Hili swala lina dhana pana sana na linahitaji Mwanaume anayejitambua kama mimi na kujua dhamani ya mwanamke,
single mother ni wanawake kama walivyo wanawake wengine,
Tatizo la mmoja usiwausishe wote kwani hata katika ukoo wako ukichunguza huwezi kosa single mother,
Kwa hiyo unapo nyoosha kidole angalia vingine vinapoelekea.
Jaribu "kupambana na hali yako " kijana.
Haya mengine yaache ukikuwa utaelewa.
 
Vizuri mganga wa ukoo tumloge nini huyu mtoto?
 
Sema sio wote kwani wengine ni bahati mbaya ama kubakwa, kuachika chanzo ni mwanaume, kufiwa nk. Kuna single mother wazuri sana na wenye nyota nzuri ukiwapata wewe ni kupaa tu. Naomba ubadilishe ile kauli ya soda, Mbona umeshazinywa nyingi bila kujijua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshuhudia Mimi Mdingi aliwahi kuoa single mother imefika uzeeni wale watoto wasio wake ndio msaada mkubwa kwake kuliko wanae aliowazaa. Hata kabla hajafariki alitamka kua hao ndio wanae.

Akawa anawakataa watoto waliotoka viunoni mwake.

Msiwe na majibu rahisi kwenye maisha ambayo ni complex sana.

..No one knows what future may hold ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pata kiroba hapo kwa mangi nitalipa ndugu yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda hata mama yako alikuwa in single mother babaako angeona hivyo,hata Ww usingezaliwa ,lkn kwa mwanaume umejitahidi japo sijajua kazi yako ,mwanaume WA awamu yatano unapata wapi muda WA kutafiti mambo ya ajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mambo ya ajabu yanapaswa kufanyiwa utafiti. Kama umekugusa vumilia
 
kiukweli nawapenda single mama.. ni moja kati ya wanawake wenye akili na wavumilivu..wenyebusara na subira...
 
Ndio maana nikasema asiyezaa aliyezaa wote sawa tuu achana na past ya mtu wewe angalia ulivyomkuta pambana na hali
Sawa kivipi mkuu hebu dadavua vizuri
Yaan aliye na mtoto ni sawa na asiyetoa hebu kuwa serious au unamaanisha aliyetoa mimba ni sawa na aliyewahi kuwa na mtoto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi kipi bora kuoa single mama au mwanamke aliyetoa mimba saba?unafikiri yupi anamaumivu? bado mdogo hujui bado kwanini hayo yalitokea hivyo kuwa na muda wa kutosha wa kujifunza zaidi kuliko kuwahukumu.
hebu jaribu kuvaa uhusika wa mazingira hayo au huyo ndio mama yako.
 
Kuna hali huwa inatokea wakajikuta hivyo, muombe Mungu wako akupe hekima, una dada, mama wadogo na hata watoto wako wa kuwazaa, ipo siku watajikuta kwenye mazingira kama hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…