Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Mikutano ya kisiasa iliyozuiwa kwa miaka mitano huku CCM wakiifanya kwa mgongo uzinduzi wa vitu au miundombinu iliyojengwa kwa fedha za wananchi ,misaada na mikopo kutoka benki mbalimbali za duniani.

Miezi 2 tu ya kampeni Mh. Tundu Lissu (unshakable) ameleta kimbunga ambacho kinawasomba wanaCCM na viongozi wao mpaka imefika hatua ilani yao wameiweka kando na kutoa ahadi za papo kwa papo bila kujali ilani yao inasemaje.

Mikutano na wanahabari haikatiki sasa ili kujikinga na kimbunga cha Lissu. Itokee CCM waendelee kutawala au waanguke 28 Oct. hawataweza kukisahau kimbunga cha Lissu.
 
Back
Top Bottom