Singida ni mkoa maskini Sana ukipita kwenda vijijini utashangaa kuona jinsi kulivyo Giza.ilongero Kijiji cha zamani hamna kitu zaidi ya majungu ukienda mbele huko vijiji vya ngamo, gh'ata hakuna umeme mpaka Singa huko mkalama hamna umeme Wala maji.
Ukija vijiji vya barabara kuu ya arusha umeme hamna.nguzo zimewekwa karibu mwaka wa pili huu sijui wanasubiri mpaka kalimani waziri aje apatie kick.vijiji vya bonde la ufa hamna kitu umaskini umejaa. Ukija mjini mpaka Wana nchi wamemkataa mbunge sima kwa kuwa hamna maendeleo zaidi ya taa za barabarani na lami mpya mitaa michache haizidi hata mitatu, Mungumaji tu yenyewe haina umeme na iko ndani ya manispaa aibu sana.
Haya sasa Lissu amejitokeza ndugu yenu kabisa msimuache hivihivi mpeni kura zenu mtoto wa homeboy. Singida inapaswa iende mbele Sana inaunganisha majiji Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma ni mkoa muhimu katika uchumi hasa kwenye usafirishaji ila umeachwa nyuma sana hauna hadhi.
Mwisho kabisa viongozi wa singida rekebisheni jengo lenu la CCM na jengo letu la TRA lipigeni rangi liwe na muonekano mzuri.