Nimestushwa sana na kujaa mshangao mkubwa kwa mapokezi.makubwa sana, ambayo naweza kuyaita siyo ya mafuriko tena, Bali ni ya kimbunga na ya kihistoria aliyoyapata Tundu Lissu, jijini Mwanza, siku ya Jana, ambapo inasidikiwa kuwa yamevunja rekodi ya kupokelewa kwake, ambapo maelfu kwa maelfu, waliujaza uwanja wa Nyamagana, kumsikiliza shujaa huyu, Tundu Lissu akimwaga Sera yake, ambayo ni ya kuleta Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu.
Mapokezi hayo ameyapata huku vyombo vyote vya habari hapa nchini, vikiwa vimempa "blackout" bila kutangaza ratiba ya ujio wake!
Kilichonistua zaidi ni kuwa hapo jijini Mwanza ndipo tuliaminishwa kuwa ndiyo ngome kubwa ya mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli
Nadiriki kusema kuwa huyu Tundu Lissu, kwa hivi sasa, hakuna mtu anayeweza kumzuia kufikia azma yake ya kuwa Rais wa 6 wa nchi hii, katika uchaguzi mkuu ujao!
Kama alivyosema, mtumishi wa Mungu, Augustine Mwingira kuwa, huyu Tundu Lissu, hajajenga mafly overs wala hajajenga SGR, hajajenga chochote ndani ya nchi hii,lakini kila anapokwenda, watu maelfu kwa maelfu wanamfuata!
Ndipo hapo Mwingira alipomalizia mahubiri yake kwa kusema kuwa I DON'T UNDERSTAND THIS!
Nami na watanzania wenzangu ni lazima hivi sasa tujiulize hivi hii hali ya kupendwa kupita kiasi kunatokana na nini, kama siyo kuinuliwa kwa njia ya muujiza na Mungu mwenyewe, kutokana na mapitio aliyopitia huyu Tundu Lissu kwa kumwokoa na zile "mvua" za risasi, ambazo watesi wake, waliamini kabisa kuwa zitakuwa "zimeshammaliza" lakini kwa muujiza mkuu wa Mungu, hadi Leo anatembea huku akiwahubiria upendo watanzania wote na kuwa hana nia ya kulipiza kisasi na atakuwa amesamehe mara saba mara sabini kwa yote aliyopitia!
Hiyo ni kuthibitisha kuwa mawazo yetu sisi binadamu na tunachopanga, sicho kinachopangwa na Mungu wetu
Mungu ibariki Tanzania na endelea kumjazia baraka zako mja wako Tundu Lissu