Tatizo siyo wao . Wamewekewa mtutu kisogoni mwa miradi yao (tcra)
 
Hizo media zimpe attention kafanya nini?. Kuwasema vibaya viongozi wako,ni jambo la kizalendo?. Sidhani kama media yoyote smart inaweza kufanya unavyofikiri.
Wagombea wapo wengi,sio lazima kuweka habari za Lissu kila mara.kwani Lissu ni nani mpaka kila siku na yeye awepo kwenye habari.kalifanyia nini hili taifa la Tanzania mpaka apewe umuhimu kama mnavyotaka nyinyi.
Wote watatu mnawakilisha akili za kishetani zinazowasumbua watu wa Ccm. Hiki ni kipindi cha campaign. Mgombea kupewa nafasi ya kuwafikia watu ni pamoja na kupewa nafasi kwenye vyombo vya habari.

Huyo wenu tangu 2016 amepewa kavareji hata akishiriki ibada. Lakini haijawafanya WaTz wawasahau wapinzani wake . Hata kwenye campaign hizi atangazwe peke yake lakini bado ushindi wake ni wa kutengeneza na kulazimisha
 
Ukweli ni kwamba magu hapendwi kabisa hata ndani ya ccm ni unafiki tu umejaa watu wanatafuta upenyo.
 
Hata Lissu akikesha kwenye media anaongea,lakini ukweli ni kwamba hawezi shinda uchaguzi.
ondoa robo ya kura za CCM kisha apewe Lissu bado hawezi shinda.kupewa nchi ni zaidi ya kupiga kura.umenielewa bwana Omera?.
 
Hata Lissu akikesha kwenye media anaongea,lakini ukweli ni kwamba hawezi shinda uchaguzi.
ondoa robo ya kura za CCM kisha apewe Lissu bado hawezi shinda.kupewa nchi ni zaidi ya kupiga kura.umenielewa bwana Omera?.
Sasa campaign na uchaguzi wa nini kama kura hazina maana ?!.

U communist ni laana ktk nchi yoyote duniani. Nchi zote zilizofanikiwa duniani ni zile za ki democracy ya kweli .
 
Hizo ni media za Fisiemu, ni sehemu ya Mfumo kandamizi, tunapambana nao pia
 
"Kiongozi akiwa bora sio wa kubadilisha kama nguo" mwalimu nyerere ,kila vyombo vya habari vinahepuka hilo.
 
CHADEMA tumewaomba sana mtutafutie TV moja itakayokuwa inarusha mikutano ya Lissu lakini paka sasa bado mnasuasua, Kama TV za hapa zinaogopa kurusha mikutano ya Lissu basi nendeni Kenya, kwenye dstv yenyewe kuna channel zaidi ya tano za Kenya zinazoonekana hapa nchini.

Kama tatizo ni pesa, basi semeni ili tuongeze michango, Ikibidi hata muwe mnawarushia recordings tu wazioneshe tumwone kamanda wetu.Tunataka sasa na sisi kusikia Sera za Tundu Lisu , na si kila siku ukifungua TV ni rangi ya mboga mboga, Magazeti yote nayo ni mboga mboga, redio ndo usiseme, yani paka imekuwa kero sasa hivi watu hawataki hata kutazama TV bora waweke movies waangalie.

Sasa tunasema Tumechoka, CHADEMA tafuteni TV hata ya nje ioneshe kampeni. SI OMBI, NI LAZIMA.
 
Sasa campaign na uchaguzi wa nini kama kura hazina maana ?!.

U communist ni laana ktk nchi yoyote duniani. Nchi zote zilizofanikiwa duniani ni zile za ki democracy ya kweli .
Demokrasi ya kweli utaipata wapi duniani?,Trump amewaonya Democracy wasijaribu kucheza na sanduku la kura,kuna kitu ameona ndo maana akatoa onyo sembuse africa?

Hata ndani ya Chadema hakuna demokrasia ya kweli ni uhuni tu umejaa.
 
Demokrasi ya kweli utaipata wapi duniani?,Trump amewaonya Democracy wasijaribu kucheza na sanduku la kura,kuna kitu ameona ndo maana akatoa onyo sembuse africa?.
hata ndani ya Chadema hakuna demokrasia ya kweli ni uhuni tu umejaa.
Kule kwa kina Trump , Taasisi za kusimamia chaguzi zina nguvu kuliko Rais au mtu yeyote. Matamshi yake hayana maana ktk process zao za uchaguzi . Na ndiyo maana yeye (Trump) alimshinda mgombea wa chama tawala wakati huo 2016 . Kwa hiyo mkwara wake hauna maana .

Kwetu hapa mgombea anawateulia tume ya uchaguzi !!. Kichekesho na dhihaka ktk mfumo wetu wa uchaguzi
 
Nakubaliana na wewe,demokrasia yetu bado ni changa sana,mpaka ndani ya vyama kama CCM,Chadema,Cuf n,k.
mfano Chadema ukitaka nafasi ya mwenyekiti yatakupata kama yaliyowapata wakina Chacha Wangwe,Cecil Mwambe na Zito Kabwe.hivyo hivyo kwa vyama vingine.

Lowasa alinunua nafasi ya kugombea urais Chadema 2015 kwa pesa zake akupata kwa mchakato wa kidemokrasia.
Kwahiyo kwa siasa zetu hizi Chadema kupata nchi msahau kabisa.mpaka demokrasia ikomae ndani ya vyama na nje ya vyama.
 
Hizo media zimpe attention kafanya nini? Kuwasema vibaya viongozi wako, ni jambo la kizalendo? Sidhani kama media yoyote smart inaweza kufanya unavyofikiri.
Ni Tanzania pekee mtu anatukana viongozi, watendaji wa serikali , vyombo vya usalama, taasisi zote na bado akaruhusiwa kugombea Urais.
 
Uchaguzi wa mwaka huu 2020 unaonekana utakuwa mgumu sana kwa CCM ya Magufuli. Kuingia kwa Mhe. Tundu Antipas LISSU kwene kinyang'anyiro hiki kumebadili na kupandisha joto la Uchaguzi kwa kiwango ambacho hakikutarajiwa kabisa.


Watz mamia kwa maelfu wanahudhuria mikutano ya Kampeni za Mhe. Lissu kiasi Cha kupelekea kiwewe, hofu na pressure kwa Magufuli, CCM na Serikali yake.

Huu ni Ushahidi tosha kuwa this time around things won't be the same again come 28 October, 2020.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…