Yes, Tundu Lissu umebakiza mikoa ya Dar, Pwani, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Manyara na Tanga. Najua mikoa yote ya kusini kwako itakuwa ni mtelezo maana utaungana na chama mshirika cha ACT Wazalendo katika kuipasua pasua CCM. Hapa Dar napo utaenda vizuri kufagia upepo alioacha Magufuli ambao nao hauvumi tena.
Najua bado pia Hai, Moshi mjini, Same na Mwanga bila kusahau Tukuyu, Kyela na Chunya.
Tukazane tumalize nchi maana muda nao unaenda sana hasa ukizingatia tuna siku 10 tu za kumaliza kampeni. Tunataka tufike mpaka Mafia hatuachi kitu.
Kila lakheri na Mungu akuepushie nongwa.