View attachment 2689550
Binafsi huwa sipendi kabisa kabisa mno mwanamke mwenye mazoea na wanaume hata akiwa ni girlfriend tu achana na mke. Eti mwanamke ana rundo la male besties; na wote anabebishana nao; na hata kuwatembelea/kutembelewa na kuonana nao physically pamoja na kupewa pesa.
Hizi ni red flags ambazo ukizipuuzia zitakuja kukugharimu sana huko mbele ya safari maana kusema kweli hakuna urafiki wa bure bure tu kati ya mwanamke na mwanaume ambao siyo ndugu wa karibu. Mwanaume anakupa pesa kisa eti ni male bestie na asitegemee cho chote kutoka kwako?
Matokeo yake unakuja kugundua kuwa hawa ma male besties wake kumbe baadhi yao, kama siyo wote, huwa wanamla.
Huwa inauma sana hasa kama binti unamkubali na una mipango naye ya muda mrefu. Siwalaumu wanaoishia kukimbia japo binafsi sitakaa nikimbie jukumu takatifu la kulea kiumbe kimalaika nilichoshiriki kukileta hapa duniani tena bila ridhaa ya chenyewe. Hata mamake awe pasua kichwa namna gani tutapambana hivyo hivyo tu!
View attachment 2689570