuuzia zitakuja kukugharimu sana huko mbele ya safari maana kusema kweli hakuna urafiki wa bure bure tu kati ya mwanamke na mwanaume ambaye siyo ndugu wa karibu. Mwanaume anakupa pesa kisa eti ni male bestie na asitegemee cho chote kutoka kwako? We ulisikia wapi?

Matokeo yake unakuja kugundua kuwa hawa ma male besties wake kumbe baadhi yao, kama siyo wote, huwa wanamla.

Huwa inauma sana hasa kama binti unamkubali na una mipango naye ya muda mrefu. Siwalaumu wanaoishia kukimbia japo binafsi sitakaa nikimbie jukumu takatifu la kulea kiumbe kimalaika nilichoshiriki kukileta hapa duniani tena bila ridhaa ya chenyewe. Hata mamake awe pasua kichwa namna gani tutapambana hivyo hivyo tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…