Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Ni huyu mgombea wa chadema ambae kwa mshangao wa wengi, haikutarajiwa kama angevutia watu katika mikutano yake hata kufikia kiwango cha mitaa kufungwa. Je ni kwa vile tu alipigwa risasi 16 akapona, au kuna siri nyingine!?
 
Siri ni kwamba Lissu ni mshindi.Kushindana na mshindi ni unapoteza muda wako tu
 
limenishangaza hata mimi
cha ajabu hata mabango huko barabarani hana watu wanapata taarifa tu kupitia social media kwamba kesho atakua sehemu fulani...
 
Watanzania wana tabia ya kushangaa shangaa.

Hata ubalozi wa Marekani uliporipuliwa walikimbilia kwa maandamano kwenda kushangaa kadhalika lori la mafuta liliporipuka pale Morogoro!
 
Watanzania wengi wanahitaji matumaini,furaha, haki,kuthaminiwa na amani.
 
Niliumia nilipomsikia Lissu akiwakemea polisi kwa kuwaita "mapolisi wajinga". Hawa ni wenzetu wanapata shida hizi hizi tunazohitaji ziondolewe kwa njia ya kura. Hata wao wangependa maisha bora zaidi.

Tatizo ni kwamba wao wako kwenye ajira hiyo ya upolisi kama wewe ulivyo kwenye ajira ya uwakili, na wengine walivyo kwenye ualimu, umachinga, kilimo nk. Shida zetu ni zilezile. Wabaya wetu ni walewale.

Usigombane na polisi, na tena tafadhali sana usiwagombeze vile, utasababisha waone kuwa hakuna nafuu kati yako na yule, actually huenda wakasema yule ana unafuu kwa vile anawalipa mshahara, yale mambo ya "zimwi likujualo....."

Unapohutubia jukwaani, hawa polisi ni miongoni mwa hadhira yako, ni miongoni mwa walengwa wako katika mabadiliko, unataka kura zako pia, na tena nikuhakikishie sana kuwa nao wanatamani sana unafuu wa maisha upatikane. Hiyo mambo ya uhuru, haki na maendeleo ya kweli hata wao wanataka. Ongea nao vizuri, waeleze utakavyowasaidia iwapo utachaguliwa.

Pambana na JPM ndiye level yako kwa sasa (kwa maana ya mgombea mwenzako), usijishushe kwenda kugombana na watumishi wake.

Ikiwezekana tafuta muda uwaombe radhi wale waliokwazika, waambie ilikuwa bahati mbaya na usirudie. Wape ahadi nzurinzuri, tena wape ahadi nzuri kuliko za yule mpinzani wako.

Nasema hivi, stay focused, don't bark at the wrong tree. Fight at your level. Keep the composure.

All the best.
 
Niliumia nilipomsikia Lissu akiwakemea polisi kwa kuwaita "mapolisi wajinga". Hawa ni wenzetu wanapata shida hizi hizi tunazohitaji ziondolewe kwa njia ya kura. Hata wao wangependa maisha bora zaidi...

Umempa ushauri mzuri ila chamdomo watakuja hapa kukutukana badala ya kutoa hoja. Hoja kama hizi huwa hawataki kuoziona
 
Kysema Kweli, miaka miwili mitatu iliyopita hali ya upinzani ilikua tete,?wabunge na madiwani wengi “walijiuza”, ili kujenga destiny zao, Lowasa alibanwa mbavu hadi akasahau unabii wa TB Joshua! Sumaye akaonyesha ubinadamu wake, hapo tukiwa hatunaye Lipumba! Membe akanyimwa form, ikaprintiwa moja tu!

Silinde na Mwambe wakaenda kuponya maumivu yao, na Lijuha-likali, akaenda mbali sana, masikini mtoto wa watu akakamua kamasi lote na mchozi mzito tu!! Hata kupigwa kwa Mbowe ikaamuliwa ni ulevi tu!

Nani angejua kwamba, hata Lisu mwenyewe angeweza kuamsha dude? Uchochezi ungekua kosa, Lisu angekua mkosaji, maana kwa ukweli ametuchochea kuimaliza CCM. Lissu ameliamsha taifa na kuleta vugu vugu la mabadiliko.

Mabadiliko ya Lissu ni ya kudumu kwa sababu ni mpinzani asiye toka CCM kinyume kabisa na ile kasumba kwamba upinzani wa kweli utatoka ccm! Eti kwamba CCM ni kila kitu, watawale wao na wafanye upinzani wao!! Eti hata hotuba za upinzani waediti kwanza!
Lala kwa mkono wa buriani, CCM! Kuna waliokupenda nasi tulikuchukia sana, lakini sasa, kaburi limekupenda zaidi, linakusuburi 28, October, 2020
 
Ndugu zangu,

Sisi wengine huwa kila siku tuna kitu cha kununua iwe madukani au sokon.Jana ndugu yetu Tundu Lissu alionekana viunga vya kariakoo akinunua maembe. Je, hana kingine cha kununua?akumbuke Dar kuna masoko mengi sio kariakoo pekee. Mtu haishi kwa maembe tu kuna mahitaji mengine mengi ambayo kimsingi angweza kwenda hata soko la Tegeta Nyuki.

Pia ninamkumbusha akapande treni ya "Mwakyembe" ili aje atuambie je barabara ya mwendokasi na reli ni maendeleo ya watu au vitu?

Nawasilisha


FB_IMG_16021517377590271.jpeg
 
Kaka yetu sisi tunakushauri tu tumia lugha vizuri kwenye kampeni zako, usiseme uwongo.

Hili swala la kuzusha wakurugenzi wamekutana na Rais, tunajua uliingizwa chaka kwa kutumiwa meseji watu wakupime weledi wako, na wewe bila kutafakari ukawaambia wafuasi wako kitu kilichokuingiza kwenye adhabu.

Tunakushauri chunga kauli zako tumia siku zilizobaki vizuri uongeze kura, hali si shwari mtaani unaweza kukosa hata wabunge wawili.

Pia jiepushe kufungiwa tena, you have to grow up brother.
 
Kufikia oktoba 28 ufahamu utakuwa umekurudi na utampigia kura Mhe.Lissu. Nafsi inazidi kukusuta kupingana na mpango wa Mungu.
#UhuruHakiMaendeleoYaWatu
 
Kaka yetu sisi tunakushauri tu tumia lugha vizuri kwenye kampeni zako, usiseme uwongo.

Hili swala la kuzusha wakurugenzi wamekutana na Rais, tunajua uliingizwa chaka kwa kutumiwa meseji watu wakupime weledi wako, na wewe bila kutafakari ukawaambia wafuasi wako kitu kilichokuingiza kwenye adhabu.

Tunakushauri chunga kauli zako tumia siku zilizobaki vizuri uongeze kura, hali si shwari mtaani unaweza kukosa hata wabunge wawili.

Pia jiepushe kufungiwa tena, you have to grow up brother.
Hatuhitaji ushauri toka kwa wauaji
 
Back
Top Bottom