Bado wanamawazo na mipango ya kuwaengua wagombea uchaguzi wa kiti cha Uraisi kutoka ACT na Chadema.kila nikipiga mahesabu naona hizi mbinu zipo ,tatizo bado kunasubiriwa wakati muwafaka ,na kama mnaona sasa kuna majaribu yanarushwa ila kinachowashangaza kuna komando mmoja hawamuoni kwenye majukwaa,wanasubiri vihabarishi kujua msimamo wa komando huyu na yupo wapi na watamtega kivipi maana hawamwoni popote zaidi ya kwenye twitter na kila wanapochokonoa na kubahatisha majibu ni sifuri.
Sasa wanajaribu kumuweka Lissu kwenye kona waone kama kuna kauli itatoka kuhusiana na komando alieko pembeni akiangalia Tundu anavyowapelekesha CCM,kama hawa makomando wawili wangekuwa uwanjani basi kila mmoja angetafutiwa mtego na kuenguliwa by red card ndani ya uwanja.Ukimya wa mmoja umewaweka CCM kamati ya mipango ya wizi sehemu ngumu sana.
Makomando msije mkaingia tamaa na kuona uwanja mweupe endeleeni na style hio hio ,adui bado yupo mawindoni.