Nategemea Lissu atashinda, ila Sina uhakika Kama atatangazwa. Vyovyote itakavyokua Lissu ataingia kwenye kumbukumbu Kama mgombea Urais alieshinda kwa mbinde. Lissu anagombea wakati Vyombo vya habari vinatishwa visitangaze habari zake hasa za kampeni, Lissu anafanyiwa kila aina ya hujuma.
Lissu hana hata bango moja barabarani lakini Bado anapata watu wengi kumsikiliza. Magazeti ambayo yangekua yanaripoti habari zake yalifungiwa mapema, kimkakati. Mfano Tanzania Daima.
Habari za Lissu huwezi kuzipata kwa undani kwenye TV na radio lakini watu wanajazana kwenye mikutano yake. Kitu Cha ajabu mgombea wa CCM, TBC wanarusha mambo yake tokea asubuhi lakini Lisu hapati fursa kama hiyo, lakini watu wanajaa kwenye mikutano yake.
Hata hivyo kubwa kuliko ni kwamba Lissu wa CHADEMA ndio mgombea Urais wa Tanzania ambae habari zake zinatawala sana kwenye mitandao ya kijamii. Hii yote inaonesha kuwa Lissu anakubalika zaidi na Vijana wasomi, wasomi na watu wenye ufahamu wa Juu wa TEHAMA na wenye kipato cha kati na kuendelea.
Pia Lissu habari zake zinatamba sana mitandaoni kwa sababu vyombo vingine vya kawaida vimepigwa biti. Hata hivyo mitandao ya kijamii ndio njia za mawasiliano na kupashana habari za kizazi kipya na tayari imekwisha ifunika Vyombo vya habari vya zamani.
Hitimisho: Tundu Lissu katawala media na kama magazeti Redio na tv zingekua huru kuripoti habari za Lissu Kuna mgombea asingesikika.
Magazeti yangeuza Sana habari za Lissu.