Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na Salum Mwalimu
Haya ni baadhi ya tathmini yangu
1.Hajaweka sera za Chadema zikaeleweka kwa wananchi hadi sasa
2.Anajinadi yeye zaidi sio chama au wabunge na madiwani
3.Anamzungumzia zaidi Dr Magufuli badala ya kuelezea atakachofanya yeye na chama chake wakishika dola
4.Anachukua vitu vingi humu jamii forums na kuviundia hotuba kwa asilimia 90 ya hotuba zake source ni jamii forums
5.Mahudhurio kwenye mikutano yake bado ni changamoto ni madogo
6.Anapokelewa kwa mbwembwe anapowasili kwa mapikipiki nk lakini ikifika wakati wa kuondoka anaondoka peke yake kama mwanga na wenye pilipiki wakimfikisha tu wanambwaga wala hawakai mkutano
7. Kwa kukosa viongozi wa dini kwa kutomuunga mkono kila anakoenda anazunguka na Askofu Mwamakula mjanja wa Dar es saalam kumsaidia kupiga dua hewa walau ionekane viongozi wa dini wako naye
8.Mikutano yake anaigeuza kama darasa badala ya kampeni analigeuza darasa la historia alizosoma HGL na sheria alizosoma chuo kikuu
9.Hoja ya maendeleo ya watu na sio vitu hadi sasa imemshinda kuitetea kwenye kampeni
10.Hafichi chuki yake kwa watu wa kanda ziwa
11.Hadi sasa hana uhusiano mzuri na vyombo vya ulinzi,vyombo vya habari,tume ya uchaguzi
12.Hana hela na kitendo cha kuchangisha kinawaudhi wanaotakiwa kuchanga .Hasira zao wengi wanazionyesha kuondoka mkutanoni mapema
13.Hana nyota ya mvuto hata akipita njiani na magari yake watu hawaoni kama kuna mtu mgombea uraisi anapita
14.Hajui kupanga point anapoongea.Hana mpangilio unaoeleweka na hivyo kusababisha akimaliza kuhutubia hujui hata aliongelea nini
15.Hana support ya watu wazima kwenye chama mikutano yake haijai watu wa aina zote ina na wa jinsia zote wengi unakuta ni vijana tena wa kiume ukiona mwanamke ni wa kumulika na tochi na watu wazima kuwaona ni shida ni mmoja mmoja tu
17.Kitengo cha uchakachuaji picha cha Chadema kimeharibu credibility ya Mikutano kiasi kuwa picha na video zao wanazorusha haziko credible tena hasa za mahudhurio na haziaminiwi
18.Hajali muda.Wa kufika anapotakiwa kwenye mkutano wa kampeni wala wa kuondoka
19.Hajali maamuzi ya chama chake mfano chama chake kupitia vikao vyake vya kamati kuu na mkutano mkuu vilimteua mgombea uraisi wa Chadema zanzibar yeye kufika zanzibar akaanza kumnadi Maalim SEIF
20.Majukwaa anayotumia sio presidential materia yanadhalilisha hadhi ya ugombea uraisi vijukwaa utafikiri meza ya muuza mitumba
21.Sound system iko very poor
22.Bado watu hajawakuna vizuri ana kazi kubwa ya kuwafanya wapokee hotuba zake he is not a good public speaker .Anaweza eleweka zaidi bungeni,mahakamani na kwa wasomi zaidi.Huku chini hakuwezi

Mengine ongezeni nyie
 
Ulitaka amnadi babako eti au aseme CCM oye Kama mwaka 2015 aliyafanya Lowassa?

Mwaka huu ni zamu yenu kulia lia hapa.
 
Umeshindwa kutoa tathimini ya kampeni za Mwenyekiti wako unakimbilia za upinzani
 
Rais Mtarajiwa wa Tanzania Tundu Lissu mwenye uwezekano mkubwa wa kushinda kwa asilimia 70% ya kura Jana alilakiwa kwa Shangwe Kuu na Nderemo mjini Tunduma mkoani Songwe.

Tunaweza kusema biashara zilifungwa na familia zilifunga nyuma zao kwenda kumlaki mwana huyo wa Tanzania aliyecharazwa risasi 16 kwenye mwili wake na washenzi wanaoitwa wasiojulikana Lakini kaponywa na mkono wa Mungu.

Ifuatavyo ni Video inayoonyesha jinsi Malaki ya watu yalivyomlaki na kumsindikiza barabarani Mbeba Maono huyo
 

Attachments

  • VID-20200917-WA0074.mp4
    17.2 MB
Back
Top Bottom