Kysema Kweli, miaka miwili mitatu iliyopita hali ya upinzani ilikua tete,?wabunge na madiwani wengi “walijiuza”, ili kujenga destiny zao, Lowasa alibanwa mbavu hadi akasahau unabii wa TB Joshua! Sumaye akaonyesha ubinadamu wake, hapo tukiwa hatunaye Lipumba! Membe akanyimwa form, ikaprintiwa moja tu!
Silinde na Mwambe wakaenda kuponya maumivu yao, na Lijuha-likali, akaenda mbali sana, masikini mtoto wa watu akakamua kamasi lote na mchozi mzito tu!! Hata kupigwa kwa Mbowe ikaamuliwa ni ulevi tu!
Nani angejua kwamba, hata Lisu mwenyewe angeweza kuamsha dude? Uchochezi ungekua kosa, Lisu angekua mkosaji, maana kwa ukweli ametuchochea kuimaliza CCM. Lissu ameliamsha taifa na kuleta vugu vugu la mabadiliko.
Mabadiliko ya Lissu ni ya kudumu kwa sababu ni mpinzani asiye toka CCM kinyume kabisa na ile kasumba kwamba upinzani wa kweli utatoka ccm! Eti kwamba CCM ni kila kitu, watawale wao na wafanye upinzani wao!! Eti hata hotuba za upinzani waediti kwanza!
Lala kwa mkono wa buriani, CCM! Kuna waliokupenda nasi tulikuchukia sana, lakini sasa, kaburi limekupenda zaidi, linakusuburi 28, October, 2020