Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
IMG_20200902_171055.jpg
 
Baada ya CHADEMA kuona kwenye viwanja hamna nyomi waanza kuzungusha misafara ya Lisu masokoni,kwenye vijiwe vya bodaboda mitaa ya machinga ili awapungie mikono picha walau zionyeshe kuwa apokelewa na maelfu kumbe anayafuata yaliko kabla kufika viwanja anakohutubia!! yaani analazimisha kupokelewa kwa kuwafuata watu huko huko waliko wampokee!!!

Yaani hata kama barabara iko straight lazima msafara upinde kona upite maeneo yenye watu wengi wauza mboga,sokoni,vijiwe vya bodaboda,wasukuma mikokteni walau ajisikie vizuri kuwa anapungiwa mikono

Chadema kwao kujaza watu viwanjani bado ni changamoto
Kawazuie wasimpokee... Usituchoshe.
 
Lakini nakumbuka Chadema walisema watakuwa wanaanza na maandamano kabla ya kwenda sehemu ya kufanyia Mkutano. Pengine hayo ndo maandamano yenyewe.
 
Baada ya CHADEMA kuona kwenye viwanja hamna nyomi waanza kuzungusha misafara ya Lisu masokoni,kwenye vijiwe vya bodaboda mitaa ya machinga ili awapungie mikono picha walau zionyeshe kuwa apokelewa na maelfu kumbe anayafuata yaliko kabla kufika viwanja anakohutubia!! yaani analazimisha kupokelewa kwa kuwafuata watu huko huko waliko wampokee!...
Lissu alishasema wataandama kabla ya Mkutano .... labda ndiyo hayo maandamano ya amani aliyoyazungumzia!!
 
Baada ya CHADEMA kuona kwenye viwanja hamna nyomi waanza kuzungusha misafara ya Lisu masokoni,kwenye vijiwe vya bodaboda mitaa ya machinga ili awapungie mikono picha walau zionyeshe kuwa apokelewa na maelfu kumbe anayafuata yaliko kabla kufika viwanja anakohutubia!! yaani analazimisha kupokelewa kwa kuwafuata watu huko huko waliko wampokee!...
Usisahau kwamba ni mkakati wa CDM kufanya kampeni nyumba kwa nyumba na kitanda kwa kitanda. Tutakwenda hadi masokoni na makazini kuwaeleza watu sera zetu.
 
Niende moja kwa moja kwemye mada, mimi ni mkereketwa wa chadema, ninapashwa kukishauri chama pale ambapo ninaona kabisa kuwa wanakosea na kukisifu pale ninapoona wanafanya vizuri.

Chadema imejipambanua kuwa hawana rasilimali pesa kuendesha kampeni zao na ndio maana tunachangia kidogo tulichonacho ili waweze kufanya kampeni vizuri.

Ile leo nimeshtushwa sana na nilichokiona, unawezaje kutoka mwanza kwenda shinyanga kwa ndege?

Ok, tuseme sio jambo baya, lakini ubaya unakuja kama ulisema hauna pesa. Ni jambo zuri kama una pesa. Haya matumizi yanayofanywa yananipa mashaka ya kuendelea kuchangia chama.

Kutoka Mwanza kwenda Shinyanga ni takribani kilomita 160 tu. Kwa mwendo wa magari waliyonayo si zaidi ya masaa mawili na nusu.
Kwa matumizi haya mabaya, nina mpango wa kusitisha kuchangia chama.

IMG_20200902_164928.jpg
 
Hao wagombea wa vyama vingine nawashauri wasilewe na wingi wa watu katika mikutano yao inayofanyikia Mijini, watakuja kulia siku ya uchaguzi baada ya kutangazwa matokeo.

Nilishuhudia mwenyewe uchaguzi wa mwaka 2015. Kule vijijini matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:

- Kituo A, CCM Kura 325 na Chadema Kura 17.

- Kituo B, CCM Kura 321 na Chadema Kura 12.

- Kituo C, CCM Kura 278 na Chadema Kura 13.

Kwa upande wa Mjini Chadema walikuwa wakijitahidi sana kwa baadhi ya vituo walikuwa wanaizidi CCM kwa Kura zisizozidi 12, 15 au 23 .
Kwa tathmini hiyo fupi ni kwamba, Kituo kimoja tu cha kijijini kina uwezo wa kukomboa vituo vingi vya mjini vilivyozidiwa na Chadema.
Kwa hiyo, ukweli ni kwamba, vyama vingine hata vifurukute namna gani, kwa upande wa Urais havitaweza kumshinda JPM.
 
Baada ya CHADEMA kuona kwenye viwanja hamna nyomi waanza kuzungusha misafara ya Lisu masokoni,kwenye vijiwe vya bodaboda mitaa ya machinga ili awapungie mikono picha walau zionyeshe kuwa apokelewa na maelfu kumbe anayafuata yaliko kabla kufika viwanja anakohutubia!! yaani analazimisha kupokelewa kwa kuwafuata watu huko huko waliko wampokee!...
Yangekuwa ni kweli unayoyasema ungekuja na supporting evidence.
 
Goma linaendelea kubuma buuuuuu!!!! Uraisi sio kila mtu anafaa, kuna mwingine kipaji chake ni kujua Sheria Tu Ila sio kuwa Raisi
Kuna mwingine kipaji chake mchambuzi mzuri wa hoja Ila sio kuwa Raisi, kuna mwingine mpiga kelele tu, Ila sio kuwa kiongozi maana atawapoteza.

Kuna mwingine anaweza kuonekana anafiti kuwa Raisi lakini Mungu mwenyewe hamtaki tu basi atafanya watu wampuuze Kwa kuwa Mungu ndiye aonaye sirini, na kiti hicho huombewa maombi yote, Kwa hiyo huwezi kulazimisha
 
Kuna kijana wa kizungu anamikwara bubu anakesha mitandaoni ati kuwatishia Watanzania wamchague wakala wao

Ndugu lissu ulimwahidi nini huyu bwana Roberts mbona anaweweseka?

Je, ulimwahidi madini yetu?

Je, ulimwahidi gesi yetu?

Au ulimwambia utawapa zawadi ya twiga km ndugu yako Nyalandu alivyokuwa anawepelekea

Au uliwaahidi utawapa ardhi?

Je, uliwaahidi bandari?

Au uliwaahidi Tanzania itakuwa hub ya madawa ya kulevya?

Umeula wa chuya ndugu hako ka robert katakufanya kitu mbaya ukirudi ubeligiji baada ya Uchaguzi

Hii ni Nchi ya Nyerere, USA alitushindwa, ujerumani akatuangikia, Malikia wa uingereza akanyoosha mikono

Sasa haka ka robert ati kanamtisha Tanzania, dunia haishi vituko
 
Goma linaendelea kubuma buuuuuu!!!! Uraisi sio kila mtu anafaa, kuna mwingine kipaji chake ni kujua Sheria Tu Ila sio kuwa Raisi...
Kwa maon yako, inahis Jiwe Aliwah kufaa kua Rais?

Mtu asokua na Hekima,wala Busara? Matusi yamemjaa km nn
 
Kuna kijana wa kizungu anamikwara bubu anakesha mitandaoni ati kuwatishia Watanzania wamchague wakala wao

Ndugu lissu ulimwahidi nini huyu bwana Roberts mbona anaweweseka?

Je ulimwahidi madini yetu?

Je ulimwahidi gesi yetu?...
Nitatoka nje ya siasa . Ila sentec yako yanmwisho. Kuwa america walitushindwa..ujerumani nao hivyo hivyo. Ndugu nikwambie tu.. kama ufaham ..kuwa ndege mbili za shirika la airtanzania ya kwanza kabisa..boeing 737-200. tulisaidiwa na wao wenyewe ndege zikapatikana.

America akiamua kutukomoa anaweza..na hapa mifano unaifaham. Usiilinganishe tz na america in powers. Wao ni moja ya super powers countries. .. ujerumani akiamua anaweza. The difference ni kwamba hawana interest kubwa na tanzania. Wana mambo makubwa wanayoshughulika nayo dunian.
 
Back
Top Bottom