Mhe. Lissu salaam, pole na majukumu na mizungunguko yako ya kunadi sera zinazotugusa sie tulio wanyonge haswa. Binafsi nimekuwa nikikufutilia kwa karibu kampeni zako popote kwa njia ya mtandao na agharabu niliwahi kuhudhuria kwenye uzinduzi wa kampeni moja mkoa wa nyanda za juu kusini, hakika Mungu akulinde.
Kuna mambo mengi yakuleta matumaini umekuwa ukiyaeleza vizuri namna utakavyo yashughulkia kwa kweli inatia moyo. Lakini kuna jambo moja bado hujaliweka wazi sana namna utakavyo shughulika nalo na hili unalijua lina kundi kubwa la watu na unalijua vizuri.
Binafsi pia ningependa uliongee kila pahala unapokwenda kunadi sera (nitalieza). Kwakifupi niorodheshe mambo unayoyaeleza vizuri na hayana shaka ili uliongeze na hilo liwe miongoni mwa haya(msomaji waweza ongeza ambayo nimesahau) .
1. Kila mtanzania kumpatia bima ya afya
2.Kuongeza mishahara kwa watumishi(mujibu wa sheria)
3. Kulipa malimbikizo kwa watumishi.
4. Kurudisha fao la kujitoa
5. Kupunguza makato bodi ya mikopo mpaka 3% ya awali
6. Kutoa mikopo kwa waombaji/ wanafunzi wote elimu ya juu.
7. Kulipa fidia kwa wahanga waliobomolewa nyumba zao kupisha ujenzi wa barabara na kuwafariji wahanga wa tetemeko Kagera.
8. Kuondoa kitambulisho cha ujasiliamali kwa machinga na wengineo
9. Kuwapatia watanzania katiba mpya(ya Jaji Warioba).
10. Kurudisha ardhi iliyopokwa kwa wananchi.
11. Kuwatoa magerezani Mashehe wa uamsho(na wanaharakati waliobambikiwa kesi).
12. Kuunda tume ya maridhiano kwa viongozi waliojihusisha kunyanyasa raia bila makosa ukiwemo wewe, kuuweka bayana wa mambo hayo na sababu ya kufanyika kwake na kisha kusamehana.
13. Kuondoa vikwazo kwa wakulima (kundoa kodi za magetini, kuwa na soko huru na upatikanaji rahisi wa pembejeo za kilimo pamoja na bei zake).
14. Kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara(kuondoa kodi mpaka kufika 10%, kuifumua upya TRA, nk).
15. Kuweka mazingira safi ya Uwekezaji ili kukuza uchumi na kuongeza ajira.
16. Kurekebisha mfumo wa elimu ili uweze kumpa maarifa mwanafunzi na sio kuongeza ufaulu tu bila kuwa na maarifa. (Kuaandaa wasomi watakaoajirika popote duniani na kuwa katika soko la ushindani).
17. Kuzipa nafasi sekta binafsi kuratibu shughuli zao kwa uhuru na kuifanya serikali kuwa msimamizi na kuzipa mazingira safi ya shughuli zao.
18. Kuwa na serikali za majimbo na viongozi wake kupatikana kwa kuchaguliwa ama kuondolewa na wananchi(kurudisha nguvu na mamlaka kwa wananchi).
19. Kulinda na kutetea haki, utu, na uhuru wa kila raia.
20. Kujenga uhusiano mzuri na mataifa mengine(Diplomacy Restoration)ambayo pengine yamezorota hivi karibuni.
21. Kuondoa laana ya rasilimali(wananchi kutobugudhiwa/kubezwa kwa rasilimali zinazopatikana maeneo waliopo/yanaowazunguka). Raia kuwa wanufaika kwa rasilimali zinazopatikana mahala walipo.
22. Kurudisha uhuru wa vyombo vya habari (kuondoa sheria kandamizi za utoa aupokeaji wa habari)
23. Kuondoa kinga ya viongozi na kupunguza mamlaka ya Rais. (Kuweza kushtakiwa akifanya makosa). nk nk
Kwa uchache hayo ndiyo nayasikia mara nyingi na yanatugusa mojakwamoja. Sasa hitaji langu nitajikita kwenye namba 16 kwa sababu kwa namna moja ama nyingine vijana na wazazi wameathiriwa vibaya mno na hili.
MFUMO WA ELIMU na AJIRA kwa VIJANA
------------------------------------------------------
Mh. T. A. Lissu kama unavyojua mfumo wa elimu umekuwa ukituandaa vijana kuwa tegemezi(dependents) yaani soma, faulu, na uandaliwe ajira. Mfumo huu hautupi uwezo wa maarifa na kisha kupambana na mazingira bali uajiriwe baada ya kuhitimu. Hiki ndicho kinachogharimu wasomi wengi na kufifisha matumaini kwa wazazi wanaosomesha vijana wao. Nimeridhika na namna unavyotaka sekta binafsi zipunguze tatizo la ajira lakini ujue kuna kundi lililomaliza vyuo toka 2015-2020 almost 6years halina ajira rasmi na liliandaliwa na mfumo huo tegemezi wa elimu.
Hivyo basi ningependa katika kampeni zako ungeliongelea katika kila mkutano wa kampeni ipi mipango mikakati ya dharura ya kushughulika na kundi hili kabla ya kuanza na mfumo mpya wa elimu. Kumbuka hawa vijana ni kundi kubwa wao na wazazi/walezi wao wanataka kujua hatma yao na namna utawafanya wawe kwenye ajira rasmi.
Serikali ya sasa nikama haina mipango yoyote juu ya hili na ndio maana kumekuwa na ukosefu mkubwa wa ajira kwa miaka hii mitano. Hawa ni vijana waliosomeshwa na wazazi maskini kwa kuuza mazao yao, mali zao, mashamba, mifugo ili tuu wapate elimu.
Katika kundi hili ni wachache wanaopatiwa ajira rasmi agharabu kwa wale wenye ndugu walio na nafasi kubwa serkalini ila the rest wapo mitaani. Kwa heshima yako naomba utoe mwongozo kwa vijana, wazazi au walezi kila mkutano wako wa kampeni maana ni tatizo la nchi nzima.
Asante na kila la kheri katika mapambano yako. (Nashuku katika kampeni zako jana 27/09/2020 Musoma umeanza kuliongelea kiundani, ningependa liwe ni endelevu kwa kila mkutano wako).
Naomba kuwasilisha.