Ni kweli ndugu,tulikuwa tunasikia mabarabara,madaraja sijui mandege,sasa hivi ukimwambia mtu habari hizi unaonekana kituko
 
Hata magazeti bila lisu ayauzi nashangaa wale sijui umoja wa wahariri waliorubiniwa kususia habari za CDM, wasuse walala njaa wakafungie vitumbua magazeti yao.
Wakati ni ukuta alishasema Nyerere thus aling'atuka kulinda heshima
 
Lissu ndo habari taaamu kusikikiza na kufuata. Watu walikata tamaa ya uchaguzi huu. After the arrival of The GAME CHANGER everything turned well. Asant mungu
 
Mtaji wa fisiemu ni wajinga na wenye kipato cha chini hicho ndio wanajidaia sana ila Dunia inaenda kasi karibuni watu watajitambua na kumuondoa mkoloni mweusi kwenye utawala
 
Kura hazipigwi kwenye mitandao ya kijamii comrade unakwama wapi?
 
#Ni yeye , Tundu A Lissu ndio anauzika hapa Tanzania kwenye Chaguzi za mwaka huuu 2020 kuliko habari yoyote ile.
Farhia Middle, Leo ameanza na Habari pendwa ya Tundu Lissu,

Uzi tayari.
Tayari uzi,pathetic
 
Anajua kuvutia watazamaji, wameifanya ITV ianze kupendwa tena, hasa baada ya yale mahojiano kati ya Lissu na Farhia.
ITV imejiongezea watazamaji Mara dufu, Heko ITV ile kauli ya tume kuhusu usawa katika habari za uchaguzi katika kila chama imekuwa ahueni.
 
Nikiri wazi kwamba tangu Tundu Lissu arejee na kupitishwa na tume ya taifa ya uchaguzi ameweza kubadilisha upepo wa siasa hapa nchini.

Nimefuatilia kampeni za CCM na CHADEMA tangu kampeni zianze nimejifunza mambo yafuatayo

1. Tundu Lissu ni shujaa ana uwezo wa kujenga hoja na kushawishi watu na jamii imemkubali sana, hali ambayo imemfanya aombe mdahalo na mgombea uras wa CCM huku akijua kabisa MTU wa CCM hawezi kukubali mdahalo.

2. Mgombea urais wa CCM anafanya kampeni zake kwa hasira na kufokafoka kwani bado hajaamini jinsi watu wanavyomkubali Tundu Lissu.

3. CCM INA hofu na Tundu Lissu tu na sio vyama vingine rejea hotuba zote za mgombea urais amejikita kujibu hoja za Lissu tu na si wagombea wa vyama vingine.

4. CHADEMA inafanya kampeni katika mazingira magumu sana kwani mikutano yake haiko mubashara kama ya chama tawala.

Hongera Tundu Lissu kwa kubadili upepo kwa kasi Kubwa kiasi cha kumfanya mgombea wa chama cha mapinduzi kutokulala na kuwakuwaza Lissu tu. Rejea totuba za Magufuli. Hongera sana Lissu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…