Imani? Imani kwenye siasa za ushindani?
Lisu ni kidagaa! Ataprove hilo oktoba 28
Siyo tu ni kidagaa, Lissu ni hamnazo kwa kuwa hajui kuwa anaowasimulia porojo zake wanajijua. Km leo Kanda ya Ziwa anawakumbusha wavuvi kuchomewa nyavu kana kwamba ni jambo jipya. Asilolijua ni faida iliyopatikana kwa hatua hiyo. Sasa hivi aina na kiwango cha samaki wanaovuliwa wavuvi na walaji wanashukuru.
Anawaambia wafanya biashara ndogo kuwa bei ya vitambulisho ni ya kinyonyaji. Wahusika wamemjibu faida ya vitambulisho hivyo.
Anaishitumu Serikali kwa uwongo ati wajawazito wanatozwa kodi. Kwa kuwa yeye si mwanamke wala hana mjamzito hajui kuwa huduma yao imeboreshwa maradufu.
Anachukua nafasi ya wafanya biashara na kudai wengi wamefunga biashara. Kwa kuwa hakuwa nchini muda mrefu, na hasa wakati wa korona, kushuhudia Taifa likijitegemea kwa mahitaji yote kutoka kwa biashara ya ndani.
Hakika, mfa maji hutapatapa maana angalau angewauliza wagombea wa chama chake (wabunge + madiwani) kero na mahitaji ya wakazi wa maeneo husika ili porojo zake angalau ziwe na uhalisia.
Nilisema awali kwamba, baada ya kampeni zake za kashfa, lawama na dharau, anawachia wagombea wa CCM kazi nyepesi ya kuomba kura. Wanachofanya ni kutoa ushahidi ulio wazi kujibu tuhuma hizo. Na hili linafanyika kwenye Kata, nyumba kwa nyumba (ya mvuvi, mfanya biashara ndogo, mja mzito, mfanya kazi, nk).
Kwa upande wa wagombea wa chama chake wanakuwa na mtihani mgumu wa kutetea tuhuma alizozisema Boss wao. Humu JF wafuasi wanashangilia ushindi wa nyomi, kama siyo ujuha ni ni upotoshaji wa kitoto (sifa ya Mpumbavu na Lofa).