Habari wanajf, kama ilivyo kawaida yangu kuelezea kinagaubaga habari za mgombea wetu lissu.
Chadema tulikuwa na ngome nyingi sana ambazo tuna uhakika kama mashambulizi yakifanyika basi tutapata kura nyingi sana.
Lakini katika hizo ngome ninaona kabisa mwaka huu hali haipo vizuri kwa kuwa mapokezi ya mgombea wetu hayakuwa mazuri kabisa.
Mfano siku ya jana mgombea wetu alitakiwa kufanya mkutano kwenye jimbo la chalinze, lakini nimeshtushwa sana muitikio wa watu kwenye mkutano.
Inawezekana watu wa chalinze hawakupata habari au basi tu wameamua kutupuuzia.
Mkutano ulipangwa ufanyike saa 6 mchana, lakini cha kushangaza kabisa hadi muda huo kulikuwa hakuna watu kabisa uwanjani jambo ambalo pengine lilipelekea mgombea wetu kuhairisha kufanya mkutano hapo chalinze.
Ila ninaomba chama chetu chadema waandae mkutano mwingine hapo chalinze na watu wajulishwe mapema sana, matangazo yawepo kila sehemu ili kuvuta watu wengi waje kwenye kampeni zetu, bila kufanya hivyo tutakuwa tunapaka rangi upepo.
Chama kinatakiwa kufanya maandalizi makubwa ya mikutano ili kuondoa aibu tunazopata, mfano leo mgombea wetu yupo morogoro lakini hadi sasa hivi hakuna kinachoendelea huko morogoro.
Chini hapa ni picha za hali ilivyokuwa chalinze, watu walikuwa wachache tu ambao ni viongozi tu wa chama chetu, cha kushangaza watu walikuwa wanapita mbali kabisa na eneo la mkutano kana kwamba hakuna kinachoendelea
Picha za tukio