hayo yafanyike kwa mipango na taratibu sio kukurupuka
 
umesema vyema kabisa mkuu, mwanamke akishakuwa na mazoea na wanaume wengi huyo ni chawote tena kwa anaetanguliza shida ndio hana namna ya kuliepuka hili
 
"2. Unamtukana na kumfokea baba mtoto wako, huku ni kukosa heshima. Hili ndio lililonifanya nilete ili bandiko, hivi mwanamke mwenye heshima na unaitaka ndoa unaanzaje kumtukana mwanaume? Unamwambia mwanaume acha Useng3 we ms3nge tuma hela mtoto anaumwa na ni mzima kabisa kisa tu umelala huna bundle alafu unategemea huyo baby dady ndio aje akufanye mke? Kuna wanaume wanataabika sana kisa hawa watoto."



Hio no mbili ndio ilisababisha nikaachana na mzazi mwenzangu na bado anaendelea na hio tabia so solution nimeamua kukaa kimya na kukata huduma nilizokua natoa ili awe na haki kabisa ya kunitukana
 
aise too bad hivi wanapata wapi huo ujasiri wa kumtukana mwanaume? Tena mbaya zaidi mwanaume anaetekeleza wajibu wake
 
Hiyo siyo sheria bali ni busara.

Sheria inasema mtoto awe na miaka 7+ ndiyo alelewe na baba
Kifungu cha 26( 2 ) cha Sheria ya mtoto, namba 21 ya 2009 kinasema kuwa ni vizuri mtoto aliye chini ya umri wa miaka saba akae na mama. Hata hivyo ni vema kufahamu kuwa kifungu hiki hakikusema ni lazima( shall) mtoto wa umri huo akae na mama.
Kifungu kinasema suala la mtoto chini ya umri wa miaka saba kukaa na mama ni dhana inayoweza kutozingatiwa( rebuttable presumption). Ni dhana inayoweza kutozingatiwa kwa maana kuwa zipo sababu ambazo mtoto chini ya umri huo inaweza kuamuliwa kukaa na baba au mtu mwingine yeyote ambaye ataonekana kufaa zaidi kuliko mama.
Kwahiyo lazima tuzingatie kuwa sio lazima mtoto chini ya umri wa miaka 7 kukaa na mama.
 
Kifupi mleta mada ukitaka yote hayo yasikukute oa officially usizalishe kwanza

Peleka posa ,pangiwa mahari lipa,funga ndoa kidini kisha mzae baada ya ndoa hizo shida huwezi ona sababu kazaa ndani ya ndoa sio barabarani

Ukizaa barabarani mwanamke hana marriage security kuwa ana uhakika kama mke au mwanawe kupata huduma ya mzazi wa kiume sababu hana hata cheti chochote cha kisheria kama cha ndoa ukimbwaga.Atakosa pa kukimbilia yeye na mwanawe.

Solution rasmisha acha ubwege.Peleka posa,kalipe mahari na urasimishe kwa ndoa ya kidini huo.ujinga utaisha
 
Bidada unakuwaga una hekima mno ninaposoma comment zako, mtu atayekuoa au kama umeolewa kapata mtu sahihi sana huna ufeminism na ushindani wakijinga na wanaume
 
Wanawake wa ckuiz Ni miyeyusho Sana, atakung'ang'ania umzalishe ili akugeuze kiteka uchumi chake kila siku haishi kukupiga mizinga.

Huyo jamaa yako Ana akili Sana aachane na huyo mchunaji aendelee na maisha Yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…