Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Hiki ndicho kigingi kilichobaki. Sijui upinzani umejipangaje katika hili; Ila tume ijue kabisa katika hili, mgombea wa sasa wa upinzani ni mpinzani kweli, si zao la CCM. Wasimame katika haki, watimize yale yaliyoamuliwa na wananchi wenyewe kwa manufaa ya nchi yao wenyewe. Wakifanya tofauti na watanzania waliyoamua tar 28 mwezi ujao wajue machafuko yatakayotokea, damu itakayomwagika haitawaacha salama.
Mungu ibariki Tanzania
Nafikiri JPM atakuja na some kind of deal hususani kwa Mbowe, nahisi JK na Mbowe watakaa chini watakuja na Compromise.

Na nahisi Compromise itakuwa kwenye katiba mpya, kwamba wamuachie JPM amalize muhula wa mwisho ila wao CDM waongoze mchakato wa kubadili katiba ila Uchaguzi wa 2025 uwe na tume huru etc.

Yaani hii ndio karata pekee ambayo CCM wanaweza kuicheza kwa sasa.
 
Maamuzi ya kiakili ni kuacha uhuru, haki itendeke na kuheshimu maamuzi ya wananchi tu si vinginevyo mkuu.
Tatizo CCM sio chama cha Siasa, CCM ni mfumo wa Maisha. Tumeona watia nia wa CCM kutoka kila kona ya Taasisi na Mashirika yawe ya Serikali au Binafsi.

Na sijui kama watakubali kuondolewa kwenye position zao kirahisi rahisi.
 
Nimestushwa sana na kujaa mshangao mkubwa kwa mapokezi.makubwa sana, ambayo naweza kuyaita siyo ya mafuruko tena, Bali ni ya kimbunga, aliyoyapata Tundu Lissu, jijini Mwanza, siku ya Jana, ambapo inasidikiwa kuwa yamevunja rekodi ya kupokelewa kwake, ambapo maelfu kwa maelfu, waliujaza uwanja wa Nyamagana, kumsikiliza shujaa huyu, Tundu Lissu akimwaga Sera yake, ambayo ni ya kuleta Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.
Kuna watu wamehudhuria ili kumshangaa coz
1. Hawajawahi kumuona live
2. Kweli ni yeye...? Maana hawaamini kana kweli amepona kwa mkasa uliompata. Na wakitoka kwenye mkatano, majadiliano ya wahudhuriaji wengi huwa yanahusu kupona kwa Lisu nasio sera za chama.
3. Kuna watu huwa wanahudhuria mikutano yote ya siasa, hawabagui chama.
4. Kuna watu wanahudhuria ili wajionee kama mgombea ata pata wahudhuriaji wengi (wanajikuta na wao ni miongoni mwa wahudhuriaji)

Hata JPM, huwa anajaza watu coz
1. CCM fiesta/festival (Tukamuone ZUCHU)
2. Tukamuone raisi wetu.

KUPATA WATU WENGI KWENYE KAMPENI SIO KIBALI CHA USHINDI.
 
Hapo ndio kwenye mtego, je wanaohudhuria wanaondoka na nini kwenye mkutano huo.

Lissu kafanya homework yake vizuri sana
Kwenye kampeni anaongea maneno machache sana.
 
Nafikiri JPM atakuja na some kind of deal hususani kwa Mbowe, nahisi JK na Mbowe watakaa chini watakuja na Compromise.

Na nahisi Compromise itakuwa kwenye katiba mpya, kwamba wamuachie JPM amalize muhula wa mwisho ila wao CDM waongoze mchakato wa kubadili katiba ila Uchaguzi wa 2025 uwe na tume huru etc.

Yaani hii ndio karata pekee ambayo CCM wanaweza kuicheza kwa sasa.
Hilo halitawezekana kabisa.........

Na Tundu Lissu amelielezea kwa undani kabisa suala hili kwa kuwatahadhalisha watawala hawa wa CCM kuwa wasithubutu kufanya wizi kwa uchaguzi huu, ama sivyo wote watakaofanya "upuuzi" huo wataishia kuburuzwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya The Hague, kule Uholanzi!

Akaendelea kutoa uthibitisho wa hiko anachosema kwa kueleza kuwa kama Magufuli anataka yamkute yaliyomkuta mwenzie Laura Gbabo, basi athubutu kufanya wizi wa kura katika uchaguzi huu
 
Tatizo CCM sio chama cha Siasa, CCM ni mfumo wa Maisha. Tumeona watia nia wa CCM kutoka kila kona ya Taasisi na Mashirika yawe ya Serikali au Binafsi.

Na sijui kama watakubali kuondolewa kwenye position zao kirahisi rahisi.
Na hili ndio tatizo kubwa; wale waliokwenye nafasi flani flani wakifikiria baada ya ushindi wa upinzani hawatakuwa tena katika hizo nafasi na ndiomana wanatengeneza figisu nyingi, wako tayari hata kumwaga damu za watanzania ili kulinda maslahi yao. Sawa ila wakati wa Mungu mwenyewe kufanya mabadiriko kupitia sauti ya wengi huwa hauchelewi wala haukawii bali huja kwa muda muafaka. Huwa hauwangalii waneemekaji na mfumo dhalimu wanalia kwa machozi ya damu au wamevaa magunia wakitubu na kuomba neema.
Wakati ni sasa tar 28
 
Nafikiri JPM atakuja na some kind of deal hususani kwa Mbowe, nahisi JK na Mbowe watakaa chini watakuja na Compromise.

Na nahisi Compromise itakuwa kwenye katiba mpya, kwamba wamuachie JPM amalize muhula wa mwisho ila wao CDM waongoze mchakato wa kubadili katiba ila Uchaguzi wa 2025 uwe na tume huru etc.

Yaani hii ndio karata pekee ambayo CCM wanaweza kuicheza kwa sasa.
Mbowe na kamati kuu ya Chama watakuwa wamewasaliti watanzania. Hayo maswala ya katiba yanaweza yakafanyika Tundu Lissu akiwa mjengoni kama rais wa awamh ya 6 wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Hilo halitawezekana kabisa.........

Na Tundu Lissu amelielezea kwa undani kabisa suala hili kwa kuwatahadhalisha watawala hawa wa CCM kuwa wasithubutu kufanya wizi kwa uchaguzi huu, ama sivyo wote watakaofanya "upuuzi" huo wataishia kuburuzwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya The Hague, kule Uholanzi!

Akaendelea kutoa uthibitisho wa hiko anachosema kwa kueleza kuwa kama Magufuli anataka yamkute yaliyomkuta mwenzie Laura Gbabo, basi athubutu kufanya wizi wa kura katika uchaguzi huu
Kwenye hili la ICC Tanzania inaweza kujitoa, japokuwa kujitoa kunaweza kuleta implications kwenye misaada ya Kimataifa.

Prof. Kabudi anaweza kuja na hoja Kama Donald Trump haiamini ICC kwa nini Tanzania iiamini Taasisi hiyo?
 
Mbowe na kamati kuu ya Chama watakuwa wamewasaliti watanzania. Hayo maswala ya katiba yanaweza yakafanyika Tundu Lissu akiwa mjengoni kama rais wa awamh ya 6 wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tuombe dua, kwa sababu at some point ni lazima TL apunguzwe makali. Speech zake japokuwa ni fupi lakini zinachoma sana, anaongea mambo ambayo hakuna mtu yoyote amejaribu kuyaongea kwa miaka 5.

Swali linakuja atazuiliwa aje?
 
Nani wa kumpunguza makali na kwa njia gani au makubaliano gani? He has nothing to loose mkuu. The guy survived 16 bullets remember
Kama ni mpango wa Mungu awe rais wa Tanzania hakuna namna......
 
Na hili ndio tatizo kubwa; wale waliokwenye nafasi flani flani wakifikiria baada ya ushindi wa upinzani hawatakuwa tena katika hizo nafasi na ndiomana wanatengeneza figisu nyingi, wako tayari hata kumwaga damu za watanzania ili kulinda maslahi yao. Sawa ila wakati wa Mungu mwenyewe kufanya mabadiriko kupitia sauti ya wengi huwa hauchelewi wala haukawii bali huja kwa muda muafaka. Huwa hauwangalii waneemekaji na mfumo dhalimu wanalia kwa machozi ya damu au wamevaa magunia wakitubu na kuomba neema.
Wakati ni sasa tar 28
Watawala wetu na wanaccm wote, wanapaswa kuanzia sasa wajiandae kisaikolojia kuweza kukabidhi madaraka ya nchi kwa Tundu Lissu, bila kusababisha unwagikaji wa damu ya wananchi wasio na hatia............

Hiyo ndiyo "solution" pekee ninayoiona wanayoweza kuifanya ndugu zetu maccm
 
Nakubaliana nawe mkuu.
 
Nimestushwa sana na kujaa mshangao mkubwa kwa mapokezi.makubwa sana, ambayo naweza kuyaita siyo ya mafuriko tena, Bali ni ya kimbunga na ya kihistoria aliyoyapata Tundu Lissu, jijini Mwanza, siku ya Jana, ambapo inasidikiwa kuwa yamevunja rekodi ya kupokelewa kwake, ambapo maelfu kwa maelfu, waliujaza uwanja wa Nyamagana, kumsikiliza shujaa huyu, Tundu Lissu akimwaga Sera yake, ambayo ni ya kuleta Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.

Mapokezi hayo ameyapata huku vyombo vyote vya habari hapa nchini, vikiwa vimempa "blackout" bila kutangaza ratiba ya ujio wake!

Kilichonistua zaidi ni kuwa hapo jijini Mwanza ndipo tuliaminishwa kuwa ndiyo ngome kubwa ya mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli

Nadiriki kusema kuwa huyu Tundu Lissu, kwa hivi sasa, hakuna mtu anayeweza kumzuia kufikia azma yake ya kuwa Rais wa 6 wa nchi hii, katika uchaguzi mkuu ujao!

Kama alivyosema, mtumishi wa Mungu, Augustine Mwingira kuwa, huyu Tundu Lissu, hajajenga mafly overs wala hajajenga SGR, hajajenga chochote ndani ya nchi hii,lakini kila anapokwenda, watu maelfu kwa maelfu wanamfuata!

Ndipo hapo Mwingira alipomalizia mahubiri yake kwa kusema kuwa I DON'T UNDERSTAND THIS!

Nami na watanzania wenzangu ni lazima hivi sasa tujiulize hivi hii hali ya kupendwa kupita kiasi kunatokana na nini, kama siyo kuinuliwa kwa njia ya muujiza na Mungu mwenyewe, kutokana na mapitio aliyopitia huyu Tundu Lissu kwa kumwokoa na zile "mvua" za risasi, ambazo watesi wake, waliamini kabisa kuwa zitakuwa "zimeshammaliza" lakini kwa muujiza mkuu wa Mungu, hadi Leo anatembea huku akiwahubiria upendo watanzania wote na kuwa hana nia ya kulipiza kisasi na atakuwa amesamehe mara saba mara sabini kwa yote aliyopitia!

Hiyo ni kuthibitisha kuwa mawazo yetu sisi binadamu na tunachopanga, sicho kinachopangwa na Mungu wetu

Mungu ibariki Tanzania na endelea kumjazia baraka zako mja wako Tundu Lissu
Sawa mkuu lakini mafuriko hayo huwezi linganisha ya yale Rais Magufuli. Mbili unkiangalia kwa makini utaona washangiliaji wote wako mbele ya lakini watu walio nyuma wengi ni wasikilizaji tu.

Kitu kingine nacho taka kukueleza ili usije pata mshangao kwenye matokeo ni kwamba shangwe nyingi katika mafuriko hayo inasikika kutoka kwa watu wachache, umejiuliza kwa nini? Kujaa kwa watu ni kawaida hasa mikoani maana vitu kama hivyo hawavioni kila wakati.

Lakini kwa umati wa watu kujaji kuwa ndiyo wingi wa kura hiyo nakukatalia na naona umeitoa mbali sana. Unauhakika gani kuwa hao wote wataenda piga kura? Na watampigia nani? Usijidanganye kwa hilo kwani ukilinganisha na mwaka 2015 Lowassa alipata watazamaji wengi sana kuliko Lissu na isoteshe kulikuwa na wasaliti wengi sana waliokimbia kutoka CCM, wewe mwenyewe unajua na pia Magufuli alikuwa bado hana umaarufu kama wa hivi sasa, lakini hata hivyo alishinda.

Sasa leo unataka kuniambia kwa mafanikio haya yote ambayo Magufuli ameyaleta na kuyaonyesha, watanzania wamwache yeye waende kumpigia kura mtu ambaye hawaju ataipeleka wapi hii nchi? Basi nafikiri watanzania hao watakuwa wamelogwa au akili zao sio timamu.

Yaani mtu kama wa Dar, Morogoro, Dodoma, Singida na Mwanza aache kuipigia kura SGR badala yake apigie kura risasi 16 ambazo hazina ukweli ndani yake. Hayo yatakuwa maajabu makubwa sana.

Wana Dar waache kumpigia mtu ambaye ameondoa foleni barabarani na umeme wa mgao badala yake wampigie kura mtu kwa ajili ya huruma?

Zaidi ya hayo chukulia idadi ya wanachama wa CCM na ile ya CHADEMA, hapo peke yake inaonyesha jinsi gani CCM hata bila Magufuli wamejipanga. Na ukiongeza umaarufu wa Magufuli hapo si utaenda kichaa?

Any way sitaki kukukatisha tamaa, ngoja niishie hapo. Ni vizuri watu wanakwenda kumsikiliza ni wajibu wao na haki yao, lakini usw exagerate kuwa wingi huo wa watu ndiyo idadi ya wapiga kura na hata recorde ya Rais bado hajaivunja.
 
Nani wa kumpunguza makali na kwa njia gani au makubaliano gani? He has nothing to loose mkuu. The guy survived 16 bullets remember
Kama ni mpango wa Mungu awe rais wa Tanzania hakuna namna......
Ndio maana nakwambia njia pekee ya kumpunguza makali Lissu ni kumzunguka.

Njia inayotumika kwa sasa haimtishi kwa sababu hana cha kupoteza.

Ila all in all CCM wamechemsha kwenye kila kitu, hata watu ambao wangetumika kumzunguka TL (Kinana, Makamba, JK) waliwekwa pembeni wakidhalilishwa, wakakebehiwa n.k

Anyway siku zimebaki chache tusubiri tuone.
 
Kuna watu wamehudhuria ili kumshangaa coz
1. Hawajawahi kumuona live
2. Kweli ni yeye...? Maana hawaamini kana kweli amepona kwa mkasa uliompata. Na wakitoka kwenye mkatano, majadiliano ya wahudhuriaji wengi huwa yanahusu kupona kwa Lisu nasio sera za chama.
3. Kuna watu huwa wanahudhuria mikutano yote ya siasa, hawabagui chama.
4. Kuna watu wanahudhuria ili wajionee kama mgombea ata pata wahudhuriaji wengi (wanajikuta na wao ni miongoni mwa wahudhuriaji)

Hata JPM, huwa anajaza watu coz
1. CCM fiesta/festival (Tukamuone ZUCHU)
2. Tukamuone raisi wetu.
3. Kuna watu huwa wanahudhuria mikutano yote ya siasa, hawabagui chama.

KUPATA WATU WENGI KWENYE KAMPENI SIO KIBALI CHA USHINDI.
Watanzania wanapenda mikusanyiko na nimependa point yako ya hawabagui. Ukienda underground ndo utauona ukweli tusubiri 28 just few weeks from now
 
Nimestushwa sana na kujaa mshangao mkubwa kwa mapokezi.makubwa sana, ambayo naweza kuyaita siyo ya mafuriko tena, Bali ni ya kimbunga na ya kihistoria aliyoyapata Tundu Lissu, jijini Mwanza, siku ya Jana, ambapo inasidikiwa kuwa yamevunja rekodi ya kupokelewa kwake, ambapo maelfu kwa maelfu, waliujaza uwanja wa Nyamagana, kumsikiliza shujaa huyu, Tundu Lissu akimwaga Sera yake, ambayo ni ya kuleta Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.

Mapokezi hayo ameyapata huku vyombo vyote vya habari hapa nchini, vikiwa vimempa "blackout" bila kutangaza ratiba ya ujio wake!

Kilichonistua zaidi ni kuwa hapo jijini Mwanza ndipo tuliaminishwa kuwa ndiyo ngome kubwa ya mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli

Nadiriki kusema kuwa huyu Tundu Lissu, kwa hivi sasa, hakuna mtu anayeweza kumzuia kufikia azma yake ya kuwa Rais wa 6 wa nchi hii, katika uchaguzi mkuu ujao!

Kama alivyosema, mtumishi wa Mungu, Augustine Mwingira kuwa, huyu Tundu Lissu, hajajenga mafly overs wala hajajenga SGR, hajajenga chochote ndani ya nchi hii,lakini kila anapokwenda, watu maelfu kwa maelfu wanamfuata!

Ndipo hapo Mwingira alipomalizia mahubiri yake kwa kusema kuwa I DON'T UNDERSTAND THIS!

Nami na watanzania wenzangu ni lazima hivi sasa tujiulize hivi hii hali ya kupendwa kupita kiasi kunatokana na nini, kama siyo kuinuliwa kwa njia ya muujiza na Mungu mwenyewe, kutokana na mapitio aliyopitia huyu Tundu Lissu kwa kumwokoa na zile "mvua" za risasi, ambazo watesi wake, waliamini kabisa kuwa zitakuwa "zimeshammaliza" lakini kwa muujiza mkuu wa Mungu, hadi Leo anatembea huku akiwahubiria upendo watanzania wote na kuwa hana nia ya kulipiza kisasi na atakuwa amesamehe mara saba mara sabini kwa yote aliyopitia!

Hiyo ni kuthibitisha kuwa mawazo yetu sisi binadamu na tunachopanga, sicho kinachopangwa na Mungu wetu

Mungu ibariki Tanzania na endelea kumjazia baraka zako mja wako Tundu Lissu
 
Attachments

  • VID-20200925-WA0000.mp4
    22.2 MB
Watanzania wanapenda mikusanyiko na nimependa point yako ya hawabagui. Ukienda underground ndo utauona ukweli tusubiri 28 just few weeks from now
Siyo kweli kuwa watanzania wanapenda sana mikusanyiko..................

Kwanini hujiuluzi kama ni hivyo ni kwanini kati ya wagombea Urais 16 waliopitishwa na Tume ya uchaguzi, ni wagombea wawili pekee, ambao ni mgombea wa CCM, John Magufuli na mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu ndiyo wanaokusanya nyomi?

Hata hivyo nimempa "advantage" Tundu Lissu ya kushinda uchaguzi huu, kwa kuwa katika mikutano yake hakuna vivutio vya wasanii, kama ilivyo kwa ndugu zetu wa CCM...................

Wala kujazwa mikutano hiyo na watoto wa shule, wafanyakazi "wanaolazimishwa" kuhudhuria mikutano hiyo, wala kuwaleta wafuadi hao kwa mabasi na malori ya kukodistwa!
 
Wakati umewadia wa salamu za wagonjwa tunawapa pole. Ajuae ni Mwenyezi Mungu kwa mgonjwa kuwa salama na mzima kuwa mfu tunawapa pole. Wagonjwa mahospitalini tunawapa pole.
Wagonjwa majumbani tunawapa pole.

Hemu toa hiyo avatar maana inanizuia kusomanga ujumbe na comment Zako!
 
Nafikiri JPM atakuja na some kind of deal hususani kwa Mbowe, nahisi JK na Mbowe watakaa chini watakuja na Compromise.

Na nahisi Compromise itakuwa kwenye katiba mpya, kwamba wamuachie JPM amalize muhula wa mwisho ila wao CDM waongoze mchakato wa kubadili katiba ila Uchaguzi wa 2025 uwe na tume huru etc.

Yaani hii ndio karata pekee ambayo CCM wanaweza kuicheza kwa sasa.
hiv jamaa unamjua kwel asee....hawez ruhusu hivyo...kibur hasa

Sent from my SM-J500FN using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom